Ni halali Wazanzibari kufanya kazi za Watanganyika?

Ni halali Wazanzibari kufanya kazi za Watanganyika?

Hawajawahi kusema hawataki muungano! Kumbuka Maalimu kafariki hakuwahi kusema hataki
Kwasasa wanaweza kuvunja kwani Marais wote ni Wazanzibar, kwanini wanashindwa.
Kwanini wasisuse kuja Dodoma, waondoka katika nafasi za JMT ili muungano ufe
Nitajie Mzanzibar mmoja tu wa ndani na nje anayesema hataki muungo (siyo waarabu )

Ndio maana tuna wa encourage, fursa ya kuvunja muungano ni sasa. SSH na Mwinyi itisheni referendum haraka sana Zanzibar, fanyeni mnavyoweza , vunja muungano! hakuna tatizo. Wanasita nini

Hii prestige ni kweli lakini sasa ni too much. Watu chini ya milioni wanapewa resources nyingi kuliko mamilion ya watu. Hili linakera sana. Halafu hata mchango hawana, na kile chao wanakimbiza kama mafuta, umuhimu wa resources kuelekezwa huko ni upi?

Muungano ni nguvu za kiuchumi na kiusalama.
Watanzania bara hawana tatizo na Wazanzibar ndio maana wanawakubali huku bara ila ubaguzi wala masharti
Mbegu chafu ya ubaguzi inapandwa na Wazanzibar wanaoamini Uzanzibar ni ubora
Hilo ndilo linawatibua Watanganyika hasa wakijua ubora wa Zbar ni kivuli cha Tanganyika!

Waulize Wazanzibar ambao hawautaki Utanzania bali pale tu wanapoona kuna mafao
Mbegu ya ubaguzi wanaipanda wao na itawatafuna sana maana nje ya muungano kuna kipili pili na mashombe

Mbona Tanganyika inapakana na nchi 8! kwani tuna masilahi sawa?
Kumbuka Zenjibari hakuna vyanzo vya kuzalisha umeme. Muungano ukivunjika kisha Tanganyika ikikataa kuuza umeme huku je? Au umesahau kuwa mwaka 2016 Zanzibar iliwahi kwenda miezi mitatu bila ya umeme. Hali ilikuwa tete. Kipindi hicho bado sikuwa naishi huku ila simulizi zinasema kuwa hali ilikuwa mbaya
 
Hapana swali ni hili, SMZ inachangia nini? Hatuzungumzii mtu binafsi.

Ikitokea suala la kugawana Wazanzibar wanataka usawa, je, wao wanachangia nini?

Kumbuka muungano hauendeshwi kama jahazi la upepo.
EeeenHeeee Heee!
Tuanze na swali hili: Je SMZ inapato kiasi gani? Tukishapata jibu, ni halali mchango wao uendane na pato lao. Kama sasa hivi hawachangii chochote, huo ni unyonyaji alioukataa Mwalimu.
 
Hawajawahi kusema hawataki muungano! Kumbuka Maalimu kafariki hakuwahi kusema hataki
Kwasasa wanaweza kuvunja kwani Marais wote ni Wazanzibar, kwanini wanashindwa.
Na kama hili linafahamika vizuri, kwa nini viongozi wenye asili ya Tanganyika hushiriki kuwadekeza na mambo ya "kero za Muungano" zisizokwisha? Kuna sababu gani za "kuwahonga" watu ambao inajulikana wazi hawawezi kujiondoa kwenye Muungano kwa vile Muungano unamaslahi makubwa kwao?

Binafsi ningependa kuanzia hapa. Tuache tabia za kudekeza watu.
Mbona Tanganyika inapakana na nchi 8! kwani tuna masilahi sawa?
Kuna tofauti kubwa sana kati ya hizo nchi nane tunazopakana nazo na kupakana kwetu na Zanzibar.
 
Muungano hautovunjika bali unaweza ukaboreshwa !! Let say kama Rasimu ya katiba ya Mzee Warioba ilivyopendekeza !! Serikali tatu ! Au vipi ??!
Serikali tatu ni kufifisha muungano bila sababu. Serikali ni moja tu basi!

Serikali mbili zilikuwa ni za mpito kuelekea kwenye moja; wakati umewadia hilo litimizwe.
 
Watanzania bara hawana tatizo na Wazanzibar ndio maana wanawakubali huku bara ila ubaguzi wala masharti
Mbegu chafu ya ubaguzi inapandwa na Wazanzibar wanaoamini Uzanzibar ni ubora
Na hapa ndipo panapotakiwa kuwekwa tahadhari kubwa. Hiki kikundi kilichopo huko Zanzibar sauti yao inakuzwa sana kuliko uhalisia ulivyo; na mbaya zaidi, sisi wenyewe (waTanganyika) nasi tunaweza kujikuta tukisaidia kukuza sauti hiyo tunapoonyesha kwamba ni waZanzibari wengi wasiopenda Muungano. Tutakuwa tunajiunga na kikundi hiki bila hiari yetu katika juhudi za kuudhoofisha Muungano.

Kinachotakiwa ni kuwakabili hawa watu kwa hoja za kuimarisha Muungano, na siyo kuudhoofisha kwa kudai Tanganyika nayo ishikirie ya kwake.
 
Na kama hili linafahamika vizuri, kwa nini viongozi wenye asili ya Tanganyika hushiriki kuwadekeza na mambo ya "kero za Muungano" zisizokwisha? Kuna sababu gani za "kuwahonga" watu ambao inajulikana wazi hawawezi kujiondoa kwenye Muungano kwa vile Muungano unamaslahi makubwa kwao?

