Zawadini
JF-Expert Member
- Feb 2, 2012
- 2,369
- 1,775
Mkuu Kalamu; muungano huu sio wa porojo au wa kienyeji. Tatizo, lalamiko au pendekezo lolote linapaswa kwanza kuangaliwa kisheria, na ni kupitia mkataba wa muungano (Articles of Union) na Sheria ya muungano (Act of the Union), ila kwa bahati mbaya, hili haliguswi kwa sababu wakubwa wanajua tukienda huko muungano huu haupo tena kisheria.Lakini inawezekana pia ikadaiwa kwamba hiyo siyo njia sahihi ya kuondoa matatizo. Njia iliyo sahihi ni kutengeneza Katiba Mpya inayofafanua vizuri haya maswala ya Muungano.
Kwa kutumia njia hii, wananchi wenyewe ndio watakaokuwa wameamua hatma ya Muungano wao.
Hiyo katiba mpya tunayoililia sasa ni lazima ifuate matakwa ya sheria hiyo na mkataba huo. Hii ndio sababu kubwa mimi na wewe tunazungumza juujuu tu na wanasiasa wanatuletea visingizio vya udini, umajimbo na mengine wakijua tutacheza ngoma yao na kuacha kujadili mambo muhimu.