Ni ipi siri ya Wachaga kuwa kabila lililoyaacha makabila mengine mbali mno kwenye mafanikio?

Ni ipi siri ya Wachaga kuwa kabila lililoyaacha makabila mengine mbali mno kwenye mafanikio?

Elimu! Elimu! Elimu!
Hii ndo siri kuu ya wachaga. Wakati uhuru unapatikana tayari wachaga walikuwa mbali sana kielimu. Shule za msingi na sekondari za kutosha. Kingine pia ni kujali mila na tamaduni zao. Kwa Afrika mashariki, kati na kusini hakuna kabila lenye maendeleo kuwazidi wachaga.
Hujafika kiambui mkuu. Wachagga wangekuwa mbali sana kama sio jitihada haramu za serikali kuwazuia.
 
Hujafika kiambui mkuu. Wachagga wangekuwa mbali sana kama sio jitihada haramu za serikali kuwazuia.
Mnalaumu serkali tena? Nikujurishe tu Wachaga walikuwa na fursa sana miaka hiyo! Saizi mambo yashabadilika maana hata Makabila mengine yanafanya biashara kwa ufanisi mkubwa tu! Mfano Wakinga hapo kariakoo,Waha hapo, Wakurya,Wasukuma huko Kanda ya ziwa (Mwanza,Kahama na Katoro).
Ukitaka kujua kuwa kuna jamii zina mafanikio makubwa wahoji wafanyakazi wa Mabenk nk
 
Us
Wachaga ni lile kabila kati ya 12 la Israel lililopotea (Lost tribe of Israel).

Kwa kifupi wachaga ni wayahudi wa Africa.

Tafiti za DNA zimethibisha kabisa.
Usifananishe wachaga na hao mashenzi mabaguzi yenye roho mbaya. Hivi kwani kujilinganisha nao ni sifa? Kwani hamuwezi kuwa nyie kama nyie? I hate this. Hakuna tafiti yoyote ile inayowaunganisha na mayahudi hayo. Na wala sio dili kuwa ndugu zao.
 
Wazanaki wapo juu, nafasi yenu bado ipo katika historia ya nchi hii, Nyerere tutamkumbuka sana maana pamoja na urais wake aliiweka nchi mbele na sio kupendelea kwao kwenye maendeleo, hata watoto wake hakuwapa upendeleo, ingekuwa vinginevyo basi wazanaki wangekuwa wameikamata sana hii nchi na huko uzanakini serikali ingekuwa imepaendeleza sana.

Ni kweli Nyerere hakutoa upendeleo sio Kwa wanae tu lakini hata mtoto wa dada yake wala mkwewe yeyote.

Lakini siku hizi utasikia kiongozi fulani ni ndugu wa Rais, ni Mtoto wa Rais, ni mpwa wale, ni mkwe wake, n.k.

Inaleta mgongano wa maslahi ya Umma na ya udugu/familia n.k.

Lakini hawaoni hata haya!

Tangu awamu ilopita tulishuhudia na sasa yanaendelea?!
 
Mnalaumu serkali tena? Nikujurishe tu Wachaga walikuwa na fursa sana miaka hiyo! Saizi mambo yashabadilika maana hata Makabila mengine yanafanya biashara kwa ufanisi mkubwa tu! Mfano Wakinga hapo kariakoo,Waha hapo, Wakurya,Wasukuma huko Kanda ya ziwa (Mwanza,Kahama na Katoro).
Ukitaka kujua kuwa kuna jamii zina mafanikio makubwa wahoji wafanyakazi wa Mabenk nk
Bro mchagga ni next level mkuu. Wewe unawapima kwa kuwaangalia kkoo. Unatakiwa ufanye utafiti kwa mfano. Kila nyumba moja ya familia ni watu wangapi wameendelea au kizazi cha ngapi kina hela. Ni kama mo dewji yule jamaa ni kizazi cha tatu chief so usije ukafungua duka au mkawa wengi ofisin ukasema mshakuwa sawa. Wenzio kwasasa ni system kabisa sio mtu mmoja. Unakuta familia ina mfumo wa maendeleo wa pamoja. Kwa mfano cc kijijin tunajenga barabara ya lami na daraja na juz kati tumemalizia kujenga ofisi ya kijiji na kituo cha polis. Hatusubir serikali. Tuna mfumo mtu yeyote akifa kila familia inatoa hela so kabla ya mazishi kuna ml.3 watu wote kijijin wameingizwa kwenye Kanz data. So hiyo unayosema ni hatua lakin bado sana kufikia level za watu wa kule kwetu aisee. Kwa mfano uchagan ukizungimzia familia kwa sasa unamaanisha baba mama na watoto. Lakin wengine ukizungimzia familia unamaanisha mjomba shangaz cjui nani so wigo wa matatizo ni mkubwa. Juz kati wakati wa Mh Magufuli. Laiti ungeweza kujua watu walivyocheza na biashara za Bond na masoko ya hisa huko dunian wala usingesema. So ni kweli watu wamepiga hatua lakin bado hatua endelevu hawajazianza japo ni vizur kupongeza.
 
