Ni halali Wazanzibari kufanya kazi za Watanganyika?

Hatari Sana Sasa Wamejaa Sana, Vp Tanganyika Kule Mchambawima Tutapata Kazi
 
Hizi ni porojo na upindishaji kama ilivyokawaida ya watu kama wewe.
Ni kifungu kipi cha Katiba kinachozungumzia haya uliyoandika hapa?
Ukitaka kifungu utasoma mpaka macho yatapofuka hutaona hicho kifungu.
Ukiyataka hayo niliyoyaeleza nenda kwenye Jadweli.
 
Ndiyo. Unaonekana kutaka rais atupiwe lawama ya kuukataa muungano kwa sababu ni Mzanzibari. Kama kuna watu wa kuanzisha hilo ni Wabara. Kama hawakufanya unataka kumtwika gunia la misumari Samia? Naombea hilo lisutokee kwake. Sasa kwa vile sasa Wabara mumeanza kuonja ladha ya kukosa haki, kama munavyoonesha, ni wakati sasa kwa wao kulianzisha. Siku zote usimtendee mtu lile ambalo wewe hupendi utendewe. Mpendelee mwenzio lile unalolipenda wewe.
Hapa unakiri kwamba waTanganyika wanaporwa HAKI.

Anayesimamia kupora HAKI hiyo ni Samia, Rais wa Muungano

Wakati huo huo, unajifanya Samia atatupiwa lawama kama akisimamia zoezi la Referendum!
Maana yake ni kwamba huoni shida yoyote akitupiwa lawama ya kunyima HAKI. Mantiki iko wapi hapa?

Na zaidi ya yote, unaonyesha kwamba urais wa Samia unakasoro zinazotokana na uZanzibar wake!

Sasa rais wa aina hii ataleta manufaa gani kwa taifa analoliongoza?
 
Mkapa si ndiye alikuwa amiri jeshi mkuu wa majeshi yote? Kwa nini majeshi yatii amri za watu wengine za kuja kuuwa Wazanzibari? Samia hana nguvu ya kuuvunja huo muungano wakati chama chake CCM kinautaka na vyombo vya dola vinaulinda huo muungano.
Mbona unajichanganya mwenyewe.
Samia siyo Amiri Jeshi Mkuu wa vyombo vya dola kama alivyokuwa Mkapa? Kwa nini majeshi yatii amri za watu wengine katika kulinda au kuvunja muungano!
 
Hata mimi napenda iwe hivyo.

Sipendi Watanganyika wawaonee, wawadhulumu au wawadharau Wazanzibari na hivyo hivyo kwa Wazanzibari dhidi ya Watanganyika.
Ila wote waheshimiane kwa uTanzania wao, bila ya kujiona uTanganyika au uZanzibari kuwa bora zaidi.
 
Juzi shirika la POSTA limetangaza kutenga Asilimia 25 ya AJIRA zake Kwa wazanzibar labda ndio wakati watu wenyewe hawazidi Asilimia moja ya watanzania wote
Kwani Nani aliwaambia mtuvamie na kutuuwa kwa maelfu ?
 
Ila wote waheshimiane kwa uTanzania wao, bila ya kujiona uTanganyika au uZanzibari kuwa bora zaidi.
Watanzania bara sidhani kama wanajiona bora! si Watanzania!
Wazanzibar ndio wanaoona Uzanzibar ni BORA isipokuwa wakihitaji mafao ya Tanganyika , Tanzania ni muhimu

Katika ubora wa kizanzibar, kwanini wanakimbia referendum?
Fursa ipo Marais wote ni Wazanzibar, kipi kigumu hapo? Mbona kero zimetatuliwa haraka sana na SSH na VP Mpango?
 
Ndiyo. Unaonekana kutaka rais atupiwe lawama ya kuukataa muungano kwa sababu ni Mzanzibari. Kama kuna watu wa kuanzisha hilo ni Wabara. Kama hawakufanya unataka kumtwika gunia la misumari Samia? Naombea hilo lisutokee kwake. Sasa kwa vile sasa Wabara mumeanza kuonja ladha ya kukosa haki, kama munavyoonesha, ni wakati sasa kwa wao kulianzisha. Siku zote usimtendee mtu lile ambalo wewe hupendi utendewe. Mpendelee mwenzio lile unalolipenda wewe.
Kwanza, Wabara hawana lalamiko la kukosa HAKI. Wanachosema ni kuwa Wazanzibar wapewe haki zao

Kwa mfano, hakuna sababu ya kuongeza mambo ya muungano nje na yale ya 1964
Kwa mantiki hiyo Wazanzibar wasilamishwe kufanya kazi sehemu zisizo za muungano, na pia itasaidia vijana wa Tanganyika kunufaika na fursa zao kama zile za Zanzibar zinavyolindwa kwa Ubora wa Kizanzibar

Pili, matumizi ya rasilimali ni kuwabebesha mzigo. Hivi Ofisi ya Waziri mkuu Zanzibar inahusu nini?

