Ngorongoro - Loliondo: Askari Polisi amekufa baada ya kupigwa Mshale mmoja tu, RC Mongella amlilia

Ngorongoro - Loliondo: Askari Polisi amekufa baada ya kupigwa Mshale mmoja tu, RC Mongella amlilia

Hili Taifa tumerogwa. Nilisema jana huyu waziri mkuu atoke tu lakini wakaja juu Sasa ona mambo yote hadharani. Siku zote njia ya mwongo nifupi. Mkuu wa mkoa wa Arusha amesema askari wao kafa kwa mshale chanzo ni vita inayoendelea Kati ya wamasai na polisi. Jana waziri mkuu alikanusha na kusema loliondo ni shwari. View attachment 2257218
Hata jamaa aliwahi kusema JPM ni mzima wa afya na anaendelea hazi. Kumbeee duhhh!!
 
Hili Taifa tumerogwa. Nilisema jana huyu waziri mkuu atoke tu lakini wakaja juu Sasa ona mambo yote hadharani. Siku zote njia ya mwongo nifupi. Mkuu wa mkoa wa Arusha amesema askari wao kafa kwa mshale chanzo ni vita inayoendelea Kati ya wamasai na polisi. Jana waziri mkuu alikanusha na kusema loliondo ni shwari. View attachment 2257218
Nyumbu bhana...kwani PM alitoa kauli hiyo muda gani na kifo kimetokea muda gani?, kauli ya PM ilikuwa mahsusi kwa clip ya juzi yake na si juzi wala jana.
 
Askari Polisi mmoja ameuawa kwa kupigwa mshale wilayani Ngorongoro mkoani Arusha wakati wa zoezi la uwekaji mpaka katika eneo la pori tengefu kwenye Tarafa ya Loliondo.

Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella akisema kwamba kifo hicho kilitokea Juni 10 alasiri, na kusisitiza kwamba kama serikali wanatambua uzalendo wa askari huyo.

Ametumia nafasi hiyo kuwataka wananchi wa Tarafa ya Loliondo wilaya ya Ngorongoro kuwa watulivu na kusikiliza maelekezo ya serikali katika zoezi la uwekaji mipaka.

Wananchi wanatakiwa na Serikali kuhama katika eneo la Ngorongoro na kwenda kuishi Handeni, Tanga ambapo Serikali itawasaidia katika kuhama. Nia ikiwa ni kuhakikisha uhifadhi endelevu katika Hifadhi ya Ngorongoro.

Baadhi ya Wananchi wa Ngorongoro hawataki kuhama katika ardhi yao ya asili kwani Wanaishi hapo kisheria na Wanatambulika.
View attachment 2257198
Tutaelewana tu
 
Kwanini Waziri mkuu anakuwa na siasa za kitoto kiasi hiki?
Kwanini aongee uongo mkubwa namna hii?
Kuna mtu aliwahi kusema msikitini, baada ya swala ya Ijumaa, kwamba; “rais wetu ni mzima, na anafanya kazi zake kama kawaida!”
 
Back
Top Bottom