Ni changamoto zipi umewahi kupitia ukiwa katika hali ya umasikini?

Waswahili wanasema Karma is a Bitch.

Mzee ameoneshwa na kufunzwa jambo kubwa sana kupitia wewe. Ingawa unasema amejizima data kujifanya hakumbuki ila Moyoni anajuta haswa.

Hii midomo tuichunge sana katika kutoa kauli kwa maana kuna siku zijazo itatuumbua.

Napenda kuwaambia wale ninaowaita marafiki tutumie midomo yetu kula na kunywa na kunenea watu yaliyo mema. Yale yasiyo ya Lazima kusemwa yaachwe moyoni.
 
Mzee ameoneshwa na kufunzwa jambo kubwa sana kupitia wewe. Ingawa unasema amejizima data kujifanya hakumbuki ila Moyoni anajuta haswa.
Mara nyingi katika maisha ni nadra sana kwa mtenda kukumbuka mabaya yake.
Nilichofanya kwake sio kwa kumdhihaki bali kwa kuwa najua nini maana ya kukosa pale unapohitaji.

Mwenye asili yake haachi, haitokuwa ajabu kesho akiwa na uwezo akaacha kumsaidia mwenye shida na ndio maana tukaambiwa fanya wema uende zako.
 
oyaaa
 
Siku ukipata pesa kidogo sio lazima ziwe nyingi, unaweza ukawa hata na buku mbili ukaichenji mia mbili mbili then ukiona madogo sehemu hasa watoto unawapa..au ukanunua hata mfuko wa pipi unawapa..trust me inafungua sana mambo!
 
Hakika.
 
Maisha niliyopitia ni magumu sana, Kuna wakati narejesha kumbukumbu machozi yanatiririka. Sikuacha kujiombea na kuwaombea wazazi.

Ila Yale maisha yamenijenga sana, wakati mwingine naijsemeza huenda ilikuwa naandaliwa niwe mtu Fulani ambaye atakuja kutegemewa.

Nauchukia umasikini sana, yale maisha niliyopitia sitayasahau.
 
Nilienda bush kumsalimia mjomba angu alikuwa ni mkulima amevuna mahindi mengi ya njano lakini anko aliishi kivyake hakuwa na mke dah alipika ugali mkubwa wa njano nikajua anko ameandaa mboga akatenga ugali kwenye chungu akatoa chupa ina mafuta ya ng'ombe (samli) yameganda akaipisha juu ya jiko ikayeyuka akamimina kwenye bakuli akaweka chumvi ikawa ndio mboga unamega tonge unatoezea kwenye mafuta unameza ugali
 
Nilinunua mkate wa buku nikawa nakula slace mbili au moja nashushia na uji.

Maana nikipiga ugali unga hautoshi na utaisha fasta na ndani kuna sukari na unga, ikawa ni mwendo wa uji na mkate.

Ukibadili mlo basi ni ugali na mboga za majani, hapo huo mlo ni mzito sana aisee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…