Ni halali Wazanzibari kufanya kazi za Watanganyika?

Ni halali Wazanzibari kufanya kazi za Watanganyika?

Kwa nini inatamaniwa Rais wa JMT ajengewe Ikulu mahali ambapo hana uwezo hata wa kuteua Mkuu wa wilaya. Huoni Ikulu ya JMT inakwenda kujengwa kwenye eneo ambalo Rais wa JMT hana mamlaka nako?

Hiyo Ardhi itakuwa ni ya JMT ama itakuwa ya SMZ na itatambulikaje kisheria, ni ardhi ya nchi ya kigeni kama zilivyo Ardhi wanazopewa mabalozi wa nchi za nje Tanzania kujenga ofisi zao ama itatambulikaje?
Mkuu Kilewella are you serious? Hivi hujui kweli kwamba Rais wa JMT ana madaraka gani? Au ndo choyo? Kule Zanzibar kuna ofisi za BOT, Uhamiaji, Posta, simu na nyingine. Hizi zinatambulika ni ardhi gani? Hemu tuwe serious wakati wa kutoa michango hapa JF. Wenyewe wanasema JF home of great thinkers. Tuchangie tukitilia maanani hili.
CC: brazaj
 
. Ninachouliza ni athari gani mnaziziona?

Wazanzibar waulizwe kama wanataka muungano au la!

Mtanganyika asiulizwe haimhusu wala haathiriki na chochote au lolote lile ukivunjika.
Kwanza nitangulie kwa hoja yako ya mwisho kwamba ni wazanzibari ndiyo wanatakiwa waulizwe kama wanautaka Muungao ama la. Kwa mujibu wa Mwalimu (na ndiyo mtizamo wangu pia) kwenye kitabu chake cha "Uongozi wetu na hatima ya Tanzania" alishangaa ni kwa nini viongozi wa CCM wanashindwaje kuwauliza Wazanzibari swali rahisi kama hilo.

Lakini pia Mwalimu aliamini wazanzibar wakiulizwa na wakipewa uhuru wa kulijibu swali hilo, ni LAZIMA watakataa kuuvunja Muungano. Miaka 29 baadaye bado CCM haiwezi kuwauliza Wazanzibari kama wanautaka Muungano au la!! Leo kina Njelu Kasaka, Jenerali Ulimwengu na wenzao, nadhani wanajuta ni kwa nini hawakuendelea na hoja yao ya kuidai Tanganyika ndani ya Muungano wakati ule.

Athari zitakazotokana na kuvunjika kwa Muungano zina sababu mtambuka. Leo ukiangalia kwa makini andiko la Abdulrahaman Kinana kwenye Jarida la "The Hill" la nchini Marekani, iliyokuja kutiwa utambi na William Lukuvi wakati wa Uchaguzi wa 2015 kuhusu Uislam na Ugaidi Zanzibar, ingawa ilikuwa hoja ya kipropaganda, lakini Muungano ukivunjika italeta athari.

Athari itakayojitokeza ni kwamba ndani na nje ya Zanzibari kuna watu wanaamini kwamba ili Zanzibar "iwe salama" ni lazima iongozwe kwa kufuata misingi ya Kiislam. Na hata zile kauli za kutunza historia na utamaduni wa Zanzibar Mara nyingi hulenga kuonesha kwamba mambo ya dini ya Kiislam ndiyo utamaduni na HIstoria ya Zanzibar.

Tatizo litaanzia pale wapo wale wanaoamini Zanzibar inatakiwa kutawaliwa kwa kufuata misingi ya dini ya Kiislam kama inavyotawaliwa Afghanistan, lakini wapo pia wale watakaotaka itawaliwe kama Oman ama Qatar. Kama makundi haya yakihasimiana yakiwa yenyewe tu, bila ya shaka athari zake lazima zitafika Tanganyika.

