Ngiri (Warthog ): Naomba wataalamu watueleze Kwa kina kuhusu huyu Mnyama

Ngiri (Warthog ): Naomba wataalamu watueleze Kwa kina kuhusu huyu Mnyama

Khee! We sema eti kichwa hakipo sawa. Lakini huku mashambani, shamba la mahindi, Wakiingia shambani kwako ujue hutavuna hata mabua - wanafyagia mwanzo mwisho halafu wakishiba wanalala hapo hapo kana kwamba wanalinda walichokifanya.
Ndio ujue umeme mdogo kichwani!

Hizi story za humu zimenichekesha sana sijawahi sikia.
 
Huyu warthog ni kiazi sana,kuna clip moja alikua amekamatwa na chui, basi simba akawa ametokea akaanza kupigana na chui ili amnyang'anye kitoweo. Sasa ikabidi chui amuachie warthog wakati anapigana na simba, ajabu sasa warthog alivyoachiliwa na chui badala ya kukimbia eti akaingilia ugomvi akaanza kumtandika vichwa chui eti anamsaidia simba. Chui ikabidi akimbie halafu simba akamkamata warthog akamtafuna.
😂😂😂😂 Au chizi!
 
Huyu jamaa kwanza ni mtukutu pili asipo toka nduki ajihisi aman kabisa ndio maana clip nyingi zinamuonesha jamaa yeye ndie mkorofi yani lazima atafute sababu za kupiga kibati hapendi kuona wenzie wametulia

Kuna clip nimeona simba alikua sijui anamkimbiza sungura yule jamaa akaona usinitanie katoka mbio kawa over take simba na sungura 😂😂😂wake mpaka nikajiuliza sasa ilikua na umuhimu gani kufanya vile.
Huyo mnyama anapenda attention kinoma.
Yupo kama watu wafupi.....wanapenda attention kwenye makundi
 
Imekua kawaida kusikia vijana mtaani wanasema mwendo wa ngiri mkia juu several times...

Nukuu ya baba wa taifa.
""UTII UKIZIDI SANAA HUZAA UOGA, UOGA UKIZIDI SANA HUZAA UNAFIKI NA KUJIPENDEKEZA NA MWISHO WAKE NI MAUTI""
 
Sawa jomba. Nimeacha ubishi.
Nyama ya khanga na ya kuku zinafanana, kwa hiyo khanga ni kuku pori.
Chimpanzee anafanana na binadamu, kwa hiyo chimpanzee ni binadamu pori.
Mende akichomwa moto hutoa harufu kama ya kumbikumbi, basi kumbikumbi ni mende wa kwenye kichuguu
Hahahahahahahaahaha mkuu umeua nimecheka sana..
 
Nahisi hivyo mara zote walikuwa na kundi la mbwa na mikuki.

Niliona nyani kamwaga utumbo wa mbwa kama utani asee zile kucha na meno ni hatari sana akiwa anatetea uhai wake.
Nyani hatari sana. Anakukusanya ngozi pamoja kama mtu anavyokamua nguo halafu ndio anang'ata. Anakuochia bonge moja la jeraha.
 
Huyu warthog ni kiazi sana,kuna clip moja alikua amekamatwa na chui, basi simba akawa ametokea akaanza kupigana na chui ili amnyang'anye kitoweo. Sasa ikabidi chui amuachie warthog wakati anapigana na simba, ajabu sasa warthog alivyoachiliwa na chui badala ya kukimbia eti akaingilia ugomvi akaanza kumtandika vichwa chui eti anamsaidia simba. Chui ikabidi akimbie halafu simba akamkamata warthog akamtafuna.
Wanasema anasahau haraka sana kupita wanyama wote huenda aliwasahau kuwa Hawa wote ni waganga njaa tu hakuna msaada wowote
 
Samahani naomba kukuuliza,hivi Warthog na wild boer ni wanyama wawili tofauti?
 
Back
Top Bottom