Ngorongoro: Tundu Lissu atimiza malengo yake

Akili za Lissu ni nyingi sana mwaka 2020 alichokifanya kwa walinzi wake hasa wale binafsi walichukia mda kidogo baadae akaja kuwaambia kwa nini alifanya vile watu walibaki hoi,

ila Lissu ana marafiki pale kanisani waliobobea kwenye kulinda mageti 🤣🤣🤣🤣🫡🫡🫡🫡🫡
Alifanyaje mkuu?
 
Wako wamasai waliokubali kwenda MSOMERA HANDENI...

Lissu anawatetea "waasi" waliokataa UAMUZI WA SERIKALI....

"Operations" za serikali lini zina HIYARI ?!!!

Ingekuwa hivyo mataifa yasingepiga hatua yoyote ile....

Tumesoma kuwa OPERESHENI VIJIJI VYA UJAMAA ilibebwa vyema kiutekelezaji na watu wote.....

TUNDU LISSU AACHE HADAA ZAKE KOKO

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Hilo bwawa la umeme limesaidia nini zaidi ya kulingiza taifa hasara, umeme bado bei na bado umeme ni unakatikati hovyo. Sasa kulikuwa na tofauti gani baada ya hilo bwawa kukamilika. Umeme bado shida gharama bado zipo juu wanachafua mazingira tu na pesa zao za upigaji
Unaanzaje kuhoji uwekezaji ambao HAUJAKAMILIKA ?!!![emoji15][emoji1787][emoji1787]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Ukweli ni Kwamba , lengo la ziara ya Tundu Lissu na Chama chake , kupeleka Oparesheni 255 kwenye maeneo ya hifadhi ya Ngorongoro ilikuwa ni kuitangazia dunia unyama wanaofanyiwa Wamasai na serikali ya Tanzania , wa kuwahamisha kwenye maeneo yao mithili ya nguruwe ama mifugo mingine .

Lissu alifahamu Jinsi viongozi walivyohongwa pesa na kukubali kuwaswaga Wamasai na kuwapeleka Handeni , na alijua kwamba aking'ang'ania ziara ile angekamatwa , na kukamatwa kwake kungeiamsha dunia kuelewa zaidi kuhusu yanayotendwa Ngorongoro , Mtego huu umefanikiwa kirahisi sana !
Ikumbukwe kwamba Tundu Lissu ni MTU WA 3 KWA UMAARUFU NCHINI TANZANIA tangu kuumbwa kwa Taifa hili , Wa kwanza ni Julius Nyerere , sasa unapokamata mtu kama huyu kwa sababu za kijinga kama hizi zilizotolewa na Polisi wa Tanzania , unakuwa moja kwa moja umeiamsha dunia na kuifanya ianze kuitupia Jicho Jambo hili kwa nguvu zaidi .

Lissu alijua kila kitu ila aliamua kujitoa Muhanga ili kuokoa Wamasai , Yaani ni kama Vile Yesu Kristo alivyosulubiwa Msalabani ili kuwaokoa wanadamu , Kimsingi Lissu amefanikiwa Malengo yake kwa 100% , Hii ndio tofauti kati ya Akili ndogo na Akili kubwa .

View attachment 2745271
Naunga mkono, ni mda huko Ngorongoro kila aliepotelewa na mpendwa wake katika hamisha kupata majina yao kwa utaratibu unaofaa na kuwakilishwa
 
Hivi viongozi wa kiislam mashehe wanKuwa na elimu ya Theolojia au Falsafa?

Hapo Rwanda bila kuwa na degree au Diploma ya dini huruhusiwi kuwa kiongozi wa dini

Misikiti mingi na makanisa yamejifunga automatic kwa kukosa mashehe na wachungaji wenye elimu ya theolojia au falsafa

Hapa Tanzania naona kama mashehe wana kalili tu kuruani na kuwa viongozi wa misikiti
Ndiyo nini hiyo? Nimeshindwa kukuelewa msomi.
 
Si unaona miaka yote ya uwekezaji hilo bwawa bado halijakamilika kama sio ufisadi ni nini? Wizi wa pesa za miradi ni jambo la kawaida kwenye utawala wa maccm.
Unajuwa mkataba wa bwawa ulikadiria miaka mingapi liishe?
 
Ukweli ni Kwamba , lengo la ziara ya Tundu Lissu na Chama chake , kupeleka Oparesheni 255 kwenye maeneo ya hifadhi ya Ngorongoro ilikuwa ni kuitangazia dunia unyama wanaofanyiwa Wamasai na serikali ya Tanzania , wa kuwahamisha kwenye maeneo yao mithili ya nguruwe ama mifugo mingine .

Lissu alifahamu Jinsi viongozi walivyohongwa pesa na kukubali kuwaswaga Wamasai na kuwapeleka Handeni , na alijua kwamba aking'ang'ania ziara ile angekamatwa , na kukamatwa kwake kungeiamsha dunia kuelewa zaidi kuhusu yanayotendwa Ngorongoro , Mtego huu umefanikiwa kirahisi sana !
Ikumbukwe kwamba Tundu Lissu ni MTU WA 3 KWA UMAARUFU NCHINI TANZANIA tangu kuumbwa kwa Taifa hili , Wa kwanza ni Julius Nyerere , sasa unapokamata mtu kama huyu kwa sababu za kijinga kama hizi zilizotolewa na Polisi wa Tanzania , unakuwa moja kwa moja umeiamsha dunia na kuifanya ianze kuitupia Jicho Jambo hili kwa nguvu zaidi .

Lissu alijua kila kitu ila aliamua kujitoa Muhanga ili kuokoa Wamasai , Yaani ni kama Vile Yesu Kristo alivyosulubiwa Msalabani ili kuwaokoa wanadamu , Kimsingi Lissu amefanikiwa Malengo yake kwa 100% , Hii ndio tofauti kati ya Akili ndogo na Akili kubwa .

View attachment 2745271
Kaka usifananishe manabii wa Mungu na wanadamu wa ajabuajabu.
 
Unajuwa mkataba wa bwawa ulikadiria miaka mingapi liishe?
Mimi sifuatiliagi mikataba haramu inayolenga kuiba mali za watanzania,. Tumeshuhudia mikataba mingi isiyo na tija kwa mwananchi wa kipato cha chini zaidi ya kuwafurahisha na kuwatajirisha watawala na familia zao huku wakiacha jamii kuishi na maumivu.
 
Wako wamasai waliokubali kwenda MSOMERA HANDENI...

Lissu anawatetea "waasi" waliokataa UAMUZI WA SERIKALI....

"Operations" za serikali lini zina HIYARI ?!!!

Ingekuwa hivyo mataifa yasingepiga hatua yoyote ile....

Tumesoma kuwa OPERESHENI VIJIJI VYA UJAMAA ilibebwa vyema kiutekelezaji na watu wote.....

TUNDU LISSU AACHE HADAA ZAKE KOKO

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Kwanini wamasai wanaondolewa Ngorongoro ?
 
Back
Top Bottom