Hebu kwanza!Nawaza sana mantiki ya kwenda kujenga Ikulu ndogo Zanzibar, ofisi ya Makamu wa Rais, na cha kustaajabisha sana ofisi ya waziri Mkuu. Hivi Waziri Mkuu ni mambo ya Muungano?? Hivi hawajui ni kwa nini tuna Waziri Mkuu kwenye serikali ya Muungano Tanzania?
iko siku tutakuwa na Waziri Mkuu toka Zanzibar na watanganyika watakaa kimya.
Tukiangalia upande wa pili wa shilingi (sarafu) ambayo haipo tena)!
Hivi mipango ya aina hii haiwezi kutumika kuwafunga zaidi wanaotafuta kujitenga huko visiwani?
Nina maana ya kwamba, mipango kama hii iwe ndiyo sababu ya kuufanya Muungano uwe karibu zaidi; hizi zikiwa hatua za kutupeleka kwenye "serikali moja" kwa mfano!
Sina maana ya kusema hapa kwamba hawa viongozi wanaofanya haya wanayafanya kwa nia hiyo; lakini haya yanaweza kuzalisha kitu ambacho hawakukitegemea kabisa, kukiwa na kiongozi mwenye ushawishi wa kustawisha muungano.
Ni wazo tu.