Ngiri (Warthog ): Naomba wataalamu watueleze Kwa kina kuhusu huyu Mnyama

Exactly yes. Ni mtunzaji mzuri wa mazingira. Lakini pia ni hulka (instict)yake hiyo.
 
πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜… Tufanye nguruwe wapo aina tatu wakisasa ,hao wako na Ngiri pori wote jamii moja
 
Huyu warthog ni kiazi sana,kuna clip moja alikua amekamatwa na chui, basi simba akawa ametokea akaanza kupigana na chui ili amnyang'anye kitoweo. Sasa ikabidi chui amuachie warthog wakati anapigana na simba, ajabu sasa warthog alivyoachiliwa na chui badala ya kukimbia eti akaingilia ugomvi akaanza kumtandika vichwa chui eti anamsaidia simba. Chui ikabidi akimbie halafu simba akamkamata warthog akamtafuna.
 
War-thog maana yake mtu wa vita purukushani na shari
 
Waw! Sio kwamba warthog naye alikuwa anajilipizia kisasi kwa chui? Simba naye hovyo sana. Simba alitakiwa amwache warthog kwani alimtia shime kwenye pambano. Ila ndo hivo tena. Simba angelimwacha warthog, isingekuwa vyema kwani huenda siku hiyo simba angelishinda njaa na ukizingatia Riziki haiji mara mbili. Simba alifanya maamuzi sahihi japo magumu.
 
Hii ni misconception iliyotokana na kujua Δ·uwepo kwa nguruwe pori. Watu wanafikiri nguruwe pori ndiyo ngiri.

Ukweli ni kuwa ngiri (Warthog) sio nguruwe pori. Na Boar (nguruwe pori) sio ngiri. Boar ukigoogle picha zake, utaona ni nguruwe kabisa.
Tunaita hivyo kwa vile akili zao vinafanana , ukimshika sikio wote wote wanatulia ...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…