Nguvu nilizowekeza kwenye ujana wangu nakula Matunda yake sasa

Nguvu nilizowekeza kwenye ujana wangu nakula Matunda yake sasa

Huyo anajiita babu yupo JF mpaka saa8 usiku anacomment upumbavu. Mkuu mbona unataka kujitoa akili wakati vitu vipo wazi kabisa baby gani wa miaka 70 usiku saa8 anachat. Hivi shule ukuenda hata pic uoni?
Mwache inawezekana kwani Andrew Nyerere nyuzi zake na comments alikuwa anaandika Muda gani? Tena Andrew Usiku wa manane ndo ulikuwa Muda wake wa kupost Habari zake.
 
Kwangu mimi navyoona umri wa kuweka nguvu ni (25-55) hapa ndo inabidi ufanye uwekezaji mkubwa na uchakarike sana

Lakini kumbukeni pia kumtanguliza Mungu kwenye kila mfanyacho, ili azidi kuwabariki,

Mimi namshukuru Mungu wanangu 4 wapo vizuri kila mtu yupo kwao NA FAMILIA ZAO

Mimi nalea wajukuu tu wakija likizo,

Hivyo ni faraja sana kwangu,

Namshukuru Mungu kwa kunijaalia uzee mzuri, japo haikuwa rahisi mpaka kufikia hapa nilipo,
Ahsante kwa kutukumbusha hili swala.
 
Sijaelewa kwakuwa hujasema ulitumia mbinu gani kutoboa.
Mbinu niliyotumia ni ajira mkuuu,

Niliweza kujipangilia vizuri, mshahara wangu kila mwezi,

Hivyo nilikuwa na mtaji mzuri, jumlisha marupu rupu

Ndo niliweza kufanya hilo kwenye kuanzisha miradi yangu,

Ila mafao ya 2016 yalini boost sana
 
Back
Top Bottom