Ni halali Wazanzibari kufanya kazi za Watanganyika?

Ni halali Wazanzibari kufanya kazi za Watanganyika?

CCM wakishindwa hoja wanaanza kuchochea ubaguzi. Nchi imewashinda.

Wazanzibar wamepiga kelele miaka mingi wanakaliwa na majeshi, wanaonewa na viongozi wa Tanganyika
Mwenyezi mungu kaleta neema, Rais wa JMT ni Mzanzibar na wa SMZ ni Mzanzibar! REFERENDUM inashindikanaje?
Hili halina nguvu. Sisi tunaongozwa na katiba na haijalishi rais ni kutoka upande gani kwani bado kuna taasisi za JMT ambazo hata raisi apende apendavyo, hana budi kufuata sheria na katiba.

Kumbuka vyombo vya usalama ndivyo vinavyosimamia usalama wa JMT. HIVI rais atafanya kitu gani ambacho kinatoshia usalama alafu aachiwe? Kumbuka kilichotokea baada ya kifo cha Magufuli.

Huu ukidogo Wazanzibari ndo unaofanya hilo kuwa gumu. Nadhani unachotaka wewe Wazanzibari wafanye alafu Bara waseme Wazanzibari wamekuwa wasaliti nawe nna hakika utakuwa wa kwanza.

Kumbuka sana maneno ya Lukuvi ambayo nayachukulia ndo msimamo wa Wabara na sitarajii kwamba Wazanzibari wataingia kwenye mtego, iwe wananchi au maraisi, kama unavyodai, kwa sababu tu wao ni Marais.
 
Duh!

Hata Jumbe mwenyewe niliyemtaja hapo juu; si ni akina Maalim waliomchomea utambi?

Kwa hiyo mambo yanaanzia huko huko kwa waZanzibari wenyewe?

Hata hivyo, sina mfano, na sijui kama unao mfano wewe, mahsusi wa waZanzibari walioko CCM, waliokomalia jambo ambalo CCM ya waTanganyika hawakulitaka na wakafanikiwa kulipitisha walivyotaka wenyewe bila ya baraka za CCM Tanganyika.
Bendera na Katiba ya Zanzibar?
Mfano mahsusi ambao wewe huna ni huu hapa.
Kabla ya kurudishwa kwa mfumo wa vyama vingi Tanzania 1992, Rais wa Zanzibar automatically alikuwa ni Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Watanganyika wakabadilisha Katiba kimabavu kumuondoa Rais wa Zanzibar asiwe Makamo wa Rais kwa kuhofia kuwa iko siku Zanzibar itaongozwa na Upinzani, Sasa itakuwaje mpinzani awe Makamo wa Rais.

Wazanzibar hawakuliafiki hili wala hawakuridhia, ulitumika ubabe tu chini ya Spika Pius Msekwa kuvunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano kwa kupindisha utaratibu wa kulipigia kura jambo kama lile.

Katiba inatamka utaratibu wa kura ni kuwa jambo kama lile ili liwe limepita lazima ni lazima likubaliwe na thuluthi 2 ( two third) ya Wabunge wa kila upande wa Muungano.

Walichofanya ni kuchukua 2/3 ya kijumla wakijua kuwa Wabunge wote wa Upande wa Zanzibar hawafiki 2/3.
 
Pili, zile ajira asilimia 21% zilizotengwa kwa Wazanzibar ni pamoja na mambo yasiyo ya muungano, je hiyo ni kuwatendea haki Watanganyika ambao hawana fursa hiyo Zanzibar kwa ubaguzi wao

Kwa lugha rahisi Wazanzibar wanalaani kuongezwa kwa mambo ya muungano kama elimu ya juu, lakini hao hao wapo bodi ya mkiopo ya elimu ya juu na wanapewa bure (hawakopi) kutoka HESLB

Nimegundua una chuki zilizopitiliza kwa Wazanzibar sijui walikufanya nini hawa watu.

Unaandika uongo hata aibu huoni ili kufitinisha Watanzania?

Enzi za awamu ile watu kama vyinyi ndio mnaookotwa kwenye viroba au kuwa wakimbizi wa Ethiopia na kuokotwa mto Ruvu.
 
