Ni halali Wazanzibari kufanya kazi za Watanganyika?

Sijui kama ni Binti, au ni jina tu analotumia mkuu "Zawadia."

Mimi ningependa kumsaidia hivi.

Samia kama kiongozi mkuu wa nchi, anayo nafasi nzuri sana ya kuitisha referendum juu ya Muungano. Ushiriki uwe wa pande zote mbili; na ili isionekane kuwa waTanganyika kwa wingi wao watatumia wingi huo kuwaburuza waZanzibari, basi iwekwe sheria (kama haipo), itakayosema kwamba pande zote mbili za Muungano zikikubali Muungano uendelee ni lazima wapiga kura wawe theluthi mbili za kura.
Referendum ikiamua Muungano uendelee, ni lazima haya mambo ya upande mmoja kujiona wao ni bora zaidi ya upande mwingine, na kutaka kujitambulisha kwa ubora wao huo yakome.

Niona vyo, sasa tumetoka kwenye kupiga kelele tu, ila tupo kwenye sehemu moja ya Muungano kuilalia sehemu nyingine. Hii haikubaliki hata kidogo.

Something is going to give pretty soon.
 
Kwa hiyo unakubaliana na wazo kwamba 'referendum' juu ya Muungano ni muhimu kwa sasa, na kwamba pande zote mbili zishiriki katika referendum hiyo?
Ndiyo na ndivyo ilivyo
 
Kwa maneno haya unakubali kwamba Wabara/Watanganyika nao wanateuliwa kushika nafasi Zanzibar kinyume na madai kwamba Wabara hawaajiriwi Zanzibar?

Wazanzibari hawatofanya hivyo na badala yake watatumia njia nyingine.

Sasa kama mumeshajua jinsi muungano huu unavyokupigeni ni muda muafaka kuachana nao na njia moja muafaka ni kupitia referandum. Tafadhalini tumieni fursa hiyo adhimu ili musipigwe tena.
 

Hiyo demokrasia ya kufanya referendum iko wapi? Kama uchaguzi tu unavurugwa sembuse hiyo referendum?


Your browser is not able to display this video.




Your browser is not able to display this video.
 
Tanzania ni matokeo ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Kama Zanzibar ipo ni kwa nini Tanganyika isiwepo.

Kwa nini kuwepo kwa Tanzania kuipoteze Tanganyika lakini Zanzibar iendelee kuwepo?
Hawawezi kukujibu hizi hoja za msingi hadi kesho.
 
Lakini si Samia ni Rais sasa, huu uoga unatoka wapi?

Unakumba aliyoandika Mkapa kwenye kitabu chake kwamba mauaji ya mwaka 2001 yalifanywa na wengine? Ina maana vyombo vya dola vikiamua vinafanya. Samia watamfungia ikulu wao wataenda kufanya uhuni.

 
Hii ndio hoja ya msingi ya serikali tatu, rais wa muungano na wa Zanzibar wote ni wazanzibari, nani anatetea maslahi ya Bara ndani ya Muungano? Bara inaporwa tu hakuna wa kuitetea, waliopigania Uhuru wa Tanganyika wanadhihakiwa mno
Kwenye genge la watafuna nchi ole wako uongelee maslahi ya wengi yenye tishio la ulaji wao.

Sent from my BBF100-6 using JamiiForums mobile app
 
Kwa Mfano , mimi wa kutoka Kajunjumele Kyela ninaweza kukubaliwa kugombea Ubunge Chake chake , Mchambawima au kisiwandui kama Husein Mwinyi alivyogombea Mkuranga ?
Ni ngumu mkuu,japo walikuwepo wanyakyusa kipindi cha nyuma akina Adam/David Mwakanjuki waliwahi kuukwa uwaziri na hata mama yao Elizabeth Mwakanjuki alizikwa huko na bado walibaguliwa ila Kwa sasa itakuwa ni ngumu zaidi kwa mbara kupewa nafasi huko.

Sent from my BBF100-6 using JamiiForums mobile app
 
Sasa hapa wewe unao uhakika gani kwamba siyo viongozi wa Zanzibar waliohusika na maamuzi ya kutumia vyombo hivyo kufanya mauaji?
 
Ni halali mkuu, si wanamchagua rais wa tanganyika,
 
Tanzania ni matokeo ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Kama Zanzibar ipo ni kwa nini Tanganyika isiwepo.

Kwa nini kuwepo kwa Tanzania kuipoteze Tanganyika lakini Zanzibar iendelee kuwepo?
Kamuulize Lukuvi
 
Lakini baada ya kukubaliana na wazo hilo, bado unadhani mtu sahihi wa kulianzisha na kusimamia zoezi hilo siyo Rais wa Jamhuri ya Muungano?
Ndiyo. Unaonekana kutaka rais atupiwe lawama ya kuukataa muungano kwa sababu ni Mzanzibari. Kama kuna watu wa kuanzisha hilo ni Wabara. Kama hawakufanya unataka kumtwika gunia la misumari Samia? Naombea hilo lisutokee kwake. Sasa kwa vile sasa Wabara mumeanza kuonja ladha ya kukosa haki, kama munavyoonesha, ni wakati sasa kwa wao kulianzisha. Siku zote usimtendee mtu lile ambalo wewe hupendi utendewe. Mpendelee mwenzio lile unalolipenda wewe.
 
Sasa hapa wewe unao uhakika gani kwamba siyo viongozi wa Zanzibar waliohusika na maamuzi ya kutumia vyombo hivyo kufanya mauaji?

Mkapa si ndiye alikuwa amiri jeshi mkuu wa majeshi yote? Kwa nini majeshi yatii amri za watu wengine za kuja kuuwa Wazanzibari? Samia hana nguvu ya kuuvunja huo muungano wakati chama chake CCM kinautaka na vyombo vya dola vinaulinda huo muungano.
 
Uliandika na nanukuu.
" Sina mfano, na sijui kama unao mfano wewe, mahsusi wa waZanzibari walioko CCM, waliokomalia jambo ambalo CCM ya waTanganyika............"

Nilikuwa najaribu kukupa huo mfano mahsusi ambao wewe huna na hujui kama uliem qoute anao mfano kama huo ili nyote wawili muwenao.

Kuhusu "irrelevance" ya mfano mahsusi nilioutoa itabidi urudishe post uliyoifuta au tuambie post uliyoifuta uliquote post # ngapi ili tuupate vizuri mtiririko wa mjadala.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…