Nguvu nilizowekeza kwenye ujana wangu nakula Matunda yake sasa

Umezaliwa 1953 na umestaafu 2016, kwa hiyo ulidanganya umri wa kuzaliwa maana ulitakiwa ustaafu 2013 (miaka 60 ).
 
Watu wanauliza maswali mengi ili,kumfanya mtoa mada aonekane muongo,chukueni hiyo point itatusaidia badae ni ukweli usio pingika
Uko sahihi, watu wanachambua sana, kumbe lengo la mtoa mada ni kutukumbusha yatupassyo kufanya kabla ya uzee.

Watu wanahoji mpaka umri, ina maana wameshindwa kuona hekima iliyo katika andiko, wanatafuta kasoro pekee. Kupanga nj kuchagua.
 
Maisha ni bahati tu ndugu

Kwa umri wako naamini umeona na kukutana na watu hawa:

01).watu wenye elimu kuliko wewe
02).watu wenye juhudi kuliko wewe
03).watu wenye imani kuliko wewe
04).watu makini na wenye mipango mizuri kuliko wewe

lakini wote hao wewe umewazidi mafanikio ..unafikiri ni kwanini?

Wewe una bahati kuliko wao.

Juhudi na mipango mizuri ina nafasi lakini kwa kiasi kidogo tu

Watu wanafanya each and every thing kwa usahihi lakini mafanikio tu ndio hakuna

Kwa kuwa hatujui ikiwa tuna bahati au la basi tuendelee kujituma na kuamini kama ulivoshauri.
 
Vijana vya sasa hivi vya ajabu sana.
Eti hiki nacho kinajiona kizee.
Aya babu tutafata ushahuri wako.
Ila maisha ya sasa hivi sio kama ya zamani.sasa unatakiwa kushikilia bomba haswa.

Hata hizo kazi unazosema umepata sasa hivi hazipatikani .
Kupata kazi sasa hivi imekuwa kazi mzee
 
Be blessed father,nazingatia hilo
 
Mzee ungeelekeza vizuri namna ulivyoanza kuwekeza na sehemu ulizowekeza uzi wako ungekuwa na manufaa sana Kwa wasomaji, ila Kwa style hii uliyokuja nayo uzi wako umejaa majigambo na mipasho.

Uwe na j.pili njema nawe pia
Watu wana hasira na hii life[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Uko sahihi, watu wanachambua sana, kumbe lengo la mtoa mada ni kutukumbusha yatupassyo kufanya kabla ya uzee.

Watu wanahoji mpaka umri, ina maana wameshindwa kuona hekima iliyo katika andiko, wanatafuta kasoro pekee. Kupanga nj kuchagua.
Kama alidanganya umri maana yake hata andiko lake inaweza kuwa chai ya rangi tu
 
Nilikuwa nakula (30-40)% inayobakia na investvau na save basi hamna kipya

Sikuwa mtu wa anasa kabisa
Eeh sasa imagine ulipwe zaidi ya million 1 kwa mwezi kwa miaka 35. Hata uwe mtu wa bia kila siku lazma utastaafu na hela tu.

Sisi hata hizo fursa za kazi hatuna sikuhizi. Unajikuta unaenda kufanya kitu ambacho kila mtu anafanya sababu ya easy entry.
 
Wala hilo andiko hajafafanua vizuri. Alitakiwa atueleweshe amewekeza nini.
Mkuu, hapa jf ukitaka kila mtu atoe uhalisia wa maisha yake hutampata hata mmoja. Wewe angalia alichoandika, chukua kile kinachokusaidia kifanyie kazi kwa njia zako.

Hata kama atakueleza njia alizopita katika kuwekeza haita kuwa na maana kwako kwa vile kila mmoja ana njia zake za kufanikiwa.
 
Eeh sasa imagine ulipwe zaidi ya million 1 kwa mwezi kwa miaka 35. Hata uwe mtu wa bia kila siku lazma utastaafu na hela tu.

Sisi hata hizo fursa za kazi hatuna sikuhizi. Unajikuta unaenda kufanya kitu ambacho kila mtu anafanya sababu ya easy entry.
Kwenye 1m *35 yrs kuna ukakasi😅
Ila cha msingi nimeona ni kujitahidi ku invest tukiwa vijana na nguvu kubwa, ili uzeeni tupate ahueni.
 
Kweli kabisa.na kwa kipindi icho kaz ni uhakika sio kama saiv mtu anasoma na kupata kazi ni kazi.
Sahizi kusoma ni jambo moja na kufanikiwa ni jambo jingine 😀! Zamani ilikuwa rahisi tu unamaliza chuo ushapangiwa kazi wewe ni kula mshahara tu. Unajipangia aina ya maisha unayotaka.

Sahizi maisha ndio yanakupangia uishi yanavyotaka. Yakiamua uteseke unateseka balaa na hamna kitu utafanya. 🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…