Yaani uvamizi alioufanya Nyerere umalizike kwa REFERENDUM au kwa kesi za mahakamani? Kama wapi kihistoria iliwahi kutokea hivyo? Uvamizi ulioletwa kwa vurugu, unaomwaga damu za Wazanzibari, unaowapa watu vilema hauwezi kumalizwa kiungwana au kidiplomasia. Acheni kupotosha umma.

Nope! hupo informed. Kama taasisi ni muhimu BUNGE ni taasisi na mhimili. Unakumbuka yaliyomkuta JOB.
Rais kutoka upande fulani ana matter sana. Rejea hoja za G55 Vs AH Mwinyi.
Hapa unalinganisha vitu visivyofanana. Ndugai ni mwanachama wa CCM. Wakuu wa vyombo vya ulinzi hawatakiwi kuwa wanachama wa chama cha siasa. Ni vivyohivyo G55. Kama unakumbuka mwalimu alisema serikali tatu siyo sera ya CCM na ndipo wahusika wakaufyata wakihofia kukosa kula.
Tanganyika anaweza akahitimisha muungano. Ili kuwa fair kwa wananchi wa pande mbili wale wenye Manung'uniko ya muda mrefu( Wazanzibar) wasikilizwe.
Hapa ndo kwenye hoja yangu. Kama ni referandum ifanywe na Wstanzania wote. Matokeo yatakavyokuwa mafuatwe ya Wazanzibari kama ilivyofanywa kwa ripoti ya Nyalali. Hii itaondoa dhana kwamba ni Wazanzibari ndo wameenda kwenye referandum.
kwasababu ya kujiona bora, Zanzibar wanataka mikopo lakini deni linalipwa na Mtanganyika
Mikopo yote inalipwa na JMT ambayo imekopa na sio Tanganyika.
kwasababu ya kujiona ni bora, wanataka ajira 21% hata
Hili ama hulijui au unapotosha makusudi. 21% ni kwa nafasi za taasisi za muungano na hili limeanza 2017 wakati muungano huu upo tangia 1964.
kwasababu ya kujiona bora Wazanzibar wanataka apewe 4.5% ya rasilimali za bara
Na hili unapotosha kwa makusudi. Swala la 4.5% lilikuja wakati wa kugawana mali za EAC iliyovunjwa na Nyerere na Kenyatta, ndipo JMT ikatafuta mshauri elekezi kushauri ambapo alishauri hiyo 4.5%. JMT ikaamua huo utakuwa ndo utaratibu kwa mgao wa muungano. Zanzibar haina lake kwenye hili.
Kama hawataki waondoke kwa amani, tutaishi nao kama Majirani
Hili ni la kila mmoja. Na Wabara kama hawataki waondoke
Maneno ya Lukuvi ni ya Lukuvi ikiwa tutaenda kudonoa maneno ya watu na kuyafanya ya jumuiya tunayo maneno na video ya Akina Ally Salehe wakiombea mabaya Tanzania bara, akina Jusa , OMO etc
Haya yametoka kinywani mwa Lukuvi lkn pia ndo msimamo wa Wabara wengi.
Unataka tufungue pandora box?
Mkuu nguruvi; hili ndo nilitakalo. Hemu fungua tuone. Haya mabox yapo mawili.
 
Hapa ndo kwenye hoja yangu. Kama ni referandum ifanywe na Wstanzania wote. Matokeo yatakavyokuwa mafuatwe ya Wazanzibari kama ilivyofanywa kwa ripoti ya Nyalali. Hii itaondoa dhana kwamba ni Wazanzibari ndo wameenda kwenye referandum.
Kwanini Zanzibar wanaogopa referendum? Si wanataka kuachana na Mkoloni?
Hili ni la kila mmoja. Na Wabara kama hawataki waondoke
Wabara waendoke wapi? Tanganyika imebeba Wazanzibar wengi duniani.Hulijui hili?
Tanganyika imebeba muungano. ''Muulize'' Jumbe, Salimin Amour na Amani Karume!
Haya yametoka kinywani mwa Lukuvi lkn pia ndo msimamo wa Wabara wengi.
Mkuu nguruvi; hili ndo nilitakalo. Hemu fungua tuone. Haya mabox yapo mawili.

