Ni halali Wazanzibari kufanya kazi za Watanganyika?

Ni halali Wazanzibari kufanya kazi za Watanganyika?

Nenda Jozani pale utakutana na kina Sara na Josephu wanafanya kazi kwenye taasisi ya utalii. Mambo ya muungano hayajulikani tena, but I hope Jozani sio taasisi ya muungano.
Hao kina Sepetu wapo huko hata kabla John Okello hajampindua Sultan Jamshid!! Au hujui mbali ya wangazija na washirazi pia Machogo wa Tabora nao wapo Zanzibar tangu enzi za utumwa??
 
Nguruvi3 wakati mwingine nikiwaza nguvu ya waziri mkuu huwa najiuliza nguvu yake bungeni. Ukiangalia hakuna wakati Bunge la Tanzania linajadili mambo mahsusi ya Tanganyika. Kila wakati wakati tunajadili mambo ya Nanjilinji Kilwa, na mbunge wa kiembesamaki naye anachangia. Ila wao kwenye baraza la wawakilishi hakuna Mtanganyika anayejadili mambo yao.
Ni hivi hili la Wabunge linatatizo sana. Kwanza Wabunge wa Zanzibar wanachaguliwa na watu 2,000 lakini wana kura sawa na Mbunge wa Ubungo mwenye watu Milioni 1 na ushee wengi kuliko Zanzibar.

Pili, wanatumia gharama za Tanganyika kuja kuwakilisha Zanzibar na si gharama zao.

Tatu, wanakaa Dodoma muda mrefu wakizoa pesa tu na kujadili mambo yasiyowahusu
Yanayowahusu hayazidi 10, hivyo walitakiwa wakae siku chache waondoke ili kupunguza gharama

Nne, Wabunge wa Zanzibar wapo katika kamati za kukagua mambo ya Tanganyika

Tano, wanapiga kura kukubali au kukataa mambo yasiyo ya Tanganyika.

Mfano, wanapiga kura za TOZO ambazo huko Zanzibar hazipo.
 
Kama ni hivyo kwann mtanzania bara haruhusiwi nunua ardhi Zanzibari kama kweli sisi wote ni uraua mmoja ambao ni JMT????
Tanzania ni the majority kila Mtanzania akiwemo Mzanzibari ana haki zote Tanzania yote ila Zanzibar ni the minority, haki ni kwa Wakaazi wa Zanzibar pekee. Mtanzania unaweza kumiliki ardhi Zanzibar kama mwekezaji.
P
 
Naona miropoko mingi.
Kimsingi wewe Mtanganyika huna ruhusa ya kujiunga na askari wa vikosi vya Zanzibar, mfano KMKM,KVZ,KIPANGA au MAGEREZA au ZIMAMOTO kwa sababu askari wa vikosi hivi wanalipwa na SMZ ambayo ni SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR na sio serikali ya JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.
Wapo Watanganyika waliojiunga ila kwa sheria maalum ambayo ni lazima uwe na kitambulisho cha Mzanzibari mkazi. Na hicho kitambulisho ili ukipate unatakiwa uwe na uthibitisho kuwa umeishi Zanzibar kuanzia miaka 10 au zaidi. Vinginevyo vaa chupi kaa pembeni
 
Tanzania ni the majority kila Mtanzania akiwemo Mzanzibari ana haki zote Tanzania yote ila Zanzibar ni the minority, haki ni kwa Wakaazi wa Zanzibar pekee. Mtanzania unaweza kumiliki ardhi Zanzibar kama mwekezaji.
P
Hii hoja yako ni kama unajipinga mwenyewe bwana Paskali. Kama Mzanzibari na Mtanganyika wote wana hadhi sawa ndani ya Jamhuri ya Muungano Tanzania, ni kwa nini Mtanganyika amiliki ardhi Zanzibar kama mwekezaji (Yaani siyo raia) wakati Mzanzibar huku Tanganyika anamiliki Ardhi kama amilikivyo Mtanganyika?
 
Hakuna sababu za kujenga ikulu hizo ambazo basically zinahudumiwa na kodi za Watanganyika. Wazanzibar hawana mchango wowote kwahiyo hili ni kuongeza mzigo kwa mlipa kodi. Ndio Tozo mnazolundikiwa kuhudumia vitu visivyo na maana kama hivi
Hakuna sababu kujenga ikulu Zanzibar? Hivi huyo Rais wa Tanzania akija Zanzibar si atafikia ikulu? Unataka afikie ikulu gani? Hivi rais wa Jamhuri huwa Zanzibar haimuhusu?
 
Hakuna sababu kujenga ikulu Zanzibar? Hivi huyo Rais wa Tanzania akija Zanzibar si atafikia ikulu? Unataka afikie ikulu gani? Hivi rais wa Jamhuri huwa Zanzibar haimuhusu?
Rais wa Zanzibar si ana Ikulu? Kwani Marais waliotangulia walikuwa wakija Zanzibar walikuwa wanafikia wapi?
 
