Kwanza, nakubaliana na msingi mmoja muhimu ulioutoa: ndiyo, mara nyingi utambuzi wa utimilifu wa unabii huhusisha kulinganisha maandiko na matukio halisi. Mfano ulioutoa wa Injili ya Luka kuhusu utimilifu wa unabii wa Isaya kupitia Yesu ni sahihi kwa muktadha wake. Lakini tofauti kubwa ipo hapa.
ule ulikuwa unabii maalum, wenye maelezo mahsusi, uliotimizwa ndani ya muktadha ule ule na kuthibitishwa moja kwa moja ndani ya maandiko yenyewe. Hapo hakuna kubahatisha wala kupanua maana nje ya kilichoandikwa.
Tatizo linatokea pale unapochukua kanuni hiyo halali kisha ukaipanua bila mipaka na kuanza kuiweka juu ya matukio ya kisasa yasiyotajwa wazi.
Utimizo wa Unabii katika Luke 4:16-21 unatokana na Unabii wa Isiah 61:1-2 The spirit of the Sovereign Lord is upon me, Because God anointed me to declare good news to the meek…, To proclaim liberty to the captives.Unabii huu Pamoja na Nabii nyingine za agano la kale zililenga kumtambulisha mtu ambaye atakuwa Masihi. Kumbuka Yesu aliishi maisha ya kawaida kabisa. Na wayahudi ktk kipindi hicho kupitia unabii ndani ya Agano la Kale walijua fika kuwa ni majira ambayo Masihi anatakiwa atokee. Luke 3:15 inasema watu walikuwa wakitarajia na walijiuliza Mioyoni mwao kuhusu Yohana; “Je labda huyu ndiye Kristo?” Kwa hiyo Yesu alipoanza Utumishi wake (kuhubiri Habari njema ya ufalme na kuponya wagonjwa na kufufua wafu) ilibidi pia ahusishe matendo anayofanya na Unabii wa Agano la kale unaomtambulisha mtu atakaye kuwa Masihi. Madai yako kuwa unabii huo una muktadha wa kipekee siyo sahihi. Angalia kwamba siyo wote waling’amua jinsi yesu alivyofafanua utimizo wa unabii huo. Mfano wayahudi wengine walimkataa kuwa ni Masihi kwa sababu tafsiri yao To proclaim liberty to the captives wao walichukulia kuwa Lazima huyo mtu atakaye kuwa Masihi ataongoza harakati za kuwakomboa toka ukoloni wa Waroma (Soma 6:15 na Acts 1:6).
Ndivyo hivyo hivyo leo hii mko nyinyi mnaopinga utimizo wa Unabii wa Biblia kwa sababu mko na tafsiri yenu ya ubinafsi kuhusu unabii huo.
Pili, hoja yako kuhusu “secular history kuthibitisha unabii” ina sehemu ya ukweli, lakini umeiruka hatua muhimu ya kimantiki.
Historia inaweza kuthibitisha kwamba tukio fulani lilitokea, haiwezi kuthibitisha kwamba tukio hilo ndilo tafsiri sahihi ya unabii fulani, isipokuwa kama maandiko yenyewe yalilitaja kwa uwazi.
Hapa umeangukia kwenye kosa la confirmation bias, unaanza na hitimisho (kwamba Biblia inaongelea matukio ya sasa), kisha unatafuta matukio yanayofanana na hitimisho hilo ili kujithibitishia.
Unabii unabaki unabii na kuuthibitisha inahusisha kwanza tukio litokee na baada ya hapo watambuzi wanapitia mrorongo wa features za tukio hilo na kuzioanisha na unabii husika. Mfano ni Unabii katika Agano la Kale Kuhusu Mtu atakayekuwa Masihi (Kristo) Mungu alihakikisha unakuwa na features nyingi ambazo ukizileta kwa Pamoja ilitakiwa zi point kwa mtu mmoja kumthibitisha kuwa ndiye masihi. Mfano wa Unabii hizo ni:
1. Born to a Virgin (Isaiah 7:14; Matthew 1:18, 22, 23)
2. Born in Bethlehem (Micah 5:2; Luke 2:4-7)
3. Protected as a Child (Hosea 11:1; Matthew 2:13-15)
4. Called a Nazarene (Isaiah 11:1, 2; Matthew 2:23)
5. Arrived at the Appointed Time (Daniel 9:25; Luke 3:1, 2, 21, 22)
Kwa maana hiyo Unabii ninaokuambia sasa, mpaka wakati huu unabakia kuwa Unabii na ndiyo maana ninakwambia kama hauniamini basi tusubirie matokea. Aidha, ninaku challenge wewe utoe tafsiri yako ya matukio yanayotokea sasa
Tatu, unapozungumzia unabii wa Daniel 8 na kuuhusisha moja kwa moja na “Anglo-American Alliance,” hapo ndipo pengo la kitaaluma linaonekana wazi.
