Ukweli ni Kwamba , lengo la ziara ya Tundu Lissu na Chama chake , kupeleka Oparesheni 255 kwenye maeneo ya hifadhi ya Ngorongoro ilikuwa ni
kuitangazia dunia unyama wanaofanyiwa Wamasai na serikali ya Tanzania , wa kuwahamisha kwenye maeneo yao mithili ya nguruwe ama mifugo mingine .
Lissu alifahamu Jinsi viongozi walivyohongwa pesa na kukubali kuwaswaga Wamasai na kuwapeleka Handeni , na alijua kwamba aking'ang'ania ziara ile angekamatwa , na kukamatwa kwake kungeiamsha dunia kuelewa zaidi kuhusu yanayotendwa Ngorongoro ,
Mtego huu umefanikiwa kirahisi sana !
Ikumbukwe kwamba Tundu Lissu ni MTU WA 3 KWA UMAARUFU NCHINI TANZANIA tangu kuumbwa kwa Taifa hili , Wa kwanza ni Julius Nyerere , sasa unapokamata mtu kama huyu kwa sababu za kijinga kama hizi zilizotolewa na Polisi wa Tanzania , unakuwa moja kwa moja umeiamsha dunia na kuifanya ianze kuitupia Jicho Jambo hili kwa nguvu zaidi .
Lissu alijua kila kitu ila aliamua kujitoa Muhanga ili kuokoa Wamasai , Yaani ni kama Vile Yesu Kristo alivyosulubiwa Msalabani ili kuwaokoa wanadamu , Kimsingi Lissu amefanikiwa Malengo yake kwa 100% , Hii ndio tofauti kati ya Akili ndogo na Akili kubwa .
View attachment 2745271