Nguruvi3 Jinsi ambavyo hakuna nafasi ya kujadili mambo ya Tanganyika kwenye Bunge la Tanzania, ndivyo hoja ya kuwepo kwa serikali tatu ama serikali za majimbo inavyopata mashiko.
 
Rais wa Zanzibar si ana Ikulu? Kwani Marais waliotangulia walikuwa wakija Zanzibar walikuwa wanafikia wapi?
Akifikia hoteli au nyumba ya SMZ. Kumbuka: inayotaka kujengwa ni ikulu ya JMT. Ila kimsingi ikiwa haikujengwa itaipunguzia Zanzibar ya kutoa ardhi ila nachangia ili kuwaelimisha wale wasiojua.
 
Nguruvi3 Jinsi ambavyo hakuna nafasi ya kujadili mambo ya Tanganyika kwenye Bunge la Tanzania, ndivyo hoja ya kuwepo kwa serikali tatu ama serikali za majimbo inavyopata mashiko.
Ni wazi Tume ya Warioba iliona tatizo hilo na tume nyingi tu zilishauri

Kuna mambo 7 tu ya pamoja, mengine kila nchi ishughulike na yake

Ikiwa wanataka muungano ni Wazanzibar watakaoamua, wanahitaji Tanganyika si vingenevyo.
Ikiwa hawataki nani awazuie? na Kwanini?
 
Akifikia hoteli au nyumba ya SMZ. Kumbuka: inayotaka kujengwa ni ikulu ya JMT. Ila kimsingi ikiwa haikujengwa itaipunguzia Zanzibar ya kutoa ardhi ila nachangia ili kuwaelimisha wale wasiojua.
Tangu 1964 hatujawahi kuwa na Ikulu, hakuna sababu

Haya yote ni kujenga majengo ili wazanzibar wapate ajira, gharama anabeba Mtanganyika.
 
Akifikia hoteli au nyumba ya SMZ. Kumbuka: inayotaka kujengwa ni ikulu ya JMT. Ila kimsingi ikiwa haikujengwa itaipunguzia Zanzibar ya kutoa ardhi ila nachangia ili kuwaelimisha wale wasiojua.
Kwa nini inatamaniwa Rais wa JMT ajengewe Ikulu mahali ambapo hana uwezo hata wa kuteua Mkuu wa wilaya. Huoni Ikulu ya JMT inakwenda kujengwa kwenye eneo ambalo Rais wa JMT hana mamlaka nako?

Hiyo Ardhi itakuwa ni ya JMT ama itakuwa ya SMZ na itatambulikaje kisheria, ni ardhi ya nchi ya kigeni kama zilivyo Ardhi wanazopewa mabalozi wa nchi za nje Tanzania kujenga ofisi zao ama itatambulikaje?
 
Ingallikuwa zama za Wabunge wa G55 haya yasingetokea, ni uharibifu wa pesa halafu kumbebesha Mtanganyika Tozo.
Tungekuwa na watanganyika wenye elimu bora ya Uraia wangewahoji wabunge waliko sasa bungeni kwenye uchaguzi wa 2025 kuwa ni kwa nini walikuwa Bungeni bila ya kutetea maslahi ya watanganyika?
 
Tungekuwa na watanganyika wenye elimu bora ya Uraia wangewahoji wabunge waliko sasa bungeni kwenye uchaguzi wa 2025 kuwa ni kwa nini walikuwa Bungeni bila ya kutetea maslahi ya watanganyika?
Yes kama tungalikuwa na elimu ya Uraia hili wangeulizwa wabunge na huenda ingalihitimisha ubunge wao
Hata hivyo kwa kizazi cha sasa kuna matumaini kuwa ipo siku wapo watakaoonja joto ya jiwe
Kwanini kero zitatuliwe kwa usiri? Nani anajua zimetatuliwa vipi?

Akina PM na VP watakumbana na hoja ya Tanganyika siku moja.
 
Nawaza sana mantiki ya kwenda kujenga Ikulu ndogo Zanzibar, ofisi ya Makamu wa Rais, na cha kustaajabisha sana ofisi ya waziri Mkuu. Hivi Waziri Mkuu ni mambo ya Muungano?? Hivi hawajui ni kwa nini tuna Waziri Mkuu kwenye serikali ya Muungano Tanzania?

iko siku tutakuwa na Waziri Mkuu toka Zanzibar na watanganyika watakaa kimya.
Sikutaka "kushangaa", nikaona bora "nisikitike"!
Haya uliyoandika hapa ni moja tu ya mambo yanayosikitisha sana yanayofanywa na serikali ambayo wananchi wanaichukulia kuwa ina watu makini wanaotekeleza mipango ya nchi yao kwa weledi!

Mbaya zaidi, hakuna chombo chochote kinachoweza kuhoji maamuzi ya namna hii. Hii ni nchi au ni jalala tu la mtu binafsi analoweza kutumia anavyotaka? Hii ni dharau kwa wananchi.

This is too much!
 
Back
Top Bottom