Mnalaumu serkali tena? Nikujurishe tu Wachaga walikuwa na fursa sana miaka hiyo! Saizi mambo yashabadilika maana hata Makabila mengine yanafanya biashara kwa ufanisi mkubwa tu! Mfano Wakinga hapo kariakoo,Waha hapo, Wakurya,Wasukuma huko Kanda ya ziwa (Mwanza,Kahama na Katoro).
Ukitaka kujua kuwa kuna jamii zina mafanikio makubwa wahoji wafanyakazi wa Mabenk nk
Wasukuma gani?,wakinga gani? ,Waha gani? Kwa Tanzania hakuna kabila la watu matajiri kama wachaga ,na wachaga hawapo sehemu moja ukienda kila mkoa utawakuta
 
Sisi wachaga hatuna mambo mengi, Tunapiga kazi Kwa mstari na Ubahili WA kiwango cha juu.

Wachaga tukizipata tunawaza chap chap wapi tumetoka na nini cha maana kifanywe .

Kitu kingine kinachotufanya tufanikiwe ni kwasababu tupo Low key .

N.k
Pia sio wachagga wote tunafanya ubahili mkuu ni baadhi ya wachagga kadhaa, mimi kama mimi siwezi kubana au kujibana kwa kitu nipendacho, yaani niko nina njaa nisile au nisinunue msosi au nimnyime mtu, hilo sinaga kwangu mkuu...

Wapare na baadhi ya wachagga wachache kama wewe ndiyo mna ubahili kiwango cha juu. Kina chuwa, sijui Swai na baadhi ya kina Mallya mna laana ya ubahili 😆😆😆
 
Wasukuma gani?,wakinga gani? ,Waha gani? Kwa Tanzania hakuna kabila la watu matajiri kama wachaga ,na wachaga hawapo sehemu moja ukienda kila mkoa utawakuta
Sio kila mkoa mimi nina ndugu zangu wapo Congo Drc wanafanya biashara, ninao waliopo Canada na USA....wajomba zangu wapo Spain.
So ni desturi yetu kama wanaija kuwa mapopo kwenye nchi za watu.
 
Pia sio wachagga wote tunafanya ubahili mkuu ni baadhi ya wachagga kadhaa, mimi kama mimi siwezi kubana au kujibana kwa kitu nipendacho, yaani niko nina njaa nisile au nisinunue msosi au nimnyime mtu, hilo sinaga kwangu mkuu...

Wapare na baadhi ya wachagga wachache kama wewe ndiyo mna ubahili kiwango cha juu. Kina chuwa, sijui Swai na baadhi ya kina Mallya mna laana ya ubahili 😆😆😆
Hatuwezi tukawa wote wabahili mangi 🤣,
wale ambao Ela ikiingia Tu ni marathon ya kumbizana na chupa, huku mbuzi choma pale kitochi uwepo wenu unatambulika na unaheshimika zaidi mwezi WA 12 .

Wachaga ela ya kutumia ikiwepo inatumika cha muhimu zaidi ni Ela kutumika Kwa Nidhamu
 
Mimi tungi sinywi ila naishi kizungu mkuu yaani sijibani kwenye matumizi muhimu niko na historia ya koo moja wanaitwa Chuwa ni wabahili sana Bibi mzaa baba alitoka huo ukoo unaambiwa alikuwa zamani anaficha pesa ndani mpaka zinatoa ukungu ule ukijani si unajua huku baridi.