Lakini kuna swali la wale Wazanzibari waliozaliwa Tanganyika na kuzaliana na kuzaliana, lakini wakiwa bado wanataka kutunza utambulisho (Identity) wao lakini wakiwa hawataki kurudi Zanzibari lakini kwa wakati huo kuna shinikizo toka kwa watanganyika kwamba Wazanzibari wote warudi kwao.

Kwenye hizo harakati za kila mtu "arudi kwao" kunatokea makundi makubwa matatu. Wapo watakaotaka warudi wakiwa mikono mitupu na kuacha kila kitu huku Tanganyika, wapo watakaruhusu waondoke na vitu vyao na wapo ambao wao waondoke na vitu vyao au waviache si jambo la msingi bali kuondoka kwao ndiyo watakachokitaka.
 
Mkuu Kilewella are you serious? Hivi hujui kweli kwamba Rais wa JMT ana madaraka gani? Au ndo choyo? Kule Zanzibar kuna ofisi za BOT, Uhamiaji, Posta, simu na nyingine. Hizi zinatambulika ni ardhi gani? Hemu tuwe serious wakati wa kutoa michango hapa JF. Wenyewe wanasema JF home of great thinkers. Tuchangie tukitilia maanani hili.
CC: brazaj
Kama kweli zinajengwa ofisi za Ikulu , VP na PM huo ni upotevu wa pesa za umma mkubwa, na unaongeza gharama za kuhudumia ofisi kwa Mtanganyika anayeumia na tozo sasa hivi.
Kumbuka ofisi hizo zinahudumiwa na JMT ambapo tuna ushahidi wa kutosha Zanzibar haina mchango

Kwasasa taasisi zote za usalama, ulinzi, mambo ya nje n.k. zinabebwa na kodi za Watanganyika.
Hivyo kujenga ofisi nyingine zisizokuwa na kazi ili kutoa ajira kwa Wazanzibar ni jambo la kulaaniwa sana

Kumbuka Nyerere, Mwinyi, Mkapa, JK , JPM hakuna aliyefikiria wazo la hovyo kama hilo. Walijua Waziri mkuu wa Tanzania hahitaji ofisi mahali asipokuwa na kazi napo. VP ofisi yake haina kazi Zanzibar
Tuna Ikulu Dar na Dodoma na maeneo mengine kwasababu shughuli za Rais wa JMT asilimia 90 zipo bara

Ni rahisi na nafuu sana kumweka Rais , VP na PM katika Hoteli ya nyota tano Zanzibar kuliko kujenga majengo yasiyokuwa na maana ili kujaza watu tu kwa kuwapa ajira kwa gharama za Watanganyika

Huu ni uharibifu mkubwa sana wa pesa, hatuhitaji ofisi hizo Zbar kwa hoja yoyote isipokuwa uharibifu na matumizi mabaya ya resources bila kujali anayebeba gharama hizi ni Mtanganyika peke yake si Mzanzibar.
 
Kumbuka Nyerere, Mwinyi, Mkapa, JK , JPM hakuna aliyefikiria wazo la hovyo kama hilo. Walijua Waziri mkuu wa Tanzania hahitaji ofisi mahali asipokuwa na kazi napo.
Bado huelewi! Ofisi ya VP ilianzwa wakati wa JK na kumalizwa wakati wa JPM.
Huu ni uharibifu mkubwa sana wa pesa, hatuhitaji ofisi hizo Zbar kwa hoja yoyote isipokuwa uharibifu na matumizi mabaya ya resources bila kujali anayebeba gharama hizi ni Mtanganyika peke yake si Mzanzibar.
Bado huelewi! Ofisi hizi ni za JMT ambayo Zanzibar ina haki sawa na Tanganyika kwani nchi hizi ndizo ziliungana kuunda JMT. Ikiwa ni sawa kuwa na Ofisi Dar na Dodoma kwanini isiwe sawa kuwa na Ofisi ndogo Zanzibar? Gharama hizi zote zinatoka JMT ambapo Zanzibar ni mshirika wa Tanganyika ISIYOKUWEPO.
 
