Ni gari gani huwezi kununua Wala kumshauri mwingine anunue?

Ni gari gani huwezi kununua Wala kumshauri mwingine anunue?

Sijui alikua na BMW mode gani labda langu lina mkosi. Sio langu tu, na za washkaji zangu zetu zina mikosi.

BM common sana Tanzania ni 3 series. Sana sana sahivi naona E90 za kutosha. Ambazo zina share platform na X3 1st generation E83 ambazo nazo zipo za kutosha.

Mzee bab, German engineering gari kali 5 years tu tokea likiwa jipya. Baada ya hapo umiza kichwa.
Mkuu tukiwaambia watu Yale Ni magari ya matajiri huwa wanabisha sana, Ile ngoma inatakiwa warranty ikiisha unachukua Chuma kingine chap.
 
1. nissan extrail, hii imeshachangiwa na members wengine humu tayari, cha kuongezea tu ni kwamba hizo nissan wenyewe walitoaga tamko kwama walibugi kwenye hizo gari, kuchemsha hilo gari ni ugonjwa mkubwa, labda ubadilishe rejeta uweke kubwa_modification

2. European cars ambazo hazijathibitshwa na wenyewe, kwamba umenunua kwa third part owners kama sbt, kwa mtu, befoward etc..yaani iwe bmw, volvo, honda etc kama umenunua used kwa mtu basi jua asilimia ya kuwajua mafundi wote hapa mjini ni mkubwa sana, nunua hata ikiwa used iwe imethibitishwa iko okay na authourised European car agent wa hayo magari..itakupa garantii kwamba sensor hazijawa bypassed etc etc engine haijawahi chezewa ili kukunusuru otherwise buy 0 km car.
ukitaka kuthibitisha hili nenda kuna mtaa mmoja hapo mwenge kule karibu na mapambano yamejaa mabmw, nenda kinondoni hananasif mtaa wote umejaa rangerover..au tembelea mitaa ya mbezi beach, makumbusho uone bmw na rangerover zimekuwa mapagale..

3. Daihatsu Terrios/ camry...automatic gear box zake mbovu

4. mazda tribute, hyundai , isuzu trooper, bighon, honda oddesy..hamna spare utachina na hela unayo, litaishia kupaki uwani liwe jumba la panya..spare mpaka nairobi au japan
5. Nissan kwa ujumla: ie terrano, navara.. hazikopeshi hizi gari, hazivumilii watu maskini, ihudumie ikuhudumie, ikose maji tu au oil mlimani inakukaangia engine dakika 0 tu..iwekee shock up og ukiweka za 80k wiki tu unayaingia mashimo mazima mazima.

Pendekezo.
Toyota ndo magari yako made for us, yanavumilia, hata ukiyawekea oil ya boda boda yatakuvumilia..nenda milimani mahenge uko utakua toyota corolla ya mwaka 89 inakilometa laki 6 na inapiga kazi mzee.
 
Nissan Xtrail generation ya kwanza. Binafsi nimemiliki na waliomiliki ambao nipo nao karibu wamepatwa na mauza uza.

Inaweza chemsha isionyeshe kwenye dash, inaweza amua isiwake tu bila sababu ukaita fundi akifika akawasha tu ikawaka na asione tatizo. Unaishia kumlipa usumbufu.

Kuna moja iligoma kuwaka ikashtakia sensor, sensa mpya ikawekwa ikagoma, kila sensor ikiwekwa inagoma ikarudishiwa ya kwake iliyokuwepo mwanzo ikakubali.
Yes Ni kweli mm pia nimeshatumia old model Nissan xtrail inazima ghafla na changamoto za kuchemsha kwa safari ndefu
 
Hii shida ilikua kwenye X5. Unatoka home vizuri tu unafika mahali unapaki.

Ikifika muda wa kuondoka kimbembe kinaanza. Unawasha inasusa for no reason...

Inabidi usubiri kidogo tena uwashe.. Unawaza kufanya attempt mara tatu hadi 4 ndio inakubali...

Ikawa sasa ukienda mahali inabidi Ukikaribia muda wa kuondoka unatoka unatest ikigoma unarudi kuendelea na mambo mengine... Ikikubali ndio hapo hapo inabidi uondoke

Sent from my MAR-LX1A using JamiiForums mobile app
Ninaamini mwishoni mlikujankujua tatizo ni electric fuel pump kuwa ilikuwa imekufa. Mlipobadili tu, tatizo likaisha
 
Back
Top Bottom