Ngiri (Warthog ): Naomba wataalamu watueleze Kwa kina kuhusu huyu Mnyama

Ukisikia boda anakwambia, hapa ni mwendo wa ngirii, mkia juu achana naye. Huyo jamaa anapita katikati ya kundi la simba hadi simba wanatawanyika wanabaki wanashangaa nini kimepita hapa.
Sema akishikwa anapiga kelele unaweza muonea huruma
Jamaa ana confidence sana haogopi kitu
 
Khee! We sema eti kichwa hakipo sawa. Lakini huku mashambani, shamba la mahindi, Wakiingia shambani kwako ujue hutavuna hata mabua - wanafyagia mwanzo mwisho halafu wakishiba wanalala hapo hapo kana kwamba wanalinda walichokifanya.
🤣 🤣 🤣
 
Ngiri ndiye mwanzilishi wa klabu za joging'i Tanzania wakati huo akiishi Gongolamboto, Pugu na Kisarawe alkokua analima mihogo. Wale wanachama wa Mzimuni Joging'i Klabu mnatakiwa mumpe heshima zake.
 
Wanyam wawili ninaopenda kuangalia clips zao ni huyo worthog na Honey burger a.k.a Mr die harder...
Huyu naye shoo yake sio ya kitoto..
Sio tuu hafi kinyonge, huko kumuwinda tuu ujipange, asilimia kubwa atakuacha na ngeu, yeye akitokomea kusikojulikana..
Wewe kiumbe ambaye chakula chake kikubwa ni Nyoka hasa Black mamba na Cobra unamchukuliaje..
 
Kweli kabisa huyu nae mtiti wake sio wa kitoto. Wanasema hata panga ukimkata haiingii. Pia nasikia akifika kwenye mzinga akiachia ushuzi tu nyuki wote wanalewa anajilia asali atakavyo. Anaitwa nyegere kiswahili kama sijakosea
 
Ngiri ndiye mwanzilishi wa klabu za joging'i Tanzania wakati huo akiishi Gongolamboto, Pugu na Kisarawe alkokua analima mihogo. Wale wanachama wa Mzimuni Joging'i Klabu mnatakiwa mumpe heshima zake.
Kisarawe walikuwepo wengi sana sijui Kwa sasa. Siku ya kwanza nilikuta meno yake na baadhi ya mabaki ya mifupa nikayachukua nikauliza wenzangu wakasema huyo ngiri kafa miaka mingi sana. Wakasema huko kwetu bara ni diri ila huwezi peleka ukikamatwa maisha!!
 
Hii ni misconception iliyotokana na kujua ķuwepo kwa nguruwe pori. Watu wanafikiri nguruwe pori ndiyo ngiri.

Ukweli ni kuwa ngiri (Warthog) sio nguruwe pori. Na Boar (nguruwe pori) sio ngiri. Boar ukigoogle picha zake, utaona ni nguruwe kabisa.
Acha ubishi huyo ni nguruwe pori tuliomla tunajua ngozi sio pana sana ,nyama mpk harufu ya nguruwe na mafuta anayo
 
Mpaka miaka ya 80 walikuwa wanaonekana Gongolamboto maeneo ya kiwanda cha KILITEX na kule kwenye machimbo ya Pugu, sasa hivi wapo Saadani Bagamoyo mitaani, usiwaogope ukipishana nao wao wako bize wanajogi.
 
Acha ubishi huyo ni nguruwe pori tuliomla tunajua ngozi sio pana sana ,nyama mpk harufu ya nguruwe na mafuta anayo
Sawa jomba. Nimeacha ubishi.
Nyama ya khanga na ya kuku zinafanana, kwa hiyo khanga ni kuku pori.
Chimpanzee anafanana na binadamu, kwa hiyo chimpanzee ni binadamu pori.
Mende akichomwa moto hutoa harufu kama ya kumbikumbi, basi kumbikumbi ni mende wa kwenye kichuguu
 
Kweli kabisa huyu nae mtiti wake sio wa kitoto. Wanasema hata panga ukimkata haiingii. Pia nasikia akifika kwenye mzinga akiachia ushuzi tu nyuki wote wanalewa anajilia asali atakavyo. Anaitwa nyegere kiswahili kama sijakosea
Honey badger nasikia hata haja kubwa huwa hajisaidii hovyo,kama ni Temeke ni huko huko,hata akibanwa akiwa Kimara anaweka furushi la majani kuziba isitoke anarudi Temeke kujisaidia,ukitaka kuprove hili nenda sehemu anapojisaidia lazima ukutane na mafurushi ya majani yaliosokotwa...
 
Kuhusu Hilo sijui ila najua anaye fanya hivo Mnyama fln anaitwa fungo.
 
Mang'ati na wasukuma kule pwani walikuwa Wana waua Kwa mbwa lakini walikuwa wanatumia hasa mikuki mara kadhaa nimewasadia kumbeba Hadi kambini wateja wanakuja kuchukulia pale.
Ili mbwa aweze kum'mudu huyo Mwamba ni lazima mbwa wawe wengi halafu na huyo mwamba awe ameshachoka sana. Vinginevyo hilo timbwili ni la kiwango cha lami.
 
Ili mbwa aweze kum'mudu huyo Mwamba ni lazima mbwa wawe wengi halafu na huyo mwamba awe ameshachoka sana. Vinginevyo hilo timbwili ni la kiwango cha lami.
Nahisi hivyo mara zote walikuwa na kundi la mbwa na mikuki.

Niliona nyani kamwaga utumbo wa mbwa kama utani asee zile kucha na meno ni hatari sana akiwa anatetea uhai wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…