Ni halali Wazanzibari kufanya kazi za Watanganyika?

Ukweli huu hapa


Your browser is not able to display this video.
 
Athari kubwa ambayo Tanganyika itapata baada ya kuvunjika kwa muungano ni kupokea wakimbizi kutoka Zanzibar.
 
Ukweli ni kwamba Tanganyika ndio inayojipendekeza kwa zanzibar, uhusiano wao unafanana na uhusiano wa mtu mke na mtu mume kwa kile kinachoitwa "Muungano"

Anachofaidi Tanganyika katika hili ni "ego na pride" tu ambazo practically hazina value yeyote. wakati anachofaidi zanzibari ni kupendwa, kubembelezwa , kuhudumiwa kitu ambacho practically kina value sababu inayotumika ni resources ya mtanganyika.

Mtanganyika ndiye anayepaswa kuukataa muungano kwa nguvu kubwa sana ama kudai haki na wajibu katika huo muungano ili kuondoa unyonyaji ama sivyo tugawane mbao. Kila mtu aende kwa mwenzake kama mgeni kwa faida ya kizazi kijacho cha Tanganyika.
 
HIV

Ulishawahi kujiuliza kwanini Tanganyika hawataki kuiachia Zanzibar???
 
Hivi Ulishawahi kujiuliza kwanini Tanganyika hawataki kuiachia Zanzibar???
Tanganyika haitaki kuiachia Zanzibar? Kwani Zanzibar wanakatazwa au kuzuiwa kutoka kwenye Muungano? Sasa Rais ni Mzanzibari na Rais wa Zanzibar ni Mzanzibari, si wakae waamue kujitoa!!?
 
Percentage kubwa ya Raia wa nchi husika kuwa waislamu sio kigezo cha kuifanya nchi hiyo kutawaliwa kiislamu !! Nchi nyingi huko Arabuni asilimia kubwa za wananchi wao ni waislamu lakini haziendeshwi kiislamu kama ulivyotolea mfano Afghanistan !! Kweli kusoma sana sio kuelimika !! Je Zanzibar kabla ya muungano ilikuwa ni nchi inayotawaliwa kiislamu kama Afghanistan ??!!
 
Wewe nawe, umesoma na kuelewa nilichoandika??
 
Kweli kabisa !
 
Unaota wewe yaani kula yako wewe unadhani inabadilisha nini?
Huyo bichwa nundu JPM,rest in hell,aliyewaweka wakina kwanaFA na Babu tale na kushinda majimbo yote ya bara alikua mzanzibar?
Hao uliowataja ni wazanzibari au ni wa bara? Kwani waligombea Zanzibar?
 
Hapana swali ni hili, SMZ inachangia nini? Hatuzungumzii mtu binafsi.

Ikitokea suala la kugawana Wazanzibar wanataka usawa, je, wao wanachangia nini?

Kumbuka muungano hauendeshwi kama jahazi la upepo.
Mkuu 'Nguruvi3', jibu hili nililisoma kitambo jana, nikaona niliweke pembeni kwanza.

Sasa nimerudi na kusisitiza kwamba hatuwezi kamwe kutozungumzia "mtu binafsi" katika mchango wa pato la nchi.
Huu pia unaweza kuwa mjadala maalum kuonyesha umuhimu wa Muungano wetu huu.

Swala la Zanzibar kudai kugawana kwa "usawa" (kwa uwiano) nina hakika hilo pia ni swala la kitaalam tu linaloweza kutatuliwa kirahisi. Tatizo ninaloliona ni hawa viongozi wanaoonekana kama wanatoa HONGO/RUSHWA, kila mara panapotokea kelele toka kwa kundi lisilotaka Muungano. Hili ndilo tatizo.
 
Huu muungano Mimi unanishinda, yaani,ni haramu mtanganyika kununua ardhi Zanzibar,ika ni halali mzanzibari kununua ardhi Tanganyika,alafu wanachukya ajira zetu huku.
 