Binafsi ningependa kuanzia hapa. Tuache tabia za kudekeza watu.

Kuna tofauti kubwa sana kati ya hizo nchi nane tunazopakana nazo na kupakana kwetu na Zanzibar.
Kwa walioishi miaka mingi watakumbuka kuwa Zanzibar walikuwa na msemo '' Msipofanya abcd tunavunja muungano'' kudekezwa kulikwisha walipoambiwa kama hawaondoi sharti la passport nao na passport.

G55 ikamaliza mzizi wa kudekezwa, ikasema Tanganyika iwepo ishughulike na mambo yake

Kinachotokea sasa hivi ni ni Rais kuwadekeza! Mfano, angalia mikopo iliyokwenda Zanzibar kwa watu laki 6 na ile ya mkoa wa Dar es Salaam ya watu milioni 7.
 
EeeenHeeee Heee!
Tuanze na swali hili: Je SMZ inapato kiasi gani? Tukishapata jibu, ni halali mchango wao uendane na pato lao. Kama sasa hivi hawachangii chochote, huo ni unyonyaji alioukataa Mwalimu.
watu hawasemi Zanzibar kwa uchumi mdogo kuliko mkoa wa Tanganyika inaweza kuchangia nusu kwa nusu. Kinachosemwa hapa ni kuwa kidogo chao kipo wapi?

Mikopo wanayochukua wanalipa wapi?
Umeme hawalipi! Ni wakazi wa wilaya kata au kaya gani Tanganyika wanalipiwa umeme na JMT?
 
Yes kama nchi zimeungana na Zanzibar inataka usawa, ofisi hizo zijengwe huko na kuhudumiwa na kodi za Wazanzibar. Hapa ndipo tatizo lilipo, kwamba itabidi Watanganyika wahudumie kwavile tuna ushahidi Zbar haichangii muungano. Huku ni kumbebesha Mtanganyika mzigo kwasababu Rais wa JMT makao yake yapo Dodoma na Dar huko kwingine ni kupita siku moja moja, likewise VP na PM

Zanzibar wajenge majengo kadri wanavyotaka kwa gharama zao na wahudumie kwa gharama zao ili kupunguza gharama kwa Watanganyika.

Zanzibar haiwezi kuwa na haki sawa kwenye mafao, wapi usawa wao kwenye kuchangia na kuhudumia muungano? Usawa gani Tanganyika waweke 100 Zanzibar 0 halafu tugawane 50! Hesaabu hizo zipo Zanzibar tu, pale wanapotaka usawa bila kuchangia.
Hapa ni Tanzania na si swala la Tanganyika au Zanzibar. Ukeshalitambus hili ndo utajua pia umuhimu wa Zanzibar kujengwa ofisi. Hakuna Tanganyika inayochangia ila ni TANZANIA kwa ukamilifu wake.
 
Serikali tatu ni kufifisha muungano bila sababu. Serikali ni moja tu basi!

Serikali mbili zilikuwa ni za mpito kuelekea kwenye moja; wakati umewadia hilo litimizwe.
Wazanzibari hilo hawatalikubali kamwe !!
 
Hii ndio hoja ya msingi ya serikali tatu, rais wa muungano na wa Zanzibar wote ni wazanzibari, nani anatetea maslahi ya Bara ndani ya Muungano? Bara inaporwa tu hakuna wa kuitetea, waliopigania Uhuru wa Tanganyika wanadhihakiwa mno
Alaumise CCM.
 
Nikiona hoja kama hizi napata hasira sana kwa Maana zinatuumiza sana kichwa tusio na maamuzi wakat wenye maamuz wanaziwngalia tu[emoji1784][emoji21]
 
2025 ni karibu sana kiuchaguzi ikiwa kutakuwa na mipango husika ya kuelekea huko, binafsi nakataa kata kata kuongozwa na mzanzibar ikiwa chama chochote cha siasa kitamteua kugombea, nitaunga upande mwingine. Narudia kwa mara nyingine, Raisi aliyepo ametokana na katiba ya nchi na watanzania temeheshimu hilo,tusubili 2025 kuona nini kitatokea.
Unaota wewe yaani kula yako wewe unadhani inabadilisha nini?
Huyo bichwa nundu JPM,rest in hell,aliyewaweka wakina kwanaFA na Babu tale na kushinda majimbo yote ya bara alikua mzanzibar?
 
Nguruvi3 hoja zako mbili ndiyo za kufanyia kazi.

Wazanzibari waulizwe kama wanautaka Muungano, wakisema wanautaka ni lazima wakubaliane na Muungano utakaotoa faida stahiki kwa Tanganyika.

Wakisema hawautaki Muungano tuagane nao kwa salama na wakubaliane na mahusiano mapya bila ya kinyongo. Scotland, Ireland, na Great Britain wanaishi hivyo sasa kwa kuheshimiana.
 
Formula yetu ni ya ajabu kidogo

Iko hivi, Mzanzibari ana haki zote za Mtanganyika na Mzanzibari
Ila Mtanganyika ana haki tu za hapa Tanganyika, mambo ya Zanzibar hayamuhusu.
 
Formula yetu ni ya ajabu kidogo

Iko hivi, Mzanzibari ana haki zote za Mtanganyika na Mzanzibari
Ila Mtanganyika ana haki tu za hapa Tanganyika, mambo ya Zanzibar hayamuhusu.
Ni formular ya ajabu lakini tunaiona haiwezi kubadilishwa.
 
Back
Top Bottom