Ni jambo gani unalotakiwa kulifanya pindi unapopitia wakati mgumu sana. Fedha na matatizo ya mara kwa mara kama vile kuuguza kwa muda mrefu

Najua vile unavyohisi najua hata usingizi wako ni shida na huenda ukishtuka usingizini unaweza usilale tena kwani hujui watoto wako watakula nini,nimepitia hayo nayajua vizur sana
Hii inaumiza sana Mkuu. inabidi ushinde mtaani maana kila ukiitazama familia machozi yanashuka.
 
Ni jambo gani la hekima sana unaloweza kufanya Ili upite salama kwenye Kipindi cha aina Hii.
Jambo dogo sana. --Shukurani.--

Ukikopa, ukila, ukiumwa, ukitukanwa, ukisaidiwa... Shukuru. Kwa kutumia shukrani utatoka hiyo level haraka sana
 
nashukuru hajanikimbia Tupo nae kwenye mapambano. Matatizo yanaitana hata ukipata laki leo utashangaa mtoto anaumwa, mama yake. vinatokea tokea Vitu hadi hela ianisha yote. Biashara haziendi maana mtaji wote umekatikia Hospi. imebidi frem ibaki na shelvu tu yaani na Chupa Tupu.
 
Ukishaleta mtoto kwenye hii dunia au kuwa na familia wakati uwezo wako bado ni wa mpeche mpeche, Matatizo na umaskini lazima vikutwange kisawasawa.

Hadi akili ikukae sawa sawa.

Kabla ya kuleta kiumbe kwenye hii dunia hakikisha utaweza kukihudumia mahitaji yake yote pamoja na kujihudumia wewe binafsi.
 
Kama mtu angeijua kesho yake kuna vitu huwezi kufanya. Kufilisika ni jambo dogo sana Mkuu. Ila asante kwa ushauri mzur
 
shukran kwa Ushauri. Mungu tunamwita sana Mkuu ila mambo yanazidi kuongezeka kila siku vitu vipya
Hakuna Mungu wa kukutatulia matatizo yako.

Chanzo cha matatizo yako ni wewe mwenyewe.

Na wakutatua matatizo yako ni wewe mwenyewe.

Mungu hajawahi kuwepo na hayupo kumsaidia kiumbe chochote kile kwenye matatizo.
 
Hakuna Mungu wakuitwa kwenye matatizo. Mungu huyo hayupo.

Chanzo cha matatizo yako ni wewe mwenyewe, Na jibu la matatizo yako ni wewe mwenyewe.
 
Ukiona mwanaume amekuja kuelezea yanayomsibu ujue hali sio hali ,,,, ! Mkuu Pole jipe moyo, sijajua status yako before, lakini kwa hiki kipndi kigumu jikite kwenye shughuli ambazo pengine hukuwahi kufanya/kuzizoea mwanzo mfano udalai, uwinga, saidia fundi n.k huku ukipata kipato kwa ajili ya kujikimu wewe na familia,,,, baada ya mda mambo yatakaa sawa tu
 
Kuna shughuli naifanya ila mambo ya kuuguza yamemaliza Uchumi na yameniacha na madeni sana Na bado naendelea Kuuguza. Shughuli inakuwa Ngumu sana bado matatizo ya hapa na pale yanajitokeza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…