Tatu, Rais SSH hawezi kulaumiwa kwa lolote, kinachofanyika ni referendum na kura zitaamua kama wanataka muungano au waondoke. Rais ana facilitate process, kura yake ni sawa na ya Mzanzibar mwingine, yaani ni 1 .

Watanzania Bara hawapaswi kufanya referendum kwasababu hawana lalamiko la muungano kama Wzbar

Tanzania bara wamewakubali ndiyo maana hakuna Mzanzibar anayebaguliwa bara kwa kitambulisho au lafudhi
Ndiyo maana Wazanzibar wanapewa nafasi za Ubunge kama kule Mkuranga, ajira popote ardhi n.k.

Kanuni za referendum ni zile zinazowahusu walalamikaji.
Mfano, Scotland walifanya referendum siyo UK. England, Wales na Ireland waliridhia kuwa chini ya Union Jack

Timor walifanya referendum kama walivyofanya Eritrea
Jimbo la Quebec Canada lilifanya referendum na siyo Canada yote

Puerto Rico, USA nao pia walifanya kama sitakuwa nimekosea

Hii ni fursa ambayo Marehemu Maalim alishawahi kuIzungumzia, kwamba iwepo Referendum

Leo Wazanzibar wanaogopa fursa iliyoletwa na Mwenyezi mungu! Nini kinawatisha?
 
Hapa unakiri kwamba waTanganyika wanaporwa HAKI.

Anayesimamia kupora HAKI hiyo ni Samia, Rais wa Muungano
Nimesema 'kwa maoni yenu'. Hapa sijaona nilipokiri.
Wakati huo huo, unajifanya Samia atatupiwa lawama kama akisimamia zoezi la Referendum!
Maana yake ni kwamba huoni shida yoyote akitupiwa lawama ya kunyima HAKI. Mantiki iko wapi hapa?
Mkuu hii ni tafsiri yako na maoni yako. Wacha yabakie kuwa yako usiyahusishe nami. Kwa lugha nyingine usinizushie uongo. Wacha yako yawe yako na yangu yabaki kuwa yangu.
zaidi ya yote, unaonyesha kwamba urais wa Samia unakasoro zinazotokana na uZanzibar wake!
Hapa unapiga ramli. Hemu jitahidi kusema ya kwako na yale yangu yaseme/yaandike kama nilivyoyaandika.

Ikitokea yamekushinda achana nayo. Wapo wanaoweza kujadili.
 
Kwa mfano, hakuna sababu ya kuongeza mambo ya muungano nje na yale ya 1964
Nakubaliana nawe. Sasa imekuwaje yameongezwa?
Hivi Ofisi ya Waziri mkuu Zanzibar inahusu nini?
Hayo ni maoni yako, una haki ya kutoa maoni. Maoni yangu ni kwamba Ofisi ya Waziri Mkuu Zanzibar ina maana kama ilivyo kwa Bara.
Watanzania Bara hawapaswi kufanya referendum kwasababu hawana lalamiko la muungano kama Wzbar
Mkuu ikiwa Wabara hawana lalamiko la Muungano wewe unsuelalamika ni Mzanzibari? Kama si Mzanzibari na si Mbara jee wewe ni Mkenya? Ikitokea hivyo hili halikuhusu wacha Watanzania tujadili
Mfano, Scotland walifanya referendum siyo UK. England, Wales na Ireland waliridhia kuwa chini ya Union Jack

Timor walifanya referendum kama walivyofanya Eritrea
Jimbo la Quebec Canada lilifanya referendum na siyo Canada yote

Puerto Rico, USA nao pia walifanya kama sitakuwa nimekosea
Hizi nchi ulizotaja ni sawa na Tanzania kama nchi; hivyo basi Wabara nawafanye.
 
Nakubaliana nawe. Sasa imekuwaje yameongezwa?
Mengine yaliongezwa kwa manufaa ya Wazanzibar. Elimu ya Juu si suala la muungano. Nyerere na akina Sitta walisema gharama za kusomesha ni kubwa Zanzibar itakuwa nyuma kielimu liongezwe.
Wazanzibar wote wamesoma bara kama Wabara . Leo hii HESLB inadhamini Wazanzibar wengi kuliko ZHESLB

Suala kama la michezo( Allen Kilewella ) , lengo llikuwa kuleta nguvu. Tazama wakati FAT ikiwa na Ligi ya pamoja jinsi Zanzibar soka lilivyokuwa. Baada ya kujitoa (na n haki) ile ligi au timu za Zanzibar nani anazungumzia tena!