Nakupa linki hii hapo chini. Ally Salehe ni Mbunge wa Zanzibar

Dakika ya 9.48 anasema Wazanzibar hawana mapenzi na Muungano. Je hiyo ndiyo kauli ya Wazanzibar?
Dakika ya 2.33 ''kuna nchi mbili'' akimaanisha Tanzania bara na Zanzibar. Kwamba Zanzibar si Tanzania.
Dakika ya 5, Ally anasema mchango wa mapato ya Zanzibar katika muungano ni 2% na Tanzania bara 98%.
Mapato ya TRA hayavuki bahari hivyo mchango wa Zanzibar ni 0, hiyo 2% ni nominal

Dakika ya 8.56, anasema pesa za muungano zinatumika bara.Muungano unaendeshwa na mapato gani?

Dakika ya 3.31 Ally anasema JMT inapuuza katiba. Ally alikuwepo katiba ya Zanzibar 2010 ikipuuza ya JMT.

Dakika ya 9.48 Ally na wenzake hawataki na hawana mapenzi na muungano

Je, kauli ya Ally ni ya Wazanzibar kama ile ya Lukuvi?

Referendum kwa Wazanzibar watoe maduku duku, tuachane na unafiki
 
Mfano mahsusi ambao wewe huna ni huu hapa.
Kabla ya kurudishwa kwa mfumo wa vyama vingi Tanzania 1992, Rais wa Zanzibar automatically alikuwa ni Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Watanganyika wakabadilisha Katiba kimabavu kumuondoa Rais wa Zanzibar asiwe Makamo wa Rais kwa kuhofia kuwa iko siku Zanzibar itaongozwa na Upinzani, Sasa itakuwaje mpinzani awe Makamo wa Rais.

Wazanzibar hawakuliafiki hili wala hawakuridhia, ulitumika ubabe tu chini ya Spika Pius Msekwa kuvunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano kwa kupindisha utaratibu wa kulipigia kura jambo kama lile.

Katiba inatamka utaratibu wa kura ni kuwa jambo kama lile ili liwe limepita lazima ni lazima likubaliwe na thuluthi 2 ( two third) ya Wabunge wa kila upande wa Muungano.

Walichofanya ni kuchukua 2/3 ya kijumla wakijua kuwa Wabunge wote wa Upande wa Zanzibar hawafiki 2/3.
"Mfano mahususi?"
Kwa kuwa unautoa wewe, ukidhani wewe ni mjuaji kuliko wengine juu ya haya mambo?

Mfano wenyewe ulioutoa ni 'irrelevant' na wala hujakana kwamba mambo mengi mnayolalamikia juu ya viongozi kutoka Zanzibar, ni nyinyi wenyewe ndio wahusika wa kuwaweka katika hatihati. Yakishawapata, mnageuka kulaumu kwamba ni watu toka Tanganyika ndio wanaowaonea viongozi hao. Huu ni zaidi ya unafiki, na tabia hiyo inajionyesha wazi hata katika maelezo yako hapa.

Hopeless Kabisa.
 
Pili, zile ajira asilimia 21% zilizotengwa kwa Wazanzibar ni pamoja na mambo yasiyo ya muungano, je hiyo ni kuwatendea haki Watanganyika ambao hawana fursa hiyo Zanzibar kwa ubaguzi wao

Kwa lugha rahisi Wazanzibar wanalaani kuongezwa kwa mambo ya muungano kama elimu ya juu, lakini hao hao wapo bodi ya mkiopo ya elimu ya juu na wanapewa bure (hawakopi) kutoka HESLB

Nimegundua una chuki zilizopitiliza kwa Wazanzibar sijui walikufanya nini hawa watu.

Unaandika uongo hata aibu huoni ili kufitinisha Watanzania?

Enzi za awamu ile watu kama vyinyi ndio mnaookotwa kwenye viroba au kuwa wakimbizi wa Ethiopia na kuokotwa mto Ruvu.
Lillobaki kwa watu kama wewe, ambao kwa kweli siyo wawakilishi wa waTanzania wengi waliko Zanzibar ni kuacha kuwabembeleza na kuwazawadia kila mnapopiga vikelele vyenu vya kipuuzi kuhusu Muungano

Samia sasa anawaweka kwenye hatua ngumu zaidi kwa haya anayoyafanya sasa. Usidhani itakuwa hivi daima, na wala usiote kamwe kwamba Muungano utavunjika. Kundi lenu halina ubavu wa kufanya hivyo. Mtaendelea kulalamika na hakuna atakayewasikiliza, na Tanzania itazidi kuimarika.