Ikifika wakati wa jua kuwaka anatoa zile noti anaanika juani 😁😁😁 kwa ubahili ni mbahili kumbe koo yao nimekuja chunguza wapo hivyo yaani ni wachoyo pia wabinafsi sana wao wenyewe hawajipendi.

Wachagga wa mbokomu huko kirua, wachagga wa Uru wanaongoza kwa ubahili, alafu wamachame na wanarumu wafuate......

Ila wamarangu wengi ni wachagga smart ni siyo wabahili.
Wakibosho na warombo wanakunywa sana ila pesa zao huwa hawajui kuzitumia wise kama wamarangu, yaani wengi wao ni washamba wako na sifa fulani hivi kama kibosho wanashusha mjengo mkali ili wapate sifa.....ila hayo si maisha.
 
ENEO PEKEE WALILOSHINDWA KUFANIKIWA, NI KWENYE NDOA.

NDOA ZAO HAZIDUMU KABISAA.

MAENEO MENGINE WAKO VIZURI
Kweli kabisa kwenye ndoa na mahusianonhawa jamaa wanayumba haswa !!
Ila wana nidhamu sana ya pesa ndo maana wanakuwa na maendeleo na kusomesha vizuri watoto wao
 
Licha ya umasikini wetu wa taifa hapakosekani kundi la watu wenye nafuu, Tukigusia makabila yenye asili ya hapa kwetu, jamaa wapo mbali mno.

Kunaweza kuwa na makabila yanayowafatia ila ni gepu refu mno.

1.Elimu: Hawa watu wamesoma sana na shule zipo huko kwao tangu zamani sana, sehem zao kuna shule nyingi sana, hapa wenzao ni wahaya lakini tatizo wahaya wana shule chache sana huko kwao na sehemu waliyosifika ni kwenye elimu tu.

Biashara - Ni kama kipaji chao cha asili hata kwa ambao wameishia darasa la 7 wapo wanaofanya makubwa, ukija kwa wasomi nako wamejaa wamefungua makampuni, najua kuna wanaofatia wapo wakinga, waha, wasukuma, n.k ila wameachwa mbali sana.

siasa - ukiachana na ccm hawa ndio waasisi wakubwa wa vyama vingi maarufu vya upinzani kuanzia tlp, nccr, chadema, vyote vina asili ya wachaga,

kuendeleza na kujenga kwao hawana mpinzani, nimeona makabila mengine wengine wanajaribu jaribu wanajenga nyumba za kisasa huko vijijini kwao ila unakuta kijiji kizima nyumba hizo zinahesabika,

Kwenye system na political positions hawajajaa sana
ila kila ofisi wamejaa, mashirika ya uma na kimataifa wapo.

kuridhika kwa wachaga ni ngumu sana, mtu alieridhika mara nyingi huonyesha majigambo na sifa, kuna baadhi ya watu wakipata hela basi wataanza laki si pesa, ist gari za watoto, n.k kwa wachaga mtu anaweza kuwa na pesa kibao ila bado ana nidhamu ya pesa laki 1 anaipangia bajeti, ataendesha hata passo ilimradi ajenge kwao nyumba nzuri, n.k.

Ni nadra sana kusikia mambo ya uchawi uchagani kwamba flani kamtupia jini jirani kisa mtoto wake kapata kazi, kurogana kisa ndugu kapiga hatua, n.k. uchawi ni adui mkubwa sana wa maendeleo na kwa kiasi kikubwa wamejitahidi kuukwepa, just imagine nina rafiki yangu wa huko Geita vijijini alitaka kuwajengea wazazi nyumba ya kisasa, watakataa, mwengine rafiki wa Njombe aliniambia huko kijijini kwao hata kuweka bati ni ishu nzito kwasababu majirani wanaweza kuchukia maendeleo wanaroga.

Wanaheshimu mila na desturi zao: kifupi wanajua wapi wametoka na wapi wanaenda, wachaga ikifika december kuna mtu asiejua balaa lao ? huwa ni kama waisrael wa sehem mbali mbali wanarudi kwao, hii pia inafanyika na kabila lililofanikiwa zaidi Nigeria waigbo hurudi kwao kila mwisho wa mwaka.
..........................

Kwa wengi unaweza kukuta kwenye elimu wapo ila kwengine zero

wengine unaweza kuta wanajitahidi biashara ila huko kwao hakutamaniki na elim bado sana

n.k.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom