Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
Uzi una mantiki sana nashangaa hujibu hoja umeingiza mambo yasiyokuwepoUzi wa kibaguzi na uliokosa mashiko. Kama mzanzibar kaoa au kaolewa huku bara huyo mtoto anayezaliwa abaguliwe kwa sababu ya wazazi wake?.
Mada nyepesi inayokwenda kinyume na tamaduni za kitanzania inaweza kuvunja mshikamano wetu badala ya kuufanya ukawa imara.
1. Mtoto anayezaliwa na wazazi wa pande mbili ni Mtanzania. Tatizo linakuja kwamba Mtanzania ni Mtu wa bara halafu kuna Mzanzibar. Mtoto huyo anabaguliwa na Wazanzibar kwasababu ya huo Uzanzibar.
2. Hoja ya Allen Kilewella : yapo mambo Wazanzibar wanalamika si ya muungano.
21% ajira zilizotengwa kwa Wazanzibar ni pamoja na mambo yasiyo ya muungano, je hiyo ni kuwatendea haki Watanganyika ambao hawana fursa hiyo Zanzibar?
Hivyo unatakiwa kujibu hoja za mleta mada si kugundua hoja nje ya mada.
Kwa lugha rahisi Wazanzibar wanalaani kuongezwa kwa mambo ya muungano kama elimu ya juu, lakini wapo bodi ya mkiopo ya elimu ya juu na wanapewa kutoka HESLB. Je Mtanganyika anapewa ZHESLB?
Hapa ni kwamba Wazanzibar wanasema '' Nguruwe ni haramu lakini mchuzi wake ni halali''
Tunakuuliza wewe, je hiyo ni sawa?