Ni dawa gani ya usingizi wanayoitumia wezi kupuliza madirishani?

Nasikia eti ni dawa za mahospitalini...za nusu kaputi...hivyo watu wa hospitalini wanahusika; sababu haziuzwi madukani...Na ni zina side effect.
Kuna duka Cape town South niliingia nikakuta spray za kumpulizia adui machoni zinauzwa madukani, wenyeji wakaniambia ndio self defence kubwa ya wanawake.

Kwahiyo kwa uzoefu wangu mdogo naamini kabisa hata hizi spray za kunogesha usingizi zitakuwa wanazipata kutoka South Afrika, kule vitu vingi siyo ilegal.

Hata Manyaunyau ile midoli yake ya paka yenye chill sourse inayofana na rangi ya damu atakuwa anainunuwa South Africa.
 
Point yangu ni kuwa hao wezi walikuwa na muda mrefu wa kufanya mambo yao mpaka kuwa na confidence ya kuamua waoge kabisa.

Wezi mara nyingi wanakuwa wanafanya mambo yao halafu wanapotea haraka eneo la tukio, ila hawa waliamua waoge kabisa
Wewe unazungumzia vibaka wakwapuaji, hawa ni wezi professional. Kuna sehemu moja kule Ubungo Dar, wezi walienda kwa mama mmoja mfugaji wa kuku wa mayai. Kuku wake walikuwa wapata miezi 6 ndio wameanza kutaga yai moja moja. Hao jamaa walikuja na majiko ya mkaa na sufuria kubwa kama ya Miraji Mapilau.

Yule mama mara ya mwisho kuwaona kuku wake ilikuwa saa kumi na nusu alfajiri alipoenda bandani kuwaongezea chakula na maji. Jamaa waliingia bandani, wakachinja kuku, wakanyonyoa na kuondoka na mzigo. Mama aliambulia Jiko la Mkaa, Sufuria, Manyoya, miguu na vichwa vya kuku wake 400. Hiyo ilikuwa saa 3 asubuhi alipoamshwa na majirani walioenda kuchota maji nyumbani kwake.

Usicheze na fani za watu mkuu.
 
Hahah umenikumbusha mbali msisiri vinyago pale zone kule kamanyora hahah
Kitambo sana tushawafataga Wezi pale na walikuwa wanashirikiana na Wezi Kino ngambo ya pili,tuliwachkuagaa wezi/wakabaji tukawaletaaa biafraaa machinjioni walichifanywa mbona heshimaa sehemu yetu ilirudi.....
 
hahah..nimependa ulivyopinga..Lakini je mtu akibisha akakwambia hakuna kibaka mwenye elimu ya saikolojia kiasi hicho?..
 
Mimi nimepitia maelelezo yooote hapa lakini kila nikijaribu kuunganisha kwa kutumia sayansi naona nyota nyota
''sayansi'' ipi ambayo hujatumwagia hapa jamvini?..Hujaonesha hata chemical formula zake 😀😀..
ebu tupatia chemical reaction basi...
 
Point yangu ni kuwa hao wezi walikuwa na muda mrefu wa kufanya mambo yao mpaka kuwa na confidence ya kuamua waoge kabisa.

Wezi mara nyingi wanakuwa wanafanya mambo yao halafu wanapotea haraka eneo la tukio, ila hawa waliamua waoge kabisa
Na inawezekana hata kabla hawajang'oa hiyo TV walikua wanafuatilia series ya kikorea.
 
Dah! Mwaka 2013 yalinikuta. Nimekaa sebuleni na familia. Wengine wamejilaza kwenye "floor" na mimi ninaangalia sinema. Ghafla nikasikia kama mtu dirishani, sekunde chache sana nikapotelea usingizini pamoja na wote waluokuwepo sebuleni. Nimestuka masaa mawili baadae hakuna seti ya runinga, na vitu kibao na walijipakulia chakula jikoni wakaweka kwenye hotpot na kuondoka nacho. Sitosahau hiyo siku!

Kaka ...
 
oh kumbe hivi vitu hutokea kweli nimesoma uzi mzima aise pole sana
 
Kabla ya kulala weka Maji kwenye ndoo au Sufuria wakipuliza dawa yao inakimbilia kwenye maji, ukiamka asubuhi utakuta maji yana mapovu ujue walikuja usiku lakini hawakufanikiwa.
 
Wanajamii mmenipa shule sana kuhusiana na hawa jamaa ila nitashukuru sana kama tukipata dawa halisi ya kudeal na hii dawa au spray mana wengine wanasema ni maji na wengine wanasema sio maji. Nashauri ni bora tupate dawa halisi ya hii kitu kutoka kwa mtu ambae imewahi kumtokea hili jambo na hiyo dawa ikamsaidia
 
Maji tu ndio dawa tena ukishtuka ukakuta ndoo ya maji imemwagika ndio unaamka ujue walikuwa wanajitaidi kuyamwaga
 
Hata Manyaunyau ile midoli yake ya paka yenye chill sourse inayofana na rangi ya damu atakuwa anainunuwa South Africa.[/QUOTE said:
Ha haa haaaa, mkuu mbona sasa hiyo ni mada nyingine!

Kaka ...
 
Hatuwa ya kwanza kabisa ya kujikinga na spray kama madirisha yako ni ya Aluminium hakikisha yote unayalock kabla ya kulala, usiache ule wavu wa mbu kwa kutaka upate hewa.

Nadhani kwa wezi wa madirishani hii ndio hatuwa ya kwanza kuwadhibiti.
 
Mkuu umefanya nimecheka kwa muda mrefu mpaka kichwa kinauma.. Wameiba mpaka shuka, whitedent kwenye mtaro wa maji machafu, kula kila kitu na kunya bila kuflash.. [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Khaaaa waseng** wamehamisha nyumba ya mwenzao.. Wallah bahati mbaya mjengo haubebeki tu..
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] mjomba umenifurahisha sana..
 
Vipi mke wa jamaa hakuwa na dalili zozote?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…