Ni changamoto zipi umewahi kupitia ukiwa katika hali ya umasikini?

Mie niko na hela kiasi cha shilingi hamsini tuu 50 nimetoka lipa kodi ya gheto ndo imenimaliza kabisa. Hela kupata kwa sasa msoto , now najaribu kopa kopa. Hata 10k tuu kwenye hizi apps za kukopa online za CASHX , PESAX , BRANCH lakini holaaaa.



NA GESIA Imekata plus msosi gheto umeisha , hapa nime gongea msosi wa kula kesho na kesho kutwa mgahawa wa mama mmoja hivi....yaaaanii tabuuu tupyuuu






Internet data nayotumia ni. DROID VPN ndo inayo ni keep online siku zotee


Madeni yako kote kote si kwa marafiki , majirani , mtandaoni. Bustista , niwezeshe , songesha. , M pawa kaka yotee



Nashukuru tuu nins sehemu ya kulala for the coming 3 months aseeee afuuu niko. Moshi , majira haya ni baridi mnoooo
 
Pole sana Mkuu
 
Hi ni kubwa kuliko
 
Wanadamu!
How? Hivi unawezaje kumtendea mwenzako ubaya mkubwa kiasi hiki?
 
Wanadamu!
How? Hivi unawezaje kumtendea mwenzako ubaya mkubwa kiasi hiki?
Amini yapo hayo hususani yanachagizwa na umasikini uliokithiri. Maskini anaweza kufanya jambo lolote baya ilimradi tumbo lake lisikae na njaa.

Kuna jamaa yangu mmoja alishawahi kunisimulia kisa kama hiki, yaani mtoto alilengeshwa na mama yake ataje kuwa jamaa ndiye amemfanyia mambo hayo. Ilikuwa kesi kubwa ila mwisho wa siku baba wa yule mtoto alilikataa lile jambo na baada ya uchunguzi kufanyika ikajulikana kuwa kuna genge la watoto waliokuwa darasa la tano na la sita ndio walikuwa wakiwafanyia michezo mibaya hao watoto wadogo.

Jamaa tokea hapo mazoea na watoto aliyakata na walikuwa wakitaka kusogelea mlango wake anawatimua vibaya sana. Mchizi mwisho alihama ile nyumba kwani aliona ni mkosi.

Rejea kesi ya babu seya na mwanae papii
 
Aise ninesoma comment ni noma! Mi mwaka 2017 kuna vitu nilipitia nikitulia nitaandika! Ila wife popote ulipo pamoja na changamoto zako haukunitesa mwaka ule zaidi ya kusema YATAPITA!
 
daah Inaumiza ! Niliachishw kaz nina sku mbil mke wng ndo amejifungua ndan cna A wala Z, aisee na vle mwanamke anapaswa ale msoc wa maan ili apate maziw. Nilipitia changamoto ming na mwisho wa ck nliondokew na mtt wng kw chanzo cha kukosa lishe ! Inauma
 
Kaza ndugu yangu
 
Dah pole mzee aisee hii inauma
 
Nimesoma huu uzi wala sijaamini, au wengine watakuwa wanapika chai.
Yaani kuna wana hapa wanaeleza eti wana familia tena mke na watoto afu wanapiga deshi asee ni chai au ni kweli.

Kwa mabachela ni sawa hata mimi nimepitia sana.
Hakuna chai hapa ndugu yangu tena mnalala vizuri tu watoto usiku ni kulalamika maana usingizi hamna kisa njaa!
 
Huyo msela wako alikua na utu, hekima na upendo wa hali ya juu, kitu ambacho ni kigumu kwa maisha ya siku hizi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…