Bandari , Zanzibar walipoondoa ili iwe huru hakuna aliyewazuia. Matokeo yake meli kubwa zinashusha Dar
Kuna Bandari kubwa Bara. Zanzibar walitakiwa waseme suala la Marine liwe Zanzibar. Kuleta ushindani na Bara ni tatizo kwao. Hivi Bagamoyo ikikamilika kuna meli itafika Zanzibar?
Hayo ni maoni yako, una haki ya kutoa maoni. Maoni yangu ni kwamba Ofisi ya Waziri Mkuu Zanzibar ina maana kama ilivyo kwa Bara.
Hapa ndipo Wazanzibar wanapokosea, hawajibu hoja kwa mantiki. Siku zote nimesisitiza kuwa muungano ni tatizo lakini kuna tatizo jingine kubwa...

Katiba ya Zanzibar ya 2010 haimtambui Waziri mkuu wa JMT
Waziri mkuu wa JMT hana mamlaka hata ya kuamuru Sheha. Leo inajengwa Ofisi yake , ya nini?
Ni kujenga tu ili watu wapate ajira, sawa! lakini anayebeba mzigo ni Mtanganyika anayelipia gharama za JMT
Mkuu ikiwa Wabara hawana lalamiko la Muungano wewe unsuelalamika ni Mzanzibari? Kama si Mzanzibari na si Mbara jee wewe ni Mkenya? Ikitokea hivyo hili halikuhusu wacha Watanzania tujadili
No ! tunasema hivi mambo yasiyo ya muungano yaondolewe. Ajira ziwe 21 ya mambo 7 tu ambayo Warioba ameyaanisha. Masuala ya ardhi kila upande uwe na sheria zake. Mchango wa kuendesha JMT utoke pande zote, yaani kuwe na HAKI na UWAJIBIKAJI isiwe suala la ' namimi, nataka, nipe, tugawane''.
Hivi unadai kugawana mali za mtu kwa usawa!
Hizi nchi ulizotaja ni sawa na Tanzania kama nchi; hivyo basi Wabara nawafanye.
Hapa huna hoja! sipendi uende kule kwa '' Zanzibar ndio nchi ya kwanza kwa TV za rangi''
Nadhani unapaswa kujibu hoja.
Referendum ya nchi gani zilioungana iliwahi kufanywa na nchi nzima?

UK: Scotland, Canada: Quebec. Kuna Puerto Rico, Eritrea na Timor. Tupe mfano mmoja tu wa hoja yako

Kama huna mfano unathibitisha kauli kwamba Wazanzibar ni Wanafiki. Si hawa walikuwa wafuasi wa Maalim?
Maalim alitaka referendum leo hawataki. Kesho wanalalamika tena fursa ikiondoka
Kwani shida ya referendum kwa Zanzibar ni ipi? Unafiki, wanaogopa kuondoka katika muungano! manafiki
 
Kalamu Allen Kilewella

Kwanini Wazanzibar wasiotaka muungano hataki Referendum itakayowapa fursa ya kuondoka?

Mengine yaliongezwa kwa manufaa ya Wazanzibar. Elimu ya Juu si suala la muungano. Nyerere na akina Sitta walisema gharama za kusomesha ni kubwa Zanzibar itakuwa nyuma kielimu liongezwe.
Wazanzibar wote wamesoma bara kama Wabara . Leo hii HESLB inadhamini Wazanzibar wengi kuliko ZHESLB

Suala kama la michezo , lengo llikuwa kuleta nguvu. Tazama wakati FAT ikiwa na Ligi ya pamoja jinsi Zanzibar soka lilivyokuwa. Baada ya kujitoa (na n haki) ile ligi au timu za Zanzibar nani anazungumzia tena!

Bandari , Zanzibar walipoondoa ili iwe huru hakuna aliyewazuia. Matokeo yake meli kubwa zinashusha Dar
Kuna Bandari kubwa Bara. Zanzibar walitakiwa waseme suala la Marine liwe Zanzibar. Kuleta ushindani na Bara ni tatizo kwao. Hivi Bagamoyo ikikamilika kuna meli itafika Zanzibar?

Hapa ndipo Wazanzibar wanapokosea, hawajibu hoja kwa mantiki. Siku zote nimesisitiza kuwa muungano ni tatizo lakini kuna tatizo jingine kubwa...

