Ni jambo gani unalotakiwa kulifanya pindi unapopitia wakati mgumu sana. Fedha na matatizo ya mara kwa mara kama vile kuuguza kwa muda mrefu

Ni jambo gani unalotakiwa kulifanya pindi unapopitia wakati mgumu sana. Fedha na matatizo ya mara kwa mara kama vile kuuguza kwa muda mrefu

Najua vile unavyohisi najua hata usingizi wako ni shida na huenda ukishtuka usingizini unaweza usilale tena kwani hujui watoto wako watakula nini,nimepitia hayo nayajua vizur sana
Hii inaumiza sana Mkuu. inabidi ushinde mtaani maana kila ukiitazama familia machozi yanashuka.
 
Ni jambo gani la hekima sana unaloweza kufanya Ili upite salama kwenye Kipindi cha aina Hii.
Jambo dogo sana. --Shukurani.--

Ukikopa, ukila, ukiumwa, ukitukanwa, ukisaidiwa... Shukuru. Kwa kutumia shukrani utatoka hiyo level haraka sana
 
Vipi kuhusu mkeo ?
mmeungana kwenye haya mapito au nae kakikumbia?
kama mpo pamoja mpaka mida hii na misukosuko yote hiyo mshukuru Mungu sana.

Panga na mkeo Nini mnaweza Fanya,mkeo anaweza anzisha biashara ndogo kama kukaanga maandazi,chapati akazungusha na wewe kuwa tayari kufanya kazi ambazo hukuzizoea jua hiki ni kipindi cha kudharirika uza hata genge Kwa kipindi hiki huku ukiaikilizia issue za maana huku mke nae anapambana mtatoboa kipindi hicho kigumu,maisha ndio yalivyo Yana ups and. downs .
nashukuru hajanikimbia Tupo nae kwenye mapambano. Matatizo yanaitana hata ukipata laki leo utashangaa mtoto anaumwa, mama yake. vinatokea tokea Vitu hadi hela ianisha yote. Biashara haziendi maana mtaji wote umekatikia Hospi. imebidi frem ibaki na shelvu tu yaani na Chupa Tupu.
 
Ukishaleta mtoto kwenye hii dunia au kuwa na familia wakati uwezo wako bado ni wa mpeche mpeche, Matatizo na umaskini lazima vikutwange kisawasawa.

Hadi akili ikukae sawa sawa.

Kabla ya kuleta kiumbe kwenye hii dunia hakikisha utaweza kukihudumia mahitaji yake yote pamoja na kujihudumia wewe binafsi.
 
Kama mtu angeijua kesho yake kuna vitu huwezi kufanya. Kufilisika ni jambo dogo sana Mkuu. Ila asante kwa ushauri mzur
 
shukran kwa Ushauri. Mungu tunamwita sana Mkuu ila mambo yanazidi kuongezeka kila siku vitu vipya
Hakuna Mungu wa kukutatulia matatizo yako.

Chanzo cha matatizo yako ni wewe mwenyewe.

Na wakutatua matatizo yako ni wewe mwenyewe.

Mungu hajawahi kuwepo na hayupo kumsaidia kiumbe chochote kile kwenye matatizo.
 
Ukipitia kipindi ambacho juhudi na maarifa ya kibinadamu vimeshindwa mwite Mungu.
Ikiwezekana jifungie mahali umwite Mungu.
Hiyo ndio njia pekee ya kutoka kwenye jambo lililokwama kibinadamu
Wafilipi 4 : 6

Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.
For read more download the Bible using this link:
Swahili English Bible - Apps on Google Play
Hakuna Mungu wakuitwa kwenye matatizo. Mungu huyo hayupo.

Chanzo cha matatizo yako ni wewe mwenyewe, Na jibu la matatizo yako ni wewe mwenyewe.
 
Ukiona mwanaume amekuja kuelezea yanayomsibu ujue hali sio hali ,,,, ! Mkuu Pole jipe moyo, sijajua status yako before, lakini kwa hiki kipndi kigumu jikite kwenye shughuli ambazo pengine hukuwahi kufanya/kuzizoea mwanzo mfano udalai, uwinga, saidia fundi n.k huku ukipata kipato kwa ajili ya kujikimu wewe na familia,,,, baada ya mda mambo yatakaa sawa tu
 
Kuna shughuli naifanya ila mambo ya kuuguza yamemaliza Uchumi na yameniacha na madeni sana Na bado naendelea Kuuguza. Shughuli inakuwa Ngumu sana bado matatizo ya hapa na pale yanajitokeza.
 
Back
Top Bottom