Ni eneo gani au sehemu gani naweza kuwekeza Tsh. milioni 1 nikapata 5,000 kwa siku?

1. Tafuta kinyozi fungua saluni ya kiume
2. Fungua kibanda cha kuingiza muvi, miziki na kukodisha cd.
3. Tafuta dogo fungua biashara ya kuuza kuku wa vipande
 
Tafuta bodabods used mpe kijana mwambie akuletee 5000 kila siku service sijui nini juu yake
 
Kama hili unaloongea unalifanya naomba twende pamoja tukalangue hao kuku.
 
Unaweza kupambania masoko ya kuku na hyo nyama kwenye mazingira unayoishi (namanisha unaweza pata wateja wakuchukua kilo mia au hamsini kwa siku).
Kama hili unaloongea unalifanya naomba twende pamoja tukalangue hao kuku.
Jipange mnada ni jumatano na jumamosi Wilaya ya Geita na Tarafa Kimwani Muleba Siku Jumatano.
 
Ila pia mleta mada mbona kama na we umetuletea ile kitu inaitwa Chemsha Bongo? Hiyo hela umeitafuta, umepewa,au umeiokota? Umejua jinsi ya kuipata ila hujui jinsi ya kuizalisha? Kweli we mleta mada aaaah inaweza kuwa unatuchezesha chemsha bongo.
Let say mtu ni mlinzi ktk kulipwa mishahara ame save mpaka imefikia hiyo pesa 1m anataka kuacha kazi ya ulinzi afanye shughuli nyingine ya kumuingizia kipato je swali lako Lina mantiki?
 
fungua kibanda cha mahitaji ya nyumbani mboga mboga, mchele,mafuta,maharage,nyanya, n.k utakuja kunishukuru baadae hii biashara inalipa sana hususa ni mkoani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…