Wazanzibar wanaoishi Bara wanatumia huduma za jamii kama afya, elimu n.k. kama Mtanganyika
Kwa wanaofanya shughuli na kulipa kodi si fadhila ni wajibu, wanatumia huduma za nchi

Kumbuka Tanganyika inatoa fungu kupeleka Zanzibar (21%) kama sehemu ya PAYE ya wafanyakazi wa muungano. Tanganyika inawalipa wafanyakazi kwa kodi za Watanganyika.

Kugawana: Hapa kuna tatizo la elimu wala si muungano. Zanzibar wanasema tuliungana kama nchi huru tunapaswa kugawana sawa. Hoja hiyo ina mantiki. HAKI inaambatana na WAJIBU. Ikiwa kuna kugawana, kuchangia kupo wapi?

Gavana wa BoT anasema Zanzibar haijachangia kwa miaka 40. Unagawana vipi kwa usawa mali za mtu mwingine? elimu!

Ikiwa kuna kugawana kama ilivyo 21% ya ajira, Zanzibar wapewe wizara moja tu ya muungano waendeshe
Tatu, mikopo inayopitia JMT, Zanzibar waonyeshe wapi wanalipa! na kwa mgao gani!

Ikiwa misaada itagawanywa sawa, vipi kuhusu 4.5% ya pato la Tanganyika inayokwenda Zanzibar?
Yaani madini, gesi ya Mtwara, kodi n.k. zinazokusanywa na TRA kwa mwezi, 4.5% inakwenda Zanzibar

TRA Bara wanakusanya Takribani trilioni moja kwa mwezi, piga hesabu, angalia SMZ inakusanya kiasi gani
 
Mkuu 'Nguruvi3', sina pumzi!

Kuna msemo maarufu ulioasisiwa toka huko huko Zanzibar (kila mara ningependa nieleweke kwamba ninaposema Zanzibar, sina maana ya kuhusisha waTanzania wote waishio huko, bali kundi linalopigana kufa na kupona kuuvunja Muungano).

Msemo wenyewe ni huu : "KERO ZA MUUNGANO," na matokeo yake yakasababisha kuwepo na (Kamati)? inayoshughulika na maswala ya hizo kero.

Mara zote imekuwa ni maswala yaihusuyo Zanzibar tu ndiyo yanayoshughulikiwa huko, sijawahi kusikia kero zinazoihusu Tanganyika zikitafutiwa ufumbuzi wake huko; na wala sijui taratibu zinazotakiwa kufuatwa ili kuwasilisha kero hizo zijadiliwe.

Bila shaka sasa ni wakati wa kushughulikia kero zinazoihusu Tanganyika zinazosababishwa na Muungano.

Lakini inawezekana pia ikadaiwa kwamba hiyo siyo njia sahihi ya kuondoa matatizo. Njia iliyo sahihi ni kutengeneza Katiba Mpya inayofafanua vizuri haya maswala ya Muungano.
Kwa kutumia njia hii, wananchi wenyewe ndio watakaokuwa wameamua hatma ya Muungano wao.
 
Athari kubwa ambayo Tanganyika itapata baada ya kuvunjika kwa muungano ni kupokea wakimbizi kutoka Zanzibar.
Mbona hata sasa tunao wananchi wengi (waTanzania) kutoka huko, una maana Tanganyika anaathirika kwa sababu ya watu hao kuwepo hapa?

Na kama hivyo ndivyo itakavyokuwa, kwa nini hao hao wakimbizi watarajiwa wasipewe uwezo wa kuzuia wasiwe wakimbizi wakati huu?
Na badala yake, hao wanaopanga kuwafanya wenzao kuwa wakimbizi, wao ndio wawe wakimbizi (sijui wakielekea nchi gani)?
 
Chamuhimu serikali ziwe tatu mengi yatajijibu huko lkn katiba hii ya serikali 2 nivurugu tuu hamna anayeelewa nini chakufanya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…