Katiba ya Zanzibar ya 2010 haimtambui Waziri mkuu wa JMT
Waziri mkuu wa JMT hana mamlaka hata ya kuamuru Sheha. Leo inajengwa Ofisi yake , ya nini?
Ni kujenga tu ili watu wapate ajira, sawa! lakini anayebeba mzigo ni Mtanganyika anayelipia gharama za JMT

No ! tunasema hivi mambo yasiyo ya muungano yaondolewe. Ajira ziwe 21 ya mambo 7 tu ambayo Warioba ameyaanisha. Masuala ya ardhi kila upande uwe na sheria zake. Mchango wa kuendesha JMT utoke pande zote, yaani kuwe na HAKI na UWAJIBIKAJI isiwe suala la ' namimi, nataka, nipe, tugawane''.
Hivi unadai kugawana mali za mtu kwa usawa!

Hapa huna hoja! sipendi uende kule kwa '' Zanzibar ndio nchi ya kwanza kwa TV za rangi''
Nadhani unapaswa kujibu hoja.
Referendum ya nchi gani zilioungana iliwahi kufanywa na nchi nzima?

UK: Scotland, Canada: Quebec. Kuna Puerto Rico, Eritrea na Timor. Tupe mfano mmoja tu wa hoja yako

Kama huna mfano unathibitisha kauli kwamba Wazanzibar ni Wanafiki. Si hawa walikuwa wafuasi wa Maalim?
Maalim alitaka referendum leo hawataki. Kesho wanalalamika tena fursa ikiondoka
Kwani shida ya referendum kwa Zanzibar ni ipi? Unafiki, wanaogopa kuondoka katika muungano! manafiki

Wewe umeshikilia referendum ikiwa wakati wa kuchagua viongozi wanaowataka kisheria , Jeshi la Tanganyika pamoja Na usalama wao wa Taifa huwafanyia unyamar huu

Hiyo referendum itafanyika vipi?

Kwanza, Wabara hawana lalamiko la kukosa HAKI. Wanachosema ni kuwa Wazanzibar wapewe haki zao

Kwa mfano, hakuna sababu ya kuongeza mambo ya muungano nje na yale ya 1964
Kwa mantiki hiyo Wazanzibar wasilamishwe kufanya kazi sehemu zisizo za muungano, na pia itasaidia vijana wa Tanganyika kunufaika na fursa zao kama zile za Zanzibar zinavyolindwa kwa Ubora wa Kizanzibar

Pili, matumizi ya rasilimali ni kuwabebesha mzigo. Hivi Ofisi ya Waziri mkuu Zanzibar inahusu nini?

Tatu, Rais SSH hawezi kulaumiwa kwa lolote, kinachofanyika ni referendum na kura zitaamua kama wanataka muungano au waondoke. Rais ana facilitate process, kura yake ni sawa na ya Mzanzibar mwingine, yaani ni 1 .

Watanzania Bara hawapaswi kufanya referendum kwasababu hawana lalamiko la muungano kama Wzbar

Tanzania bara wamewakubali ndiyo maana hakuna Mzanzibar anayebaguliwa bara kwa kitambulisho au lafudhi
Ndiyo maana Wazanzibar wanapewa nafasi za Ubunge kama kule Mkuranga, ajira popote ardhi n.k.

Kanuni za referendum ni zile zinazowahusu walalamikaji.
Mfano, Scotland walifanya referendum siyo UK. England, Wales na Ireland waliridhia kuwa chini ya Union Jack

Timor walifanya referendum kama walivyofanya Eritrea
Jimbo la Quebec Canada lilifanya referendum na siyo Canada yote

Puerto Rico, USA nao pia walifanya kama sitakuwa nimekosea

Hii ni fursa ambayo Marehemu Maalim alishawahi kuIzungumzia, kwamba iwepo Referendum

Leo Wazanzibar wanaogopa fursa iliyoletwa na Mwenyezi mungu! Nini kinawatisha?
Kama mkuu 'Zawadini' bado haelewi haya uliyoweka hapa na mifano halisi uliyoweka, siyo kwamba hana uwezo wa kuelewa, bali hataki kuelewa.
 
Nimesema 'kwa maoni yenu'. Hapa sijaona nilipokiri.

Mkuu hii ni tafsiri yako na maoni yako. Wacha yabakie kuwa yako usiyahusishe nami. Kwa lugha nyingine usinizushie uongo. Wacha yako yawe yako na yangu yabaki kuwa yangu.

Hapa unapiga ramli. Hemu jitahidi kusema ya kwako na yale yangu yaseme/yaandike kama nilivyoyaandika.

Ikitokea yamekushinda achana nayo. Wapo wanaoweza kujadili.
Ina maana wewe huna maoni, ila kazi yako ni kuwasilisha maoni ya wengine!
 
Back
Top Bottom