Ni kisa au mkasa gani uliwahi kufanyiwa na ndugu au mtu wako wa karibu?

Ni kisa au mkasa gani uliwahi kufanyiwa na ndugu au mtu wako wa karibu?

We jamaa utaenda motoni kwa ule uzi wako ambao utaishi milele na milele humu JF ambao ulikufanya uende jela kwa muda (banned) [emoji23][emoji23][emoji23][emoji1487]

Nikimuona Dogo Aslay huwa nahisi ndo wewe [emoji28][emoji1474]

Au ndiye?! [emoji848][emoji848][emoji848]
Hapana mkuu sio mimi...[emoji28][emoji28][emoji28]
 
Nilishawahi kuajiriwa na muhindi mmoja kama project manager. Ali apply tender iliyohusisha kuweka signage (mabango) nchi nzima kutoka kampuni moja maarufu ya Makaburu (South Africans). Kipindi hicho ilikuwa project yenye thamani ya kama $100,000.

Kabla ya kupata tender kulikuwa na bidding ambapo moja ya sharti ilikuwa ni kuwakilisha installation plan (proposal) iliyohusisha uchambuzi wa matumizi ya budget, utekelazaji wa kazi mpaka kukamilika kwake.

Nilifanya kazi ya kuandaa plan wiki 2 nzima usiku na mchana maana ilikuwa inahitajika haraka. Ilipotimia na kuwakilishwa muhindi akashinda tender.

Ilipoidhinishwