Ni changamoto zipi umewahi kupitia ukiwa katika hali ya umasikini?

Nkikumbuka enzi nakua mama ambaye ndo hustler wa familia alivyopambana na sisi kwenye lile wimbi la umaskini[emoji24][emoji24]
RIP dear mama japo matunda ya jasho lako hukuyaonja walao uliona milango inaaza kufunguka
[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]Daa acha tuu Mama yetu pia ameondoka kipindi mwanga ndo unaanza kuonekana.. Inaumaaa sanaa yani mnooo!
 
😄😄😄😄😄😄😄 Na wife alivyorudi mlilala wapi?
 
Mke wangu kushindia mua tu tena akiwa mjamzito. Mungu atusaidie kwa kweli.
Mimi pia nimewahi kushindia kipande Cha mua Cha sh.100 na nilikinunua Kutoka Kwa akina ya sh.300 niliyokuwa nayo..

Pili nikiwa Dar nilipigika kiasi kwamba Chakula na makazi nilikuwa nakula Kwa mama wa rafiki yangu..

Siku Moja Jamaa alisema Kila mtu aondoke akapange ,hapo Sasa ndipo Kilio kichwa kilijaa gas,ilifika mahala nikaomba Msaada wa nauli Kwa broo Fulani ambae niliwahi soma nae O level,yule ndio alinisaidia nauli nikarudisha Mpira Kwa kipa mkoani ambako Nako maswaibu yaliendelea ikiwemo Hilo la kushindia Mua huku nasaka kazi za saidia fundi niweze ku survive..

Siku Moja nikiwa kwenye kazi za saidia fundi ukiacha kejeli vilaza wale mafundi Kwa vile walishajua mie ni msomi,nikapata demu huko huko basi wakaanza kumponda akanikacha,nikapata mwingine nikajiroga kumleta geto ,getoni Kulikuwa na jiko la Mkaa,ndoo 2 ndogo ya kuogea na ya kawaida na visufuria viiwili,godoro la wanafunzi nimetandika chini na geto ni single jirani na vyoo..

Demu alivyoingia nadhani alichoka ,akaomba atoke Nje uani,aisee alisepa maxima na akaniblock na Namba yangu 🤪🤪🤪🤪

Ila Maisha yanabadilika siku huko tena Mungu anawajali watu wake.Dar sikutoka Bure nilipata Mke.
 
Humu utaishia kudhihakiwa tu hakuna msaada utapata
 
Po
[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]Daa acha tuu Mama yetu pia ameondoka kipindi mwanga ndo unaanza kuonekana.. Inaumaaa sanaa yani mnooo!
Pole mkuu, ila ndo maisha ila kila siku ya maisha yangu siwez acha kumkumbuka mama maana alipambana kufa na kupona kwa ajili yetu. Kuna siku aliumwaga tukiwa wadogo kwa mda kama wa zaid ya wiki mbili nahisi, tuliteseka sana kipindi kile
 
Kamwe do not entertain kumwaga chakula ndani kwako, hakikisha chakula kinapikwa cha kutosha watu kushiba vizuri lakini kisiwe kinamwagwa. Kosa/dhambi kubwa sana hii kumwagamwaga vyakula.
I showed this comment to my wife. Kila mara namwonya kuhusu hili. Lakini siku nikiingia jikoni lazima nikute chakula kimemwagwa.
 
Kuna Mwalimu wa somo la Behavioral science alituambia kua mojawapo ya alama ya kua umeelimika ni kutomaliza chakula unapokula
Mpaka leo hua nadhani yule mwalimu na wenzake wenye mtazamo huo ni wapumbavu
Unaposoma shuhuda kama hizi halafu anachezea chakula kwa kukimwaga ili aonekane ameelimika na kustaarabika ,pumbavu kabisa
 
I showed this comment to my wife. Kila mara namwonya kuhusu hili. Lakini siku nikiingia jikoni lazima nikute chakula kimemwagwa.
Ajue maisha sio rahisi namna hiyo, lakini pia akumbuke privilege aliyonayo na familia yake kuna wengine hata hayo makombo wanayatamani.

Nasikitika tu kuwa wapo wanawake hawajui kupima chakula, ni hawawezi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…