Ni halali Wazanzibari kufanya kazi za Watanganyika?

Ni halali Wazanzibari kufanya kazi za Watanganyika?

Lakini inawezekana pia ikadaiwa kwamba hiyo siyo njia sahihi ya kuondoa matatizo. Njia iliyo sahihi ni kutengeneza Katiba Mpya inayofafanua vizuri haya maswala ya Muungano.
Kwa kutumia njia hii, wananchi wenyewe ndio watakaokuwa wameamua hatma ya Muungano wao.
Mkuu Kalamu; muungano huu sio wa porojo au wa kienyeji. Tatizo, lalamiko au pendekezo lolote linapaswa kwanza kuangaliwa kisheria, na ni kupitia mkataba wa muungano (Articles of Union) na Sheria ya muungano (Act of the Union), ila kwa bahati mbaya, hili haliguswi kwa sababu wakubwa wanajua tukienda huko muungano huu haupo tena kisheria.

Hiyo katiba mpya tunayoililia sasa ni lazima ifuate matakwa ya sheria hiyo na mkataba huo. Hii ndio sababu kubwa mimi na wewe tunazungumza juujuu tu na wanasiasa wanatuletea visingizio vya udini, umajimbo na mengine wakijua tutacheza ngoma yao na kuacha kujadili mambo muhimu.
 
Nyerere aliunganisha hizi nchi huku akilini mwake akiiona Zanzibar kuwa ni ka nchi kadogo kenye watu wachache kwa hiyo akilini mwake akawa anawaza awape incentives na priveleges kedekede. Alisahau kuwa hata nchi ndogo inaweza kuwa na nguvu za kiuchumi kubwa kuliko nchi kubwa.

Matokeo yake leo, Zanzibar imepewa free access ya rasilimali na jasho la Tanganyika kupitia kile kinachoitwa muungano, huku Zanzibar yenyewe ikizilinda rasilimali zake ikiwemo mafuta na ardhi kwa wivu mkubwa!.

Tunapokwenda, Zanzibar itaenda juwa super rich kulinganisha na Tanganyika, na utajiri wao wataupata kupitia ujinga wa Tanganyika.

Nyerere alipopats Uhuru aliapa kuilinda Tanganyika matokeo yake kaenda kuigawa bure kwa Wazanzibari
 
1. Kundi linalopigania kuuvunja muungano kama unabvyosema linaungwa mkono sana sasa hivi na Vigogo

2. Hakuna kitu kinaitwa 'kero' bali kuna kitu ' nataka, nipewe n.k.
Mfano, Wazanzibar anataka account ya pamoja kwa mujibu wa VP OMO. Hivi account ya pamoja inakuwaje ikiwa miaka 40 hawachangii chochote? Hivi account ya pamoja inawezekana vipi ikiwa hawawezi kulipa umeme wa Bilioni 60? Account ya pamoja ina maana moja, kugawana rasilimali za Tanganyika.

Mfano wa pili: Kuruhusu bidhaa za Zanzibar ziingie bara bure. Zbar hawakusanyi kodi kwasababu ni bandari huru. Ikitokea wanachukua ni dollar 150 kwa kontena halafu wanaleta bara kwasababu ndiko soko lilipo.
Hili linafanya watu wakwepe kodi na tunakosa mapato, mwisho wa siku TOZO. Magufuli alikataa upuuzi huu lakini sasa umerudishwa.

Mfano wa tatu, wanasema account ya pamoja ni kugawana misaada. Ukiwauliza mikopo na madeni wanasema hilo ni la Watanganyika. Yaani kwao account ya pamoja ni kufaidika bila kuwajibika.

Kero ni ajira 21% za muungano, wakitaka vijana wao waajiriwe katika taasisi zisizo za muungano. Hapa kuna unafiki, wanalalamika mambo yameongezwa halafu wanataka ajira. Kuna unafiki na tatizo la elimu.
Huwezi kusema nguruwe haramu lakini mchuzi wake halali!

Marais watano hawakumaliza kero, leo kaja SSH , kamtuma Philip Mpango zimekwisha ndani ya mwezi mmoja tena kwa usiri mkubwa sana. Hakuna Mtanganyika anayejua isipokuwa Mpango.

Rais wa JMT ni Mzanzibar na SMZ ni Mzanzibar, sasa ni wakati wa REFERENDUM, waulizwe kama wanataka muungao. Wakisema wanataka turudi katiba ya Warioba mambo 7 tu. Wakisema hawataki njia nyeupee waende kuwa Singapore au Taiwani lakini pia wanaweza kuwa Haiti au Vanuata
Ninakuelewa vizuri sana.

CCM wameridhika sana, hawaoni kama kuna tatizo; kwani wao ndio wanaotengeneza hali iwe hivi.
Huko ndani ya CCM, mwenyekiti ni mungu, ndiyo maana akina Phillipo wanasujudu bila ya kuhoji. Kwa hali ilivyo huko ndani ya chama sioni mwenye ujasiri wa kuzungumzia haya wala kuanzisha mjadala juu yake.

