Ni eneo gani au sehemu gani naweza kuwekeza Tsh. milioni 1 nikapata 5,000 kwa siku?

Ni eneo gani au sehemu gani naweza kuwekeza Tsh. milioni 1 nikapata 5,000 kwa siku?

Habari wananzengo.

Nina fedha ya kitanzania Tsh 1,000,000/= nataka niiwekeze mahali nipate elfu tano Kwa siku. Nipe mawazo wajumbe lengo langu mtaji upo palepale. Mimi nakuwa muwekezaji yeye anatumia fedha yangu Kama mtaji na kwa siku elfu tano yangu ananitumia
1. Tafuta kinyozi fungua saluni ya kiume
2. Fungua kibanda cha kuingiza muvi, miziki na kukodisha cd.
3. Tafuta dogo fungua biashara ya kuuza kuku wa vipande
 
Habari wananzengo.

Nina fedha ya kitanzania Tsh 1,000,000/= nataka niiwekeze mahali nipate elfu tano Kwa siku. Nipe mawazo wajumbe lengo langu mtaji upo palepale. Mimi nakuwa muwekezaji yeye anatumia fedha yangu Kama mtaji na kwa siku elfu tano yangu ananitumia
Tafuta bodabods used mpe kijana mwambie akuletee 5000 kila siku service sijui nini juu yake
 
Kama hili unaloongea unalifanya naomba twende pamoja tukalangue hao kuku.
Naenda mnadani nanunua nyama ya nguruwe kwa 5000 kwa kilo nanunua kilo 100 sawa na laki tano nawauzia wanaokaanga kwa 8000 kwa kilo naingiza faida ya 300,000/ kwa tripu moja nikitoa gharama za usafiri nabaki na 250,000/ kwa wiki naenda mara mbili kwahyo wakika wa laki tano kwa wiki. Laki Tano inayobaki nalangua kuku mnadani kwa 10,000 kwa kuku nachukua kuku 40 sawa na laki 400,000/ nawaleta town nauza kwa 15000 kwa kuku mmoja sawa na faida ya laki 2 kwa tripu kumbuka ninaponunu nyama ndo hapo hapo napo nunua kuku kwahyo nafanya biashara mbili kwa wakati mmoja.
 
Unaweza kupambania masoko ya kuku na hyo nyama kwenye mazingira unayoishi (namanisha unaweza pata wateja wakuchukua kilo mia au hamsini kwa siku).
Kama hili unaloongea unalifanya naomba twende pamoja tukalangue hao kuku.
Jipange mnada ni jumatano na jumamosi Wilaya ya Geita na Tarafa Kimwani Muleba Siku Jumatano.
 
Ila pia mleta mada mbona kama na we umetuletea ile kitu inaitwa Chemsha Bongo? Hiyo hela umeitafuta, umepewa,au umeiokota? Umejua jinsi ya kuipata ila hujui jinsi ya kuizalisha? Kweli we mleta mada aaaah inaweza kuwa unatuchezesha chemsha bongo.
Let say mtu ni mlinzi ktk kulipwa mishahara ame save mpaka imefikia hiyo pesa 1m anataka kuacha kazi ya ulinzi afanye shughuli nyingine ya kumuingizia kipato je swali lako Lina mantiki?
 
fungua kibanda cha mahitaji ya nyumbani mboga mboga, mchele,mafuta,maharage,nyanya, n.k utakuja kunishukuru baadae hii biashara inalipa sana hususa ni mkoani
 
Back
Top Bottom