Maandiko hayo yanazungumzia falme kwa lugha ya alama (symbols) na yana muktadha wa kihistoria unaohusishwa na falme za kale. Hakuna mahali panapotajwa moja kwa moja Marekani au Uingereza, wala hakuna kigezo cha moja kwa moja kinacholazimisha tafsiri hiyo. Hivyo unachofanya si kufasiri maandiko, bali ni kuya-project kwenye siasa za leo.
Hilo ni kosa la anachronism, kuweka maana ya zama za sasa kwenye maandiko ya kale bila msingi wa ndani ya maandiko hayo.
Mr. Aristotle, umesoma vizuri hiyo Daniel 8?! Au unakimbilia tu kututisha na Philosophical Jargons zako anachronism!? Hapo anaonyeshwa vision of the ram (Medo-Persia) and the goat (Greece i.e. Alexander the Great himself and the four divided Hellenistic kingdoms). Lakini pay attention to verse 23 ambapo pana mtambulisha
a fierce-looking king who would arise in the final part of the above metioned Kingdoms. Hii Kingdom ni ipi?
Kuuelewa huu unabii inakubidi Mr. Aristotle usome pia nabii nyingine za Daniel na ikiwezekana soma pia Reveletion 13.
1. Daniel 2: the statue representing Babylon → Medo-Persia → Greece → Rome
2. Daniel 7 of the Four Beasts representing: Lion (Babylon) → Bear (Medo-Persia) → Leopard (Greece) → Fourth Beast (Rome) with ten horns and a little horn
Hivyo madai yako kuwa nimefanya kosa anachronism siyo sahihi. Unabii huo ulihusisha pia matukio ambayo yangetukia karne za mbele sana. Sasa nikuelimishe: Roman empire na baadae Pope akihusishwa ndiyo foundation ya Falme zote za Western Europe. Maandiko yaposema pembe kumi (Daniel 7:7) inamaanisha kwa ukamili wake. Kwa muktadha huu inamaanisha Ulaya yote. Ona pia baada ya kutamka hizo pembe kumi unabii unaongezea kuwa na pembe nyingine ndogo itachomoza miongoni mwao. Hiyo pembe ndogo ni British Empire. Kabla ya kufikia karne ya 16, Ufalme wa Uingereza ulikuwa insignificant as compared to others like Spain, Netherlands and France. Lakini kama ilivyotabiriwa kwenye Unabii huu baada yah apo Uingereza ilikuja kuzishinda kivita Falme hivi nyingine na kujiweka kama World superpower. Kuanzia Vita Kuu ya Kwanza, America akawa Mshirika wa Karibu wa Uingereza na hatimaye Baada ya Vita Kuu ya Pili ndipo Kinachoitwa Anglo-American Alliance kikaundwa.
Nne, hoja yako ya “chronology ya Biblia tangu Adam” pia ina tatizo la msingi. Ni kweli Biblia hutumia mifumo ya miaka ya wafalme na matukio, lakini wataalamu wa historia ya Biblia wanakubaliana kuwa hakuna makubaliano moja thabiti ya mwaka kamili wa dunia kwa kutumia Biblia pekee.
Hivyo kudai kwa uhakika kwamba “tuko mwaka fulani tangu Adam” ni kudai usahihi ambao maandiko yenyewe hayajautoa kwa uwazi. Hapa kuna kosa la overconfidence katika tafsiri ambayo kiasili ina utata.
Hoja yako ya kupinga ukadiriaji wa miaka tangua Adam alivyoumbwa, nafikiri tukubaliane kuwa hakuna hakuna makubaliano moja kwa moja ya mwaka kamili wa dunia kwa kutumia Biblia pekee. Hiyo inaeleweka. Namimi wala sikusema Biblia ndiyo iliweka hilo. Bali mimi nilisema watu waliaminishwa hilo.
Sasa ni hivi: According to the Masoretic genealogy:
Adam to the Flood = 1,656 years; According to the
Septuagint chronology: from Adam to the Flood is approximately 2,242 years. However, using Masoretic chronology the creation of Adam was in the year 4004 BCE and Jesus’ Birth was in the year 4BCE. Hence, Time from Adam creation to Jesus’ birth is approximately 4,000 years
Tano, mfano wa watu wa zama za Nuhu kutokuamini gharika hauwezi kutumika kama ushahidi wa hoja yako. Huo ni mfano wa kihisia (analogy fallacy), si ushahidi wa kimantiki.