Kwa hali ya nchi yetu ilivyo, si Kalamu wala Nguruvi3, wanaweza kuhoji na kujengea hoja kisheria na kupeleka mahakamani, ili mahakama iamue, ikiwa kama njia ya kuilazimisha serikali kuanzisha mchakato wa wananchi kuchukua hatua.

Kule kwenye "Fourth Estate", ni kama nchi haina vyombo vya habari vinavyoweza kudadisi lolote linalotokea ndani ya nchi, ili wananchi nao wapate mwamko juu ya swala husika.

Vyama vyetu vya Siasa nje ya CCM, tunawategemea (tuliwategemea) kwa matumaini CHADEMA, kwamba wataongoza juhudi hizi na kuzipeleka kwa wananchi. Lakini inaonekana sasa kuwa kuna kizingiti cha "MARDHIANO(?) kinachowabana?

Sasa tufanyeje?

Tupo hapa JF, tunafahamishana/elimishana... Nini kifanyike kurekebisha hali hii?
 
Mnatumiwa na wazungu nyie kwanza NI kwa kuwa hamna hela tu...siku nikipata hela naunganisha kutoka Moroccco/cairo mpaka cape town ! asiye taka kifo kinamuhusu!! ...mambo haya hayataki kubembelezana!
 
Mbona hata sasa tunao wananchi wengi (waTanzania) kutoka huko, una maana Tanganyika anaathirika kwa sababu ya watu hao kuwepo hapa?

Na kama hivyo ndivyo itakavyokuwa, kwa nini hao hao wakimbizi watarajiwa wasipewe uwezo wa kuzuia wasiwe wakimbizi wakati huu?
Na badala yake, hao wanaopanga kuwafanya wenzao kuwa wakimbizi, wao ndio wawe wakimbizi (sijui wakielekea nchi gani)?
Wazanzibari waliopo hapa Tanganyika wapo kwa hiari yao lakini baada ya muungano kuvunjika watakuja Wazanzibari wanaokimbia vita ya wenyewe kwa wenyewe na tutawaweka kwenye makambi!
 
Hiyo katiba mpya tunayoililia sasa ni lazima ifuate matakwa ya sheria hiyo na mkataba huo. Hii ndio sababu kubwa mimi na wewe tunazungumza juujuu tu na wanasiasa wanatuletea visingizio vya udini, umajimbo na mengine wakijua tutacheza ngoma yao na kuacha kujadili mambo muhimu.
Hapa sijakuelewa vizuri.
Una maana "sheria" hiyo ni zaidi ya Katiba itakayokuwa imewekwa na wananchi wenyewe?
Au sheria hiyo itazuia/inazuia uwepo wa Katiba Mpya?

Kukiri kwamba kuna kundi la wanasiasa wasiotaka jambo lijadiliwe ni sababu tosha kabisa ya kuchochea moto wananchi kuwepo juhudi za kulijadili jambo muhimu linalohusu nchi yao.
 
Wazanzibari waliopo hapa Tanganyika wapo kwa hiari yao lakini baada ya muungano kuvunjika watakuja Wazanzibari wanaokimbia vita ya wenyewe kwa wenyewe na tutawaweka kwenye makambi!
Dah,
Kwa hiyo Tanganyika iogope kuvamiwa na wakimbizi? Kwani haiwezi kuwawezesha wakimbizi tarajiwa wasiwe wakimbizi, na badala yake hao wanaotarajia kuwafurumusha wenzao ndio wawe wakimbizi huko kwingineko?
Kwani Tanganyika hii kweli inakosa kuwa na uwezo huo?
 
Mbona tumewashindwa Wanyarwanda na Warundi ambao kila kukicha tunapokea wakimbizi kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe!

Kumbuka hilo siyo suala la Tanganyika bali la kimataifa!
 
Mkuu Allen Kilewella , kwanza kazi ni kazi, hakuna kazi ya mtu, hivyo hakuna kazi za Mtanzania wala kazi ya Mzamzobari, kazi ni ya wote. Pili hiki ulichokileta ni ubaguzi wa kutaka kuwabagua Wazanzibari!. Mwalimu Nyerere alisema hii ni dhambi!. Kiukweli somo la uraia linahitajika sana Tanzania kwa watu kama wewe!. Tanzania ni nchi moja, ya JMT, yenye uraia mmoja tuu wa Tanzania, kila Mtanzania ana haki sawa na haki zote za raia wa Tanzania.

Ndani ya uraia wa Tanzania kuna uraia mmoja tuu wa Mtanzania.

Kwa vile Tanzania ni nchi moja ya JMT, ndani ya JMT kuna sehemu moja ya Zanzibar ina utawala wake wa ndani ambao Wazanzibari licha ya kwanza kuwa ni raia wa JMT wenye haki zote za uraia wa JMT, hawa wamepewa haki za ziada za ukaazi wa Zanzibar. Kitambulisho cha ukaazi wa Zanzibar sio kitambulisho cha uraia, hakuna uraia wa Zanzibar kuna uraia mmoja tuu wa JMT na ziada ya ukaazi wa Zanzibar.