nop kuna tanzania na zanzibar,
nilisafiri nje nchi flani nikakuta kuna chama cha diasporas cha watanzania na pia kuna chama cha wanzanzibar.
Hawa wanzanzibar hawapo kabisa kwenye. chama cha watanzania ilhali pasport wanazotumia ni sawa zote za jamhuri ya muungano wa Tanzania. Na pia wamejiandikisha kwenye ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Nikajaribu kuwadodosa watanzania wezangu mbona mmejitenga?
Wakanijibu Wazanzibari ni wabaguzi sana hata kule hawajitambulishi kama watanzania wanajitambulisha ni Wazanzibari.
Kwa kifupi kuna tatizo kubwa sana watawala wamelifumbia macho.
Ila ujinga huu aliutaka Mzee wetu RIP JK Nyerere.
The same kwenye ishu ya ardhi wao wao huku wanamilikishwa ardhi sawasawa kama watanzania wa bara ila mtanzania wa bara kwa zanzibar haiwezekani sanasana atakodishiwa kama mwekezaji mgeni rejeeni clip Askofu Mkuu Jimbo la Zanzibar alivyomchana live Rais wa Zanzibar kuhusu suala la umilikishwaji ardhi wa bara huko Zanzibar.
Ndio maana kuna hitajiko la Katiba Mpya hususani ile rasimu ya Jaji Warioba bila mabadiliko yeyote ifanywe ndio Katiba ya Nchi

Wewe ndiyo mbaguzi. Kwa nini hupigi kelele Wakenya, Wanyarwanda, Waganda, na wengineo hawajitambulishi kama Waafrika wenzako? Wanajitambulisha tu kama Wakenya, Wanyarwanda, Wanaigeria, n.k. Wazanzibari wakijitambulisha kama Wazanzibari kinakuuma. Huo ni ubaguzi. Kukataa kuutambua Uzanzibari wa Wazanzibari ni ubaguzi.

Free Zanzibar.
 
Bado huelewi! Ofisi ya VP ilianzwa wakati wa JK na kumalizwa wakati wa JPM.

Bado huelewi! Ofisi hizi ni za JMT ambayo Zanzibar ina haki sawa na Tanganyika kwani nchi hizi ndizo ziliungana kuunda JMT. Ikiwa ni sawa kuwa na Ofisi Dar na Dodoma kwanini isiwe sawa kuwa na Ofisi ndogo Zanzibar? Gharama hizi zote zinatoka JMT ambapo Zanzibar ni mshirika wa Tanganyika ISIYOKUWEPO.
Zanzibar inachangia asilimia ngapi kwenye fuko la Tanzania?
 
Lakini hii siyo athari ya kuvunjika muungano. Ninachouliza ni athari gani mnaziziona?

Wazanzibar waulizwe kama wanataka muungano au la!

Mtanganyika asiulizwe haimhusu wala haathiriki na chochote au lolote lile ukivunjika.
Naomba radhi kwa kutoelewa swali nilipojibu mara ya kwanza, kuhusu "athari zinazotokana na muungano kuvunjika."

Hata ukiwauliza Zanzibar, wao pia watakwambia hawataathirika kutokana na muungano kuvunjika (hasa wale wanaopiga kelele kila siku kulaumu waasisi wa muungano na kutaka muungano usiwepo0.

Hawa wanaamini, muungano ukivunjika tu, neema inaiangukia Zanzibar wanayoiona kama kuwa na muungano ndiko kunakozuia neema hizo; kuwa kama Singapore!

Kwa Tanganyika, pamoja na kujiona kuwa inautua mzigo mzito unaoielemea; ikiwa na pamoja na maudhi mengi ya kelele, kuvunjika kwa muungano pia itakuwa ni athari kwetu hata kama siyo athari iliyo wazi (tangible). 'Prestige' ya nchi pamoja na kuwa ni kama 'jambo tu la kuamini (abstract), lakini lina umuhimu wake. Kwa hiyo siyo jambo la kubeza.

Nadhani katika kujibu swali kama hili, inabidi pia kuuliza swali jingine: Hivi kuna sababu zipi ambazo hufanya nchi zipende kuwa na muungano? Tusitazame tu udogo wa Zanzibar na ukubwa wa Tanganyika katika kujibu swali kama hili.
Hivi katika raia wetu Tanzania, kuna tofauti zipi ambazo zinatufanya tuonekane kuwa watu wa mataifa mawili kuliko kuwa taifa moja? Tofauti zetu ni zipi zinazotufanya sisi tuwe upande mmoja na wao wawe upande mwingine kama nchi tofauti?

Tukiondoa haya yanayochochewa na wanasiasa kutufanya tuonekane tofauti, kweli mZanzibari anayo tofauti kubwa na mTanganyika kiasi kwamba hawawezi kuwa pamoja?

Pengine nitaonekana ninazungukazunguka tu bila kutoa jibu linaloeleweka; lakini tuseme kweli; hivi Tanganyika haiwezi kuathirika kukiwepo na jirani Zanzibar ambaye yeye maslahi yake ni kinyume na yale ya Tanganyika?

Acha nikomee hapa kwa sasa.
 
Leo hii tuna rais Mzanzibari anawaamulia Watanganyika mambo mengine ambayo wala siyo ya Muungano. Sasa hii inakuwaje?
Hakuna Mtanganyika mwenye power ya kuwaamulia Wazanzibari mambo yao ya ndani yasiyo ya muungano!

Mwinyi asili yake Mkuranga. Kaletwa atawale Wazanzibari lakini bado mnapiga kelele. Hakuna muungano kuna uvamizi, na hakuna nchi inayoitwa Tanganyika. Ni nchi bandia iliyokuwepo enzi za Waingereza. Leo haipo.
 
Tatizo tumeungana wakati tuna njaa, watu hufanya muungano wakishashiba. Ndio story kama hizi huibuka, umemkuta mzanzibari mmoja Dar unaanza mbona wapo huku. Umeenda Zanzibar maeneo kama Kiwengwa, Nugwi au hata pale Darajani ?
 
Kuna makundi mangapi hilo ni tatizo lao, kwa Mtanganyika wa Kigoma au Tukuyu au Tarime haathiriki
Kwa Mujibu wa Jenerali Ulimwengu anadai wakati wa mijadala yao G55 na Mwalimu pale Msasani, Mwalimu aliwahi kumuuliza Mateo Qares kuwa "Wewe una ukaribu zaidi na Wazaramo na wandengereko kuliko wao walivyo karibu na Wazanzibari?"

Ukiiangalia Tanganyika ya Tukuyu, Tarime au Kigoma na kusahau kuwa Tanga, Dar es salaam au Mtwara nako ni Tanganyika. Utakosea.
 
Zanzibar inachangia asilimia ngapi kwenye fuko la Tanzania?
Hili lisiwe swali gumu kulijibu.

Mzanzibari anapoamua kuishi na kufanya shughuli zake sehemu yoyote ya Tanganyika, huyu tayari anachangia kwenye pato.

Kwa hiyo, kama tukiondoa haya ya wanasiasa kubagua watu kwa misingi ya wanakotokea (i.e., mTanganyika asiweze kujishughulisha Zanzibar, kwa mfano), hili swala siyo swala la muhimu sana.

Ila pengine umuhimu wake utaongezeka, wakati Zanzibar akigundua na kuchimba gesi/mafuta, halafu pato hilo lihodhiwe huko huko Zanzibar, lakini gesi ya Mtwara ikiuzwa ilete faida kote Zanzibar na Tanganyika, hapo swali litakuwa na uzito wake.
 
Kapimwe akili, hauko sawa hata kidogo!! Labda nikuhoji swali dogo: hivi Watanganyika wakihamua kuwatimua Waunguja wote na Wapemba wanao ishi bara na kumiliki mashamba,aridhi ,majengo na viwanda nk, niambie mtakuwa wageni wa nani??