Kusema “waliokataa zamani walikosea, hivyo wanaokataa sasa wanakosea pia” si hoja sahihi; kila hoja hupimwa kwa ushahidi wake, si kwa kufanana kwake na simulizi la kale.
Kuhusu gharika msisitizo wangu ulikuwa kwamba watu wa wakati wa Noah walishindwa kuhusisha unabii alioutoa kuhusiana na maangamizo kutokana na gharika kwa sababu mvua kwao ilikuwa ni jambo geni kabisa. Vivyo hivyo, kuna unabii mwingi utakaotimizwa nyakati zetu watu watashindwa kutilia maanani kwa sababu matukio yatakayohusisha utimizo hu oni mambo mageni kabisa kwao hivyo kuona kama mzahaa. Sasa wewe unayesema haiwezekani kama kosa lilifanywa na watu wa kale likarudiwa na watu leo hii hiyo ni akili yako. SUBIRI MAAJABU.
Sita, unaposema Ufunuo 17 unathibitisha kuangamizwa kwa dini zote na kuhusisha hilo na taasisi za kisasa kama UN, hapo unafanya kile kinachoitwa speculative interpretation. Unachukua maandiko ya alama nyingi (symbolic text), kisha unayafunga kwenye tukio maalum la kisiasa bila ushahidi wa moja kwa moja. Hii si tafsiri ya kitaaluma, bali ni ubashiri (speculation).
Kuhusu kuangamizwa kwa DINI yako ya UONGO kama ilivyosemwa katika Ufunuo 17, ni kwambie kwamba hayo ndiyo mojawapo ya Maajabu mtakayositukizwa. Kama ilivyokuwa wakati wa Noah walivyoshindwa kughamua unabii unaohusisha mvua nanyi mtasitukizwa na kupigwa marufuku DINI yako ya Uongo. Inaelekea wala haujui kuitafakari Biblia vizuri. Ufunuo unamzungumzia Mwanamke Kahaba. Ukisoma Agano la Kale pale ambapo Taifa la Israel lilifanya Ushirika na Wafalme wa Dunia hii, Wakati wao walidai kumtumikia Mungu, Basi walitambuliwa kama Kahaba (Ezekiel 16:28-30. Aidha, huyo Mwanamke Kahaba pia anatambuliwa kama Babylon Mkuu. Sasa wakati wa Kale baylon ilitambuliwa kama Kitovu cha dini za Uongo. Hivyo Tafsiri yake kwa Dini zote za Uongo na ambazo zina USHIRIKA WA KARIBU NA SERIKALI ZA KIDUNIA AMBAZO KWA UJUMLA WAKE NI SERIKALI DHALIMU KWA WANANCHI WAO. Pole sana Dini yako iko huko. SIKU inakuja Hao viongozi wa serikali watawageuka na kuwatafuna kama ilivyosimuliwa katika Ufunuo 17.
Saba, hoja zako pia zimechanganya lugha ya uchambuzi na lugha ya imani kwa namna inayozuia mjadala wa kitaaluma. Unaposema “ukisoma bila kichwa cha panzi” au “jiandae kwa maajabu,” unahamia kwenye retorika ya shinikizo la kihisia, si hoja za uthibitisho. Katika mjadala wa maarifa, nguvu ya hoja hupimwa kwa ushahidi na mantiki, si kwa ukali wa maneno.
All in all, napenda kusisitiza hili kwa uwazi, kutafsiri unabii kunahitaji vigezo vitatu vikuu, uwazi wa maandiko, muktadha wake wa kihistoria, na uthibitisho usiohitaji kubahatisha.
Pale ambapo tafsiri inategemea kuunganisha matukio ya leo kwa nguvu, kubadili maana ya alama, au kujaza mapengo kwa mawazo binafsi, hapo hatuko tena kwenye tafsiri ya unabii, bali kwenye ujenzi wa nadharia.
Kwa hiyo, si kwamba nakataa uwezekano wa unabii kuendelea kutimia, ninachokataa ni mbinu unayotumia kuufikia huo hitimisho. Njia hiyo ina mapungufu ya kimantiki, kihistoria, na kitaaluma, na hayo ndiyo yanayoufanya msimamo wako usiwe na uzito unaodai kuwa nao.
Kwa kuhitimisha kama ulivyosema wewe mwenyewe kwamba haukatai uwezekano wa Unabii kutimia, mimi nakuambia kwamba Tuuachie muda utupe majibu. Kwani unabii huthibitishwa baada ya kutimia