Mtafanya nini?
 
Wewe ndiyo mbaguzi. Kwa nini hupigi kelele Wakenya, Wanyarwanda, Waganda, na wengineo hawajitambulishi kama Waafrika wenzako? Wanajitambulisha tu kama Wakenya, Wanyarwanda, Wanaigeria, n.k. Wazanzibari wakijitambulisha kama Wazanzibari kinakuuma. Huo ni ubaguzi. Kukataa kuutambua Uzanzibari wa Wazanzibari ni ubaguzi.

Free Zanzibar.
Iko siku haya yatakwisha tu ni suala la muda tu.
 
Kwanini Zanzibar wanaogopa referendum? Si wanataka kuachana na Mkoloni?
Wazanzibari hawaogopi na hawatoogopa muungano. Hoja ni kwamba Tanzania ni Bara na Zanzibar, kwanini Wazanzibari pekee ndo waende kwenye referendum? Wabara wao wafanyeje?
Wabara waendoke wapi? Tanganyika imebeba Wazanzibar wengi duniani.Hulijui hili?
Tanganyika imebeba muungano. ''Muulize'' Jumbe, Salimin Amour na Amani Karume
Hapa nazungumzia Tanzania. Wabara ikiwa hawataki muungano waondoke kwenye muungano na Wabaki na Bara yao au Tanganyika yao; uamuzi ni wao. Ukisoma soma kwa umakini
Dakika ya 9.48 anasema Wazanzibar hawana mapenzi na Muungano. Je hiyo ndiyo kauli ya Wazanzibar?
Kama nilivyosema kuwa kauli ya Lukuvi ndo msimamo wa Wabara wengi ni vivyohivyo kwa kauli ya Ali Saleh ni msimamo wa Wazanzibari wengi sio wote.
Dakika ya 5, Ally anasema mchango wa mapato ya Zanzibar katika muungano ni 2% na Tanzania bara 98%.
Mapato ya TRA hayavuki bahari hivyo mchango wa Zanzibar ni 0, hiyo 2% ni nominal
Nakubaliana naye
Dakika ya 8.56, anasema pesa za muungano zinatumika bara.Muungano unaendeshwa na mapato gani?
Yuko sahihi. Hivi fedha hizo zote zinahudumia muungano tu? Ie taasisi za muungano? Bakaa ktk matumizi ya muungano inaenda wapi?
Dakika ya 3.31 Ally anasema JMT inapuuza katiba. Ally alikuwepo katiba ya Zanzibar 2010 ikipuuza ya JMT.
Anasema kweli si tu inapuuza katiba bali pia inaenda kinyume na makubaliano ya muungano.
Dakika ya 9.48 Ally na wenzake hawataki na hawana mapenzi na muungano

Je, kauli ya Ally ni ya Wazanzibar kama ile ya Lukuvi?
Ukizungumza Ali na wenzake sisemi kitu kwani hili ni LAKE NA WENZAKE. Sipaswi kumuamulia mawazo yake. Niulize yangu.
Referendum kwa Wazanzibar watoe maduku duku, tuachane na unafiki
Narudia tena: kama ni swala la referandum ni kwa Watanzania wote na hapa nadhani kama kuna unafiki basi wewe ndo unaongoza.

Mkuu nguruvi; naomba kukumbusha na kutanabahisha kwamba muungano huu ni swala la kisheria na sio la kisiasa. Tusigeuze mambo kana kwamba hatujui.

Zawadini
 
Hili halina nguvu. Sisi tunaongozwa na katiba na haijalishi rais ni kutoka upande gani kwani bado kuna taasisi za JMT ambazo hata raisi apende apendavyo, hana budi kufuata sheria na katiba.

Kumbuka vyombo vya usalama ndivyo vinavyosimamia usalama wa JMT. HIVI rais atafanya kitu gani ambacho kinatoshia usalama alafu aachiwe? Kumbuka kilichotokea baada ya kifo cha Magufuli.

