Ni kisa au mkasa gani uliwahi kufanyiwa na ndugu au mtu wako wa karibu?

wewe ni mimi kabisa. ila nshamsamehe
 
Sitosahau mwaka 2021 nikiwa Arusha kwa ndugu nilifukuzwa Usiku wa saa tatu kisa sijaosha vyombo vya ndani aisee niliumia sanaa kama nisingekuwa najuana na majirani siku hiyo ningelala kwenye mitalo, nilienda kwa jirani nikapokelewa next day nikakata ticket ya kurud nyumban.

Secondly 2018 nikiwa form two nilikua naishi kwa ndugu yangu but alinipa chumba na akanambia nijitegemee Yani niwe najipikia nk na chumba alicho nipa nilikua nakilipia mwisho wa mwezi lakin funguo alikua anazimiliki yeye maana chumba kilikua ndani ya nyumba ambayo alikua akiish,, basi ikaja likizo ya mda mfupi nikarudi home vtu vyangu pamoja na vyomb nikaviacha, baada ya likizo nikarudi nikakuta chumba hakina vitu vyangu kina vitu vingne, kumbe yule mama kachukua vyombo vyangu pamoja Vitabu vyangu akaenda kutupa kwenye Banda la mbwa na kilicho niuma zaidi sufuria ambazo nilikua natumia akawa ndo anatumia yeye kurishia mbwa wake, aisee niliumia mno nikataman niache shule kabisa ila namshukuru Mungu alinisaidia alinipa moyo wa uvumilivu.

Kiufupi kuish kwa Ndugu changamoto sana labda upate ndugu mwenye moyo mzuri

Safari yangu ya Maisha Bado sana ndo kwanza naanza Mungu azidi kunitetea na kunipa moyo wa Uvumilivu.
 
Iam deeply sorry, y'al😐
 

Ila Sijui wahindi wanashida gani,

Kuna skin Product na import kutoka India, week kadhaa zilizopita nikapata ujio wa muhindi ofisini kwangu, akidai namuharibia soko kwa kuingiza bidhaa aliyokua anaingiza yeye.

Hivyo nikimaliza mzigo ni lazima nichukue kwake la sivyo atanipeleka polisi.

Ajabu ni kwamba Bei anayoniuzia kwa 500pcs ni Bei nnayouza kwa mteja wa less than 6pcs

Sasa nimekataa ananifata anaomba tufanye Kazi pamoja..
Kwa kweli nimekataa kata kata.
 
KAZA WEWEEEE!
 
Sijapata nafasi ya kua karibu na ndugu kiasi Cha kusema wafanye lini-impact directly!
Ulikuwa matawi ya juu wewe! Kongole kwa wazazi wako walijitambua wakakuandalia maisha mapema. Na hukuteseka na ndugu
 
Ndugu yangu wa mbali kaja mjini kakaa kwangu miezi 2. Cha ajabu alivyoondoka kaenda kunianika kijijini kuwa tunakula wali maharage Kila siku jioni....na Dagaa kabichi mchana na kwamba wife atakua mchoyo!
Ndugu wa hovyo wapo kila ukoo
 
Tatizo kubwa la wahindi ni kudharau uwezo wa kiakili wa watu weusi. Siku zote wanaamini mtu mweusi ni wa kuburuzwa. Hata ikitokea akakubali ufanisi wako atahakikisha anamuweka muhindi mwenzie karibu ili achukue ujuzi wako na mwisho wa siku akutimue pale anapokosa haja na wewe.
 
Sometimes watu wakiishi wenyewe wanaitwa wabinafsi. Ila inakuepusha na mengi kwa kweli. Ila yaliyonipata kwa so called ndugu na watu wa karibu hakika mengine nitaenda nayo kaburini. Naamini nafsi yangu itapona hata kama ni uzeeni [emoji119]
 
Kuna jamaaa mmoja alifukuzwa geto sekondari na wenzake hakua na msosi Wala Kodi ya nyumban mm niko kidato Cha pili yeye Cha tatu, nikamulea Hadi akamaliza shulen vizuri, siku ya mwisho nikamuomba aniachie vitabu akaomba hela, nikawa Sina, akapata kazi baadae Mambo mazuri nikwa na mm namishe kidogo nikamwambia nipo hapa Arusha vipi nikuone ndugu tusalimiane hajkujibu chochote. Akabadilishwa kituo Cha Kaz akaja mkoa nilipo akaletwa anatafuta nyumban ya kupanga kabla ya salamu akaniomba msamaha.
 

Msela mafiii huyo na mbinafsi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…