FYI, you people needs us more than we do - don't you forget that, mnatutegemea kwa mambo mengi tu, msione mambo mengi tunamezea mkafikiri sisi ni KUBWA JINGA far from it, I trust this serves you right next time utafikiria mara mbili mbili kabla huja-comment chochote kuhusu masuala ya Muungano. CHEERS.

Zanzibar kuna majeshi ya uvamizi yaliyoletwa na Nyerere na mpaka leo yamebaki kumwaga damu za Wazanzibari. Hayo ndiyo yaondoke na Zanzibar ipate mamlaka kamili. Huko bara kumejaa Wachina, Wakenya, Warundi, na watu wengine kibao. Wewe kama una uhasama na Wazanzibari wafukuze usilete visingizio vya Wazanzibari kukataa kutawaliwa kama nchi ya kikoloni ndiyo sababu.
 
Kwa Mujibu wa Jenerali Ulimwengu anadai wakati wa mijadala yao G55 na Mwalimu pale Msasani, Mwalimu aliwahi kumuuliza Mateo Qares kuwa "Wewe una ukaribu zaidi na Wazaramo na wandengereko kuliko wao walivyo karibu na Wazanzibari?"

Ukiiangalia Tanganyika ya Tukuyu, Tarime au Kigoma na kusahau kuwa Tanga, Dar es salaam au Mtwara nako ni Tanganyika. Utakosea.
Ninaposema Kigoma, Tukuyu au Tarime nina maana moja kwamba ile impact ya muungano kwa watu hao ipo wapi? Kiuhalisia nini unadhani watakosa nje ya muungano? Hawategemei chochote kutoka Zanzibar

Mwaka 1961 hadi 1963 zilikuwa nchi mbili, laiti tusingeungana tungebaki kama tulivyo na Burundi au Rwanda ambao tulikuwa wamoja wakati wa Ujerumani.

Lakini pia kuna ukweli, mtu wa Tarime anaweza kuishi Tukuyu. Mtarime huyo ni mgeni Zanzibar!
Mtu wa Kigoma anapata makazi Tanga, lakini Mkigoma huyo huyo hana nafasi Pemba.
 
Kapimwe akili, hauko sawa hata kidogo!! Labda nikuhoji swali dogo: hivi Watanganyika wakihamua kuwatimua Waunguja wote na Wapemba wanao ishi bara na kumiliki mashamba,aridhi ,majengo na viwanda nk, niambie mtakuwa wageni wa nani??
Idi Amini aliwaza hivyo alipoamua kuwafukuza wahindi, matokeo yake.....
 
Wazazibari kupata haki zote za utanganyika ni njia rahisi ya kuelekea muungano wa serikali moja.
Baada ya muda kidogo wazazibari wengi watakuwa bara kwa ardhi, mali na biashara kuliko watakaokuwa visiwani. Hapo ndipo uwanja utawekwa sawa, wakiomba wenyewe.
 
Hili lisiwe swali gumu kulijibu.

Mzanzibari anapoamua kuishi na kufanya shughuli zake sehemu yoyote ya Tanganyika, huyu tayari anachangia kwenye pato.

Kwa hiyo, kama tukiondoa haya ya wanasiasa kubagua watu kwa misingi ya wanakotokea (i.e., mTanganyika asiweze kujishughulisha Zanzibar, kwa mfano), hili swala siyo swala la muhimu sana.

Ila pengine umuhimu wake utaongezeka, wakati Zanzibar akigundua na kuchimba gesi/mafuta, halafu pato hilo lihodhiwe huko huko Zanzibar, lakini gesi ya Mtwara ikiuzwa ilete faida kote Zanzibar na Tanganyika, hapo swali litakuwa na uzito wake.
Hapana swali ni hili, SMZ inachangia nini? Hatuzungumzii mtu binafsi.

Ikitokea suala la kugawana Wazanzibar wanataka usawa, je, wao wanachangia nini?

Kumbuka muungano hauendeshwi kama jahazi la upepo.
 
Back
Top Bottom