Ni aibu kuwa na taifa ambalo Rais wake anaingilia Mhimili wa Mahakama na anajinasibu kufutia wakosaji makosa kinyume na katiba

We mbumbumbu acha zako. Ulisikia rais gani akisema hadharani kuwa alimfutia mharifu kosa

Mbumbumbu ni weee ambae unasoma halaf huelewi nilichoandika. Labda niweke kwa kiswahili, hayo mamlaka yamekuwepo toka enzi za nyerere, kila rais amekuwa akitumia kwa style tofauti. Ishu sio kusema ishu ni kutumia hayo madaraka, si kitu kipya
 
Mupe muruke.

Tunafurahia Kwasababu yaliyofanyika YANATUNUFAISHA
 
Ibara ya 107B ya katiba ya JMT imetamka wazi kuwa mahakama zitakuwa huru kuendesha mashauri.

Inashangaza rais Samia kumfutia mharifu makosa

Hii ni kinyume na katiba.
πŸ‘‡



Muwe mnaelewa nyie punguani mikesi mliokuwa mnaishabikia ilikuwa ni mikesi ya kisiasa iliyoasisiwa na mwehu mwenzenu yule huo ushamba mama hataki.
 
Ukiangalia matendo yanayofanyika.
Sawa, lakini hiyo siyo kwa sababu ya katiba.

Hiyo ni kwa sababu ya uoga, udhoofu, na ujinga wa Watanzania walio wengi.

Nishawahi kusema humu kuwa matatizo yetu ni zaidi ya katiba mpya.

Watu kiujumla inabidi tubadilike kifikra pia. Rais siyo mungu. Rais hayuko juu ya sheria. Rais si mkubwa kupita Tanzania.

Akikosea yapaswa aambiwe na hata kugomewa ikibidi.

Haya yote hata kwa sasa yanawezwkana kabisa.

Ila kwa uoga tulio nao, tunaachia tu mambo yafanyike kana kwamba Rais ana haki na mamlaka ya kuyafanya!

Hana!!
 
Kama kesi zenyewe ni za mchongo (Amri toka Juu). Kwanini Amri hiyo hiyo isitolewe kuzifuta??

Ndiyo maana tunahitaji Katiba Mpya itakayotenganisha Mihimili yote Mitatu na utengano huo uonekane wazi. Yaani Kila mmoja uweze kutekeleza majukumu yake bila ule uliojichimbia chini zaidi kuzihujumu Mingine.
 
Amri kutoka juu haimaanishi kuwa ni amri halali.

Na amri isiyo halali inapaswa kukataliwa. Nilishawahi kutolea mfano hapa kuhusu majenerali wa Marekani waliokuwa tayari kukataa kutekeleza amri yoyote isiyo halali toka kwa Rais Trump, maana jamaa alikuwa hatabiriki.

Majenerali wakakaa wakakubaliana kuwa endapo watapokea amri isiyo halali toka kwa amiri jeshi mkuu wao, basi wao walikuwa tayari kuisimamia na kuilinda katiba yao kwa kumkatalia Trump.

Huo ni ujasiri. Ni werevu. Na ni uthubutu.

Kwa hilo hatuhitaji katiba mpya. Tunahitaji tu kubadilika kifikra na kutambua haki zetu.

Amri kutoka juu ambayo si halali, haipaswi kutekelezwa.

Ni fikra. Si katiba.
 
Ibara ya 107B ya katiba ya JMT imetamka wazi kuwa mahakama zitakuwa huru kuendesha mashauri.

Inashangaza rais Samia kumfutia mharifu makosa

Hii ni kinyume na katiba.
πŸ‘‡



Eti unaamuru DPP aondoe kesi ya fulani lakini ya fulani iache kisa unabembeleza kupendwa duaniani badala ya kuwa mtumishi wa watu wote kwa usawa.

1. Kukumbatia chama kimoja kinzani katika malalamiko yao na kufumbia macho vingine visivyo maarufu ni upofu wa hekima na busara
2. Kufuta kesi za ugaidi, uhujumu uchumi na kuacha kuziondoa kesi za kubambika na uonevu kwa wasaidizi ni ubaguzi bayana usio na huruma yoyote
3. Kujihisi una furaha sana unaposikia watu unaowaongoza wakimshambulia aliyekuwa mtangulizi wako kwenye kiti ulichokalia inaonesha mpango ovu unaufahamu na umekunufaisha
4. Kusikiliza ushauri kutoka chama kimoja kinzania na kuonesha upendeleo wa wazi mbele ya watanzania huku ukuwaacha wengine wakinung'inika pasipo msaada wowote wa kukabiliana na changamoto wanakumbana nazo inaashiria kutekwa dola kisaikoljia huku ukiwa umeridhia kwa hofu ya kutoshinda kinyang'anyiro cha madaraka.
Nk....
 
Yule msukule wenu alimtoa Babu Seya Kwa Sheria gani vile?
 
Hapa Naona kizunguzungu tu.

Rais akiwa Arusha anasema alizungumza na Lema na kumwambia kwamba asihofu arudi nyumbani atamfutia kesi zake.

Jambo hili linashangaza mno.

Mosi, Rais anapata wapi mamlaka ya kuingilia mhimili mwingine?

Haoni kwamba anavunja katiba hadharani?

Tunaposoma katiba tunaona kwamba Mahakama ni mamlaka inayojitegemea.

Yeye nguvu za kuingilia Mamlaka nyingine anazitoa wapi?

Ukiachana na hilo.

Lema ni mpinzani. Yeye ni Chama tawala.

Chukulia mfano wa mtoto na mtoto wa jirani.

Yaani inakuwaje mama anaacha wanawe wanalia njaa halafu anapeleka chakula kwa watoto wa jirani.

Huyu atakua mzazi wa aina gani?

Rais yupo tayari kufuta kesi ya Lema hata kwa kuvunja katiba lakini hayupo tayari kuvunja katiba kwa kufuta kesi ya Sabaya ambaye ni mwanachama wake.

Upendo wa mashaka huu. Au tuuiteje.

Maana Logically it doesn't make sense at all.
 
Sema Sabaya na yeye, vipi mbona lema hata risasi ajachika? Hivi kikundi cha Sabaya si sawa na Waasi wa Congo. Lissu kala risasi 16 .... Sabaya ni zaidi ya Shetani
 
Sema Sabaya na yeye, vipi mbona lema hata risasi ajachika? Hivi kikundi cha Sabaya si sawa na Waasi wa Congo. Lissu kala risasi 16 .... Sabaya ni zaidi ya Shetani
Kama mwanachama ni shetani....

Mwenyemeza atakuwa nani??

Kama Rais kaamua kusamehe na kufuta kesi kwanini asifute ya Sabaya??

Mwanachama wake ??
 

Sabaya ni kesi halali za uhalifu wake, wakati Lema ni kesi za mchongo toka kwenye siasa chafu za Magufuli.
 
Waliofutiwa kesi ni kwa sababu zilikua za kisiasa na kisasi, za kubambikiwa. Ni tofauti na kesi za unyang'anyi na kupora.

Pia inawezekana ni matakwa ya wazungu wakopeshaji (uboreshaji wa demokrasia), sidhani kama kuna mkopeshaji anataka Sabaya afutiwe kesi.

Sabaya huenda kuwekwa ndani ni salama zaidi kwake kuliko kutolewa.

Pia Rais hapangiwi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…