NHIF yafuta Bima ya Afya kwa watoto "TOTO Afya Kadi". NHIF yadai hawajafuta ila wameboresha

NHIF yafuta Bima ya Afya kwa watoto "TOTO Afya Kadi". NHIF yadai hawajafuta ila wameboresha

Tatizo la hii Bima ya Watoto ya shilingi elfu 50,400 tulikuwa tunachagua mno watoto wa kujiunga, yaani nina watoto watatu basi nalipia yule mtoto tu anayeumwa, sasa kwa mtindo huu lazima mfuko ungeelemewa na wagonjwa.
Yaaani ni kama una gari unasubiri ipate ajali ndiyo uikatie Bima, hapa NHIF walijitia kitanzi wenyewe.
Sasa sidhani kama kuna mtu anakonda kubagua mtoto wa kumkatia bima kama hela unayo.

Kutokuwa na hela ndio kinachochangia mtu analna bora amlipie yule mwenye afya isiyo imara, so usione kama watu wanafanya kusudi.
 
Sasa sidhani kama kuna mtu anaconda kubagua mtoto wa kumkatia bima kama hela unayo.

Kutokuwa na hela ndio kinachochangia mtu analna bora amlipie yule mwenye afya isiyo imara,so usione kama watu wanafanya kusudi.
Ndiyo shida inapoanzia hapo sasa, ina maana huo utakuwa ni Mfuko wa kuhudumia wagonjwa sasa, baada ya muda lazima utaanguka,
Bima inatakiwa kulipiwa kabla ya kuugua, Bima inalipiwa kama kinga dhidi ya janga, siyo baada ya kupatwa na janga.
 
Naandika huku nafuta ila ukweli bima ni kama mradi mwingine wa ulaji kwa wakubwa maana watoto ni kweli wanakumbana maradhi mengi ila sio wote
Inapotokea watoto hawajaumwa mwaka mzima fedha wanajilimbikizia wenyewe
Ni kweli kwa mwaka
Na anapomwa ukienda hospital watakuambia dawa hii ipo kwenye bima ila dawa hii haipo kwenye bima, hilo swala huwa linanikwaza kweli kweli
Kwa nionavyo hii mifuko ya bima japo wanaipromote sana ila kuna siku itafail maana usimamizi thabiti haupo
 
Asanteni NHIF mi nimependa sana utaratibu wenu wa watoto kusajiliwa kupitia shule wanazosoma aisee hii imetulia kwanza mmetuondolea usumbufu wa kufuata hiyo huduma mjini sisi tuta dili na walimu wakuuu mashuleni kwetu
mbona hiyo ilikuwepo siku zote au niseme kuna baadhi ya taasisi zilisha jiongeza...
Mf: Kuna mdogo wangu alisoma chuo cha kati, na malipo yote ya Bima nilikuwa nalipa Chuoni wanafanya kila kitu wenyewe na ndio ulikuwa utaratibu za Chuo
 
Ndiyo shida inapoanzia hapo sasa, ina maana huo utakuwa ni Mfuko wa kuhudumia wagonjwa sasa, baada ya muda lazima utaanguka,
Bima inatakiwa kulipiwa kabla ya kuugua, Bima inalipiwa kama kinga dhidi ya janga, siyo baada ya kupatwa na janga.
Basi kama ni hivyo,iletwe bima ya wote kabisa..

Hapo tutakuwa tumesolve tatizo.
 
Tatizo la hii Bima ya Watoto ya shilingi elfu 50,400 tulikuwa tunachagua mno watoto wa kujiunga, yaani nina watoto watatu basi nalipia yule mtoto tu anayeumwa, sasa kwa mtindo huu lazima mfuko ungeelemewa na wagonjwa.
Yaaani ni kama una gari unasubiri ipate ajali ndiyo uikatie Bima, hapa NHIF walijitia kitanzi wenyewe.
Kipi kinabadilika Sasa hivi?
 
Hawajawahi na hawatawahi kueleweka kamwe[emoji848]

Kilio kwa wasio na uwezo sasa mweeh
 
Lengo wanataka waondoe mchangiaji mmoja mmoja, wanataka waweke nguvu kwenye shule kila mwanafunzi lazima awe na lazi, wakifanya hivyo watapata wachangiaji milioni 10 kwa mwaka ambao watagenerate zaidi ya Bilioni 50

Lengo lao ni wachangiaji wawe wengi.

Wanaondoa ile ya mtu 1 kukatiwa
Acha vituko basi yaani mzazi mwenye watoto 7, 8, au 5 (kumbuka ndio hali halisi vijijini huko) na wote wanasoma shule alipie kila mtoto elfu 50,400 tena kwa mwaka.

Bongo hii hii?
 
Bima ya afya kwa wote itajibu maswali mengi sana ambayo wananchi tunajiuliza kuhusu bima ya Afya. Serikali inatakiwa kufanya kadri wawezavyo kutuharakishia Bima ya afya kwa wote

Mamilioni ya shilingi je watanzania wa familia ya kawaida wataweza ?

Serikali kwanza ingewekeza kuzuia kama magonjwa ya malaria, magonjwa ya maji machafu, magonjwa yasiyoambukiza.

Mpango huu wa kuzuia magonjwa hayo ungepelekea watanzania wachache kwenda hospitali. Hivyo kupunguza gharama za bima na wengi kuingia ktk mpango wa bima au serikali kuweka mfuko maalum wa bima kwa wote unaolipiwa na serikali.

Kuzuia magonjwa ni gharama ndogo kuliko kutibu mgonjwa hivyo kuzuia magonjwa ya maambukizi kama kichocho, kuhara, Malaria, kipindupindu, Ameoba/ amiba, typhoid, TB, HIV, utapiamlo na pia magonjwa yasiyoambukiza kama pressure, stroke, cholesterol n.k kunaweza kupunguza gharama za matibabu.

Cuba's focus on preventive medicine

By focusing on primary care and health promotion, the Cuban health system is designed to prevent 90% of health problems. Cuba derived this ...

When we think of epidemics, we tend not to think of Cuba. Yet, Cuba has an exemplary track record when it comes to health security – that is, the prevention and control of infectious-disease threats

The first level is the grassroots level focused on primary care and prevention. This is the largest and most crucial level; everything begins in the community. Family Medicine Doctors are responsible for mobilizing the community: campaigning for sanitation, emphasizing the need for blood donations, administering vaccinations and controlling environmental infectious diseases. This investment connects subsequent levels and ensures prevention is the foundation of all provided care ...


1678743447170.png
 
NHIF ina vifurushi vya bima ya afya unavyoweza kujiunga kulingana na uhitaji, ukubwa wa familia na umri. View attachment 2549277
Wekeza afya,
Najali afya,
Timiza afya,

Tunaomba ufafanuzi wa hivi vifurushi,
Kwanini vingine gharama na vingine vina unafuu,ama vinaruhusu kupata tiba gani?
Tunaomba ufafanuzi wa kina.


Bima kwa wote ni ndoto.
 
Taarifa ya Mfuko wa Bima inasema Inafanyaa Maboresho lakini pia wazazi wanweza kuendelea kuwasajili wantoto wao kupitia mashuleni nk. lakini inatakiwa watu wajue mwarubaini wa haya yote yanayoonekana ni chabngamoto ni mfumo wa Bima ya afya kwa wote huu ni Utaratibu mzuri sana , Serikali imechelewa mfumo wa bima ya afya kwa wote unatakiwa kuharakishwa kwani utakua ni mkombozi wa mambo mengi tunayoyaona ni gharama hivi sasa , tena .Tuleteeni Bima ya Afya kwa Wote TUPONE. Maisha yaendelee tuwe na uhakika wa Matibabu kabla ya kuugua
Mliozaliwa Kwa wakunga WA kienyeji mnatabu Sana ......mkaona vitoto vinaupiga mwingi
 
Aisee NHIF mmejua kutuletea huduma karibu kijijini kwetu kwa hiyo sahizi mambo namalizia shule iliyopo kijijini kwetu hakuna kwenda wilayani mambo ni huduma karibu na wananchi.
Asante sana Mama Samia maana kwenda Bomani sie wengine hatuna nauli ya kwenda kufuatilia bora tumalizie hapahaoa kijijini kwetu
Shule gani unazungumzia, izi ambazo hazina HAta madawati ,walimu , Ndio nhif itakuwa inapatikana hapo
 
mbona hiyo ilikuwepo siku zote au niseme kuna baadhi ya taasisi zilisha jiongeza...
Mf: Kuna mdogo wangu alisoma chuo cha kati, na malipo yote ya Bima nilikuwa nalipa Chuoni wanafanya kila kitu wenyewe na ndio ulikuwa utaratibu za Chuo
HUyo jamaa anazungumza , chekechea, primary, secondary 0&A nao wapate bima wakiwa shuleni
Inchi inaenda shimoni aisee
 
Back
Top Bottom