Hivyo Wanzanzibari wana haki zote za uraia wa Tanzania na ziada ya haki za ikaazi wa Zanzibar.

Lile jambo langu likitimia, nafungua darasa la bure la Haki, kuwaelimisha Watanzania haki zao mbalimbali zikiwemo haki za uraia.
P
Hoja yake mtoa mada ni kwamba! Fursa wanazopata wazanzibari huku Tanganyika basi na sisi watanganyika tupate fursa hizo hizo huko kwao Zanzibar! Na siyo ubaguzi... Kama nimeelewa vizuri mada lakini..
 
Hoja yake mtoa mada ni kwamba! Fursa wanazopata wazanzibari huku Tanganyika basi na sisi watanganyika tupate fursa hizo hizo huko kwao Zanzibar! Na siyo ubaguzi... Kama nimeelewa vizuri mada lakini..
Wanaogopa kumezwa kutokana na uchache wao na udogo wa maeneo yao ukilinganisha na Bara ! Nadhani hii ndio hofu yao !!
 
Ni hivyo ulivyoandika lakini pia hawataki muungano uvunjike !!
Wanakula keki bila kuioka?
Wanaogopa kumezwa kutokana na uchache wao na udogo wa maeneo yao ukilinganisha na Bara ! Nadhani hii ndio hofu yao !!
Lakini ionekane kuwa sawa Tanganyika kumezwa; mithili ya mamba kummeza tembo?

Kwa nini isiwe sawa kwa wote kujulikana kwa uTanzania wetu. Lakini ipendeze zaidi kwa uZanzibari wao?

Sote tukiwa sawa kwa uTanzania wetu, kuna upungufu upi kwao?
 
Ndiyo maana tunawaambia Wazanzibar sasa ni wakati wao ikiwemo kuamua Referendum
Kwenda katiba mpya bila kujua Wazanzibar wanataka nini kutatusumbua na tutaendelea kuishi na tatizo

Kwasasa Wazanzibar wamekaa kimya ''Wana ula' kila wanachotaka wanapewa. Siku ''watakapoondoka'' utasikia kelele zinarudi. Marais wote ni Wazanzibar kitu gani kinashindikana katika referendum? Nini wanaogopa?
Hapana. Ni wakati wa Wabara kufanya hivyo kwani wao ni wengi. Wazanzibari wamesema na kudai sana. Sasa Wabara nao wafanye tuone
 
Hapa sijakuelewa vizuri.
Una maana "sheria" hiyo ni zaidi ya Katiba itakayokuwa imewekwa na wananchi wenyewe?
Au sheria hiyo itazuia/inazuia uwepo wa Katiba Mpya?

Kukiri kwamba kuna kundi la wanasiasa wasiotaka jambo lijadiliwe ni sababu tosha kabisa ya kuchochea moto wananchi kuwepo juhudi za kulijadili jambo muhimu linalohusu nchi yao.
Nakusudia umuhimu wa kuzijua nyaraka hizo mbili kwani ndio msingi wa muungano. Katiba itayotungwa lazima ifuate misingi na miongozo ya nyaraka hizo, vingine upande wowote unaweza kudai vinginavyo kama inavyotokea malalamiko ya sasa.
 
Nakusudia umuhimu wa kuzijua nyaraka hizo mbili kwani ndio msingi wa muungano.
Sawa, hata mimi ningependa kuiona; lakini sikubaliani na hilo la kusema Katiba Mpya ni lazima iheshimu hiyo sheria au sijui tuiite kitu gani.
Hii itakuwa sawa na kusema kwamba kuna sheria kuu zaidi ya katiba yenyewe, kitu ambacho si kweli.
 
Kukubali na kutokubali ni haki yako. Mimi nazungumzia hali ilivyo. Siwezi na sipaswi kukulazimisha.
 
Hapana. Ni wakati wa Wabara kufanya hivyo kwani wao ni wengi. Wazanzibari wamesema na kudai sana. Sasa Wabara nao wafanye tuone
Wrong! Wabara wanaweza kuamua kwa wingi wao ikawa, je hiyo italeta suluhu?

Kanuni zinasema referendum hufanywa kwa minority kama ilivyokuwa Eritrea, Timor, Quebec etc, VP OMO analalamika wingi wa Wabara unawanyima fursa? Wabara wanaweza kumchagua Rais bila Wazanzibar!

Pamoja na kuibeba Zanzibar Wabara hawakuwahi kulalamika hadi inapokuwa too much

Tatizo la muungano si Bara ni Zanzibar ambapo Uzanzibar ni bora lakini kwenye mafao Utanzania ni muhimu!

Wazanzibar wamepiga kelele miaka mingi wanakaliwa na majeshi, wanaonewa na viongozi wa Tanganyika
Mwenyezi mungu kaleta neema, Rais wa JMT ni Mzanzibar na wa SMZ ni Mzanzibar!
REFERENDUM inashindikanaje?

REFERENDUM! REFERENDUM! kwa Wazanzibar
 
Back
Top Bottom