Huu ukidogo Wazanzibari ndo unaofanya hilo kuwa gumu. Nadhani unachotaka wewe Wazanzibari wafanye alafu Bara waseme Wazanzibari wamekuwa wasaliti nawe nna hakika utakuwa wa kwanza.

Kumbuka sana maneno ya Lukuvi ambayo nayachukulia ndo msimamo wa Wabara na sitarajii kwamba Wazanzibari wataingia kwenye mtego, iwe wananchi au maraisi, kama unavyodai, kwa sababu tu wao ni Marais.
Sasa Wazanzibar wakifanya watakuwaje wasaliti wakati nyie mnadai wanadai haki yao?. Who cares nani atawaira wasaliti, as long as wao wanaona ni jambo la kheri basi wao wenyewe watajiita mashujaa badala ya wasaliti.

Rais wa nchi ana nguvu, anaweza kuiamuru serikali yake iitishe referendum, sasa najiuliza kwa nini Samia asiitishe Referendum. Wenzake walishindwa, kwa nini yeye ashindwe?
 
Hili
Sasa Wazanzibar wakifanya watakuwaje wasaliti wakati nyie mnadai wanadai haki yao?.
Hili neno 'nyie' umekusudia akina nani?
Who cares nani atawaira wasaliti, as long as wao wanaona ni jambo la kheri basi wao wenyewe watajiita mashujaa badala ya wasaliti
They care as long as they are Tanzanians. Watanzania wenzao wakiwemo viongozi na vyombo vya usalama baada ya kuwaita wasaliti watawashughulikia. Kwa sasa kwa kuwa Wabara wanalalamika kwanini wao wasifanye hiyo referandum? Kwanini iwe wazanzibari?
Rais wa nchi ana nguvu, anaweza kuiamuru serikali yake iitishe referendum, sasa najiuliza kwa nini Samia asiitishe Referendum. Wenzake walishindwa, kwa nini yeye ashindwe?
Hivi umewahi kujiuliza kwanini Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Magufuli kwanini walishindwa? Ikiwa hukuwahi kujiuliza au kama unajua sababu za kushindwa kwao, basi sababu hizohizo ndo zinamfanya Samia ashindwe.

Try to be fair.

Zawadini
 
Katiba inatamka utaratibu wa kura ni kuwa jambo kama lile ili liwe limepita lazima ni lazima likubaliwe na thuluthi 2 ( two third) ya Wabunge wa kila upande wa Muungano.
Hizi ni porojo na upindishaji kama ilivyokawaida ya watu kama wewe.
Ni kifungu kipi cha Katiba kinachozungumzia haya uliyoandika hapa?
 
Wazanzibari hawaogopi na hawatoogopa muungano. Hoja ni kwamba Tanzania ni Bara na Zanzibar, kwanini Wazanzibari pekee ndo waende kwenye referendum? Wabara wao wafanyeje?
Kwa hiyo unakubaliana na wazo kwamba 'referendum' juu ya Muungano ni muhimu kwa sasa, na kwamba pande zote mbili zishiriki katika referendum hiyo?
 
Hili

Hili neno 'nyie' umekusudia akina nani?

They care as long as they are Tanzanians. Watanzania wenzao wakiwemo viongozi na vyombo vya usalama baada ya kuwaita wasaliti watawashughulikia. Kwa sasa kwa kuwa Wabara wanalalamika kwanini wao wasifanye hiyo referandum? Kwanini iwe wazanzibari?

Hivi umewahi kujiuliza kwanini Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Magufuli kwanini walishindwa? Ikiwa hukuwahi kujiuliza au kama unajua sababu za kushindwa kwao, basi sababu hizohizo ndo zinamfanya Samia ashindwe.

Try to be fair.

Zawadini
Hao uliowataja ni marais waliotoja Tanganyika(including mzee Ruksa). Ambao Wazanzibari hudai imevaa koti la muungano kwa hiyo nisingetegemea wafanye chochote cha maana kulivua koti hilo

Sasa ni muda muafaka Wazanzibari wambananishe Mzanzibar mwenzao awape wanachokitaka, na sisi tutampiga presha atupe Tunachokitaka maana wengi tulikuwa tumelala kipindi kile cha maraisi waliotangulia, Sasa tumeshajua jinsi muungano huu unavyotupiga!.
 
Back
Top Bottom