Ni halali Wazanzibari kufanya kazi za Watanganyika?

Ni halali Wazanzibari kufanya kazi za Watanganyika?

Ukweli huu hapa

Naomba radhi kwa kutoelewa swali nilipojibu mara ya kwanza, kuhusu "athari zinazotokana na muungano kuvunjika."

Hata ukiwauliza Zanzibar, wao pia watakwambia hawataathirika kutokana na muungano kuvunjika (hasa wale wanaopiga kelele kila siku kulaumu waasisi wa muungano na kutaka muungano usiwepo0.

Hawa wanaamini, muungano ukivunjika tu, neema inaiangukia Zanzibar wanayoiona kama kuwa na muungano ndiko kunakozuia neema hizo; kuwa kama Singapore!

Kwa Tanganyika, pamoja na kujiona kuwa inautua mzigo mzito unaoielemea; ikiwa na pamoja na maudhi mengi ya kelele, kuvunjika kwa muungano pia itakuwa ni athari kwetu hata kama siyo athari iliyo wazi (tangible). 'Prestige' ya nchi pamoja na kuwa ni kama 'jambo tu la kuamini (abstract), lakini lina umuhimu wake. Kwa hiyo siyo jambo la kubeza.

Nadhani katika kujibu swali kama hili, inabidi pia kuuliza swali jingine: Hivi kuna sababu zipi ambazo hufanya nchi zipende kuwa na muungano? Tusitazame tu udogo wa Zanzibar na ukubwa wa Tanganyika katika kujibu swali kama hili.
Hivi katika raia wetu Tanzania, kuna tofauti zipi ambazo zinatufanya tuonekane kuwa watu wa mataifa mawili kuliko kuwa taifa moja? Tofauti zetu ni zipi zinazotufanya sisi tuwe upande mmoja na wao wawe upande mwingine kama nchi tofauti?

Tukiondoa haya yanayochochewa na wanasiasa kutufanya tuonekane tofauti, kweli mZanzibari anayo tofauti kubwa na mTanganyika kiasi kwamba hawawezi kuwa pamoja?

Pengine nitaonekana ninazungukazunguka tu bila kutoa jibu linaloeleweka; lakini tuseme kweli; hivi Tanganyika haiwezi kuathirika kukiwepo na jirani Zanzibar ambaye yeye maslahi yake ni kinyume na yale ya Tanganyika?

Acha nikomee hapa kwa sasa.
Athari kubwa ambayo Tanganyika itapata baada ya kuvunjika kwa muungano ni kupokea wakimbizi kutoka Zanzibar.
 
Ukweli ni kwamba Tanganyika ndio inayojipendekeza kwa zanzibar, uhusiano wao unafanana na uhusiano wa mtu mke na mtu mume kwa kile kinachoitwa "Muungano"

Anachofaidi Tanganyika katika hili ni "ego na pride" tu ambazo practically hazina value yeyote. wakati anachofaidi zanzibari ni kupendwa, kubembelezwa , kuhudumiwa kitu ambacho practically kina value sababu inayotumika ni resources ya mtanganyika.

Mtanganyika ndiye anayepaswa kuukataa muungano kwa nguvu kubwa sana ama kudai haki na wajibu katika huo muungano ili kuondoa unyonyaji ama sivyo tugawane mbao. Kila mtu aende kwa mwenzake kama mgeni kwa faida ya kizazi kijacho cha Tanganyika.
 
HIV
Kuna mambo yanafanyika kwa upendeleo tu hayana mantiki.

Hakuna sababu za kujenga ikulu hizo ambazo basically zinahudumiwa na kodi za Watanganyika. Wazanzibar hawana mchango wowote kwahiyo hili ni kuongeza mzigo kwa mlipa kodi. Ndio Tozo mnazolundikiwa kuhudumia vitu visivyo na maana kama hivi

Majuzi Rais anasema Zanzibar iwe special zone ya police kwasababu ya nature yake.
Hivi Zanzibar inapakana na nchi ngapi?
Tanganyika inapakana na nchi 8 inahitaji resources zaidi si Zanzibar . Kwanini special zone Zanzibar na siyo Mtwara ?

Haya yanatokea kwasababu hakuna mtu anayesimamia masilahi ya Tanganyika.

Matokeo yake Philip Mpango anakaa kwa siri na Wazanzibar wanamaliza kero kwa siri kukiwa na pande moja tu.
Watanganyika hawajui MpAngo kakubaliana nini na Wazanzibar na ni Watanganyika wanaoubeba muungano 100%. Kwenye vikao hawapo, wapo Wazanzibar

Ipo siku tutamuuliza Philip Mpango na hili akae akijua litahitimisha ndoto yake. Tutamuuliza kwanini 'alisailiti' Tanganyika kwa nini.

G55 waliona mambo kama haya! siku hizi kule mjengo wamelala wakiamka wanaimba na kusif

G55 waliona mambo kama haya! siku hizi kule mjengo wamelala wakiamka wanaimba na kusifu
Ulishawahi kujiuliza kwanini Tanganyika hawataki kuiachia Zanzibar???
 
Hivi Ulishawahi kujiuliza kwanini Tanganyika hawataki kuiachia Zanzibar???
Tanganyika haitaki kuiachia Zanzibar? Kwani Zanzibar wanakatazwa au kuzuiwa kutoka kwenye Muungano? Sasa Rais ni Mzanzibari na Rais wa Zanzibar ni Mzanzibari, si wakae waamue kujitoa!!?
 
Kwanza nitangulie kwa hoja yako ya mwisho kwamba ni wazanzibari ndiyo wanatakiwa waulizwe kama wanautaka Muungao ama la. Kwa mujibu wa Mwalimu (na ndiyo mtizamo wangu pia) kwenye kitabu chake cha "Uongozi wetu na hatima ya Tanzania" alishangaa ni kwa nini viongozi wa CCM wanashindwaje kuwauliza Wazanzibari swali rahisi kama hilo.

Lakini pia Mwalimu aliamini wazanzibar wakiulizwa na wakipewa uhuru wa kulijibu swali hilo, ni LAZIMA watakataa kuuvunja Muungano. Miaka 29 baadaye bado CCM haiwezi kuwauliza Wazanzibari kama wanautaka Muungano au la!! Leo kina Njelu Kasaka, Jenerali Ulimwengu na wenzao, nadhani wanajuta ni kwa nini hawakuendelea na hoja yao ya kuidai Tanganyika ndani ya Muungano wakati ule.

Athari zitakazotokana na kuvunjika kwa Muungano zina sababu mtambuka. Leo ukiangalia kwa makini andiko la Abdulrahaman Kinana kwenye Jarida la "The Hill" la nchini Marekani, iliyokuja kutiwa utambi na William Lukuvi wakati wa Uchaguzi wa 2015 kuhusu Uislam na Ugaidi Zanzibar, ingawa ilikuwa hoja ya kipropaganda, lakini Muungano ukivunjika italeta athari.

Athari itakayojitokeza ni kwamba ndani na nje ya Zanzibari kuna watu wanaamini kwamba ili Zanzibar "iwe salama" ni lazima iongozwe kwa kufuata misingi ya Kiislam. Na hata zile kauli za kutunza historia na utamaduni wa Zanzibar Mara nyingi hulenga kuonesha kwamba mambo ya dini ya Kiislam ndiyo utamaduni na HIstoria ya Zanzibar.

Tatizo litaanzia pale wapo wale wanaoamini Zanzibar inatakiwa kutawaliwa kwa kufuata misingi ya dini ya Kiislam kama inavyotawaliwa Afghanistan, lakini wapo pia wale watakaotaka itawaliwe kama Oman ama Qatar. Kama makundi haya yakihasimiana yakiwa yenyewe tu, bila ya shaka athari zake lazima zitafika Tanganyika.

Lakini kuna swali la wale Wazanzibari waliozaliwa Tanganyika na kuzaliana na kuzaliana, lakini wakiwa bado wanataka kutunza utambulisho (Identity) wao lakini wakiwa hawataki kurudi Zanzibari lakini kwa wakati huo kuna shinikizo toka kwa watanganyika kwamba Wazanzibari wote warudi kwao.

Kwenye hizo harakati za kila mtu "arudi kwao" kunatokea makundi makubwa matatu. Wapo watakaotaka warudi wakiwa mikono mitupu na kuacha kila kitu huku Tanganyika, wapo watakaruhusu waondoke na vitu vyao na wapo ambao wao waondoke na vitu vyao au waviache si jambo la msingi bali kuondoka kwao ndiyo watakachokitaka.
Percentage kubwa ya Raia wa nchi husika kuwa waislamu sio kigezo cha kuifanya nchi hiyo kutawaliwa kiislamu !! Nchi nyingi huko Arabuni asilimia kubwa za wananchi wao ni waislamu lakini haziendeshwi kiislamu kama ulivyotolea mfano Afghanistan !! Kweli kusoma sana sio kuelimika !! Je Zanzibar kabla ya muungano ilikuwa ni nchi inayotawaliwa kiislamu kama Afghanistan ??!!
 
Wewe nawe, umesoma na kuelewa nilichoandika??
 
Kwa Mujibu wa Jenerali Ulimwengu anadai wakati wa mijadala yao G55 na Mwalimu pale Msasani, Mwalimu aliwahi kumuuliza Mateo Qares kuwa "Wewe una ukaribu zaidi na Wazaramo na wandengereko kuliko wao walivyo karibu na Wazanzibari?"

Ukiiangalia Tanganyika ya Tukuyu, Tarime au Kigoma na kusahau kuwa Tanga, Dar es salaam au Mtwara nako ni Tanganyika. Utakosea.
Kweli kabisa !
 
Unaota wewe yaani kula yako wewe unadhani inabadilisha nini?
Huyo bichwa nundu JPM,rest in hell,aliyewaweka wakina kwanaFA na Babu tale na kushinda majimbo yote ya bara alikua mzanzibar?
Hao uliowataja ni wazanzibari au ni wa bara? Kwani waligombea Zanzibar?
 
Hapana swali ni hili, SMZ inachangia nini? Hatuzungumzii mtu binafsi.

Ikitokea suala la kugawana Wazanzibar wanataka usawa, je, wao wanachangia nini?

Kumbuka muungano hauendeshwi kama jahazi la upepo.
Mkuu 'Nguruvi3', jibu hili nililisoma kitambo jana, nikaona niliweke pembeni kwanza.

Sasa nimerudi na kusisitiza kwamba hatuwezi kamwe kutozungumzia "mtu binafsi" katika mchango wa pato la nchi.
Huu pia unaweza kuwa mjadala maalum kuonyesha umuhimu wa Muungano wetu huu.

Swala la Zanzibar kudai kugawana kwa "usawa" (kwa uwiano) nina hakika hilo pia ni swala la kitaalam tu linaloweza kutatuliwa kirahisi. Tatizo ninaloliona ni hawa viongozi wanaoonekana kama wanatoa HONGO/RUSHWA, kila mara panapotokea kelele toka kwa kundi lisilotaka Muungano. Hili ndilo tatizo.
 
Huu muungano Mimi unanishinda, yaani,ni haramu mtanganyika kununua ardhi Zanzibar,ika ni halali mzanzibari kununua ardhi Tanganyika,alafu wanachukya ajira zetu huku.
 
Mkuu 'Nguruvi3', jibu hili nililisoma kitambo jana, nikaona niliweke pembeni kwanza.

Sasa nimerudi na kusisitiza kwamba hatuwezi kamwe kutozungumzia "mtu binafsi" katika mchango wa pato la nchi.
Huu pia unaweza kuwa mjadala maalum kuonyesha umuhimu wa Muungano wetu huu.

Swala la Zanzibar kudai kugawana kwa "usawa" (kwa uwiano) nina hakika hilo pia ni swala la kitaalam tu linaloweza kutatuliwa kirahisi. Tatizo ninaloliona ni hawa viongozi wanaoonekana kama wanatoa HONGO/RUSHWA, kila mara panapotokea kelele toka kwa kundi lisilotaka Muungano. Hili ndilo tatizo.
Wazanzibar wanaoishi Bara wanatumia huduma za jamii kama afya, elimu n.k. kama Mtanganyika
Kwa wanaofanya shughuli na kulipa kodi si fadhila ni wajibu, wanatumia huduma za nchi

Kumbuka Tanganyika inatoa fungu kupeleka Zanzibar (21%) kama sehemu ya PAYE ya wafanyakazi wa muungano. Tanganyika inawalipa wafanyakazi kwa kodi za Watanganyika.

Kugawana: Hapa kuna tatizo la elimu wala si muungano. Zanzibar wanasema tuliungana kama nchi huru tunapaswa kugawana sawa. Hoja hiyo ina mantiki. HAKI inaambatana na WAJIBU. Ikiwa kuna kugawana, kuchangia kupo wapi?

Gavana wa BoT anasema Zanzibar haijachangia kwa miaka 40. Unagawana vipi kwa usawa mali za mtu mwingine? elimu!

Ikiwa kuna kugawana kama ilivyo 21% ya ajira, Zanzibar wapewe wizara moja tu ya muungano waendeshe
Tatu, mikopo inayopitia JMT, Zanzibar waonyeshe wapi wanalipa! na kwa mgao gani!

Ikiwa misaada itagawanywa sawa, vipi kuhusu 4.5% ya pato la Tanganyika inayokwenda Zanzibar?
Yaani madini, gesi ya Mtwara, kodi n.k. zinazokusanywa na TRA kwa mwezi, 4.5% inakwenda Zanzibar

TRA Bara wanakusanya Takribani trilioni moja kwa mwezi, piga hesabu, angalia SMZ inakusanya kiasi gani
 
Wazanzibar wanaoishi Bara wanatumia huduma za jamii kama afya, elimu n.k. kama Mtanganyika
Kwa wanaofanya shughuli na kulipa kodi si fadhila ni wajibu, wanatumia huduma za nchi

Kumbuka Tanganyika inatoa fungu kupeleka Zanzibar (21%) kama sehemu ya PAYE ya wafanyakazi wa muungano. Tanganyika inawalipa wafanyakazi kwa kodi za Watanganyika. Kwamba, wanapewa nafasi za upendeleo kwenye maeneo yasiyo ya muungano halafu SMZ inalipwa kwa kusaidiwa kupunguza ukosefu wa ajira!!

Kugawana: Hapa kuna tatizo la elimu wala si muungano. Zanzibar wanasema tuliungana kama nchi huru tunapaswa kugawana sawa. Hoja hiyo ina mantiki, lakini panapokuwa na uhaba wa elimu ni kwamba , HAKI inaambatana na WAJIBU. Ikiwa kuna kugawana, kuchangia kupo wapi?

BoT kupitia gavana wanasema Zanzibar haijachangia kwa miaka takribani 40. Unagawana vipi kwa usawa mali za mtu mwingine? elimu!

Pili, Ikiwa kuna kugawana kama ilivyo 21% ya ajira, Zanzibar wapewe wizara moja tu ya muungano waendeshe

Tatu, mikopo inayopitia JMT, Zanzibar waonyeshe wapi wanalipa! na kwa mgao gani!

Nne, wanasema misaada igawanywe sawa. Ni hoja ya ukosefu wa elimu, ni ya kipuuzi kama ile ya TV za rangi.

Ikiwa misaada itagawanywa sawa sawa, vipi kuhusu 4.5% ya pato la Tanganyika inayokwenda Zanzibar?
Yaani madini, gesi ya Mtwara, kodi n.k. zinazokusanywa na TRA kwa mwezi, 4.5% inakwenda Zanzibar

TRA Bara wanakusanya Takribani trilioni moja kwa mwezi, piga hesabu halafu angalia SMZ inakusanya kiasi gani
Mkuu 'Nguruvi3', sina pumzi!

Kuna msemo maarufu ulioasisiwa toka huko huko Zanzibar (kila mara ningependa nieleweke kwamba ninaposema Zanzibar, sina maana ya kuhusisha waTanzania wote waishio huko, bali kundi linalopigana kufa na kupona kuuvunja Muungano).

Msemo wenyewe ni huu : "KERO ZA MUUNGANO," na matokeo yake yakasababisha kuwepo na (Kamati)? inayoshughulika na maswala ya hizo kero.

Mara zote imekuwa ni maswala yaihusuyo Zanzibar tu ndiyo yanayoshughulikiwa huko, sijawahi kusikia kero zinazoihusu Tanganyika zikitafutiwa ufumbuzi wake huko; na wala sijui taratibu zinazotakiwa kufuatwa ili kuwasilisha kero hizo zijadiliwe.

Bila shaka sasa ni wakati wa kushughulikia kero zinazoihusu Tanganyika zinazosababishwa na Muungano.

Lakini inawezekana pia ikadaiwa kwamba hiyo siyo njia sahihi ya kuondoa matatizo. Njia iliyo sahihi ni kutengeneza Katiba Mpya inayofafanua vizuri haya maswala ya Muungano.
Kwa kutumia njia hii, wananchi wenyewe ndio watakaokuwa wameamua hatma ya Muungano wao.
 
Athari kubwa ambayo Tanganyika itapata baada ya kuvunjika kwa muungano ni kupokea wakimbizi kutoka Zanzibar.
Mbona hata sasa tunao wananchi wengi (waTanzania) kutoka huko, una maana Tanganyika anaathirika kwa sababu ya watu hao kuwepo hapa?

Na kama hivyo ndivyo itakavyokuwa, kwa nini hao hao wakimbizi watarajiwa wasipewe uwezo wa kuzuia wasiwe wakimbizi wakati huu?
Na badala yake, hao wanaopanga kuwafanya wenzao kuwa wakimbizi, wao ndio wawe wakimbizi (sijui wakielekea nchi gani)?
 
Chamuhimu serikali ziwe tatu mengi yatajijibu huko lkn katiba hii ya serikali 2 nivurugu tuu hamna anayeelewa nini chakufanya
 
Back
Top Bottom