Ni aibu kuwa na taifa ambalo Rais wake anaingilia Mhimili wa Mahakama na anajinasibu kufutia wakosaji makosa kinyume na katiba

Ibara ya 107B ya katiba ya JMT imetamka wazi kuwa mahakama zitakuwa huru kuendesha mashauri.

Inashangaza rais Samia kumfutia mharifu makosa

Hii ni kinyume na katiba.
πŸ‘‡View attachment 2538542

Mwenye kesi kisheria anaruhusiwa kufuta kesi yake, sasa kama kesi zilifunguliwa kwa maagizo ya mwenye nazo hakuna kosa wala tatizo lolote kusema anazifuta. Siamini kama kwa mfano kuna mtu ana malalamiko binafsi dhidi ya Lema kwamba hiyo kesi itafutwa. Hiyo ni kesi kati ya mlalamikaji na mlalamikiwa, mlalamikaji muda wowote ni haki yake kufuta kesi akitaka na ni utaratibu wa kawaida.
 
Sio kwamba anaiomba mahakama ifute kesi?
 
Pole sana ndugu yangu labda uliajiliwa kwa ajili ya kuuwa na kutesa wanyonge kipindi kile, sasa hivi labda kaendeshe bodaboda
 
Upeo Kaka. No.1 ana upeo mdogo.
 
Sio kwamba anaiomba mahakama ifute kesi?
Ndio maana huo ndio utaratibu wenyewe wa kisheria kwamba unaomba ili kufuta kesi. Na anayefanya hivyo ni mwenye kesi mwenyewe.

Sasa nikikwambia wewe kuwa nafuta kesi yangu juu yako kuna kosa gani? Kinachofata ni mimi kupeleka prayer yangu ili kuifuta kisheria kwenye mahakama basi.
 
Mahakama ikishasomewa sihitaji
Kama na jamhuri kesi inakuwa chini ya mamlaka ya mahakama. Ndio maana mahakama inatakiwa kuwa huru. Kama Jamhuri imesoma charge na kudai ushahidi umekamilika kwa nini zifutwe?
 
Ibara ya 107B ya katiba ya JMT imetamka wazi kuwa mahakama zitakuwa huru kuendesha mashauri.

Inashangaza rais Samia kumfutia mharifu makosa

Hii ni kinyume na katiba.
πŸ‘‡View attachment 2538542
Nyie wanaccm tulipokuwa tunawaambia rais anaweza kuingilia mahakama na kuagiza zitoe hukumu ya aina gani mbona mlikuwa mnasema mahakama ni huru?
 
Miongoni mwa Mazuzu ya CCM yanayopaswa kupuuzwa ni pamoja na wewe, ni mashetani mlionufaika na unyama wa awamu ya 5 ndio maana mnaumia kuona haki ikitamalaki
 
Twende taratibu. Kwa hiyo mama alimuundia kesi Sabaya? Mimi hapa ninakesi ya Sabaya kumpiga mdogo wangu pale Kokoriko akijaribu kumnyang'anya mchumba wake aliyezaa naye, maskini Sabaya akajua malaya kampiga dogo na kitako cha smg (video zipo).

Kesi upelelezi umeisha, tunasubiri ahukumiwe hizo, kisha na sisi tunampandia. Dogo tulimshitaki Magufuli akiwa hai, faili likawa linapotezewa. Alipokufa yule mchato, ngoma imeandikishwa na tutaweka ushahidi wa watu na video. Tujue kama mkuu wa wilaya anaruhusiwa kupiga raia mabaa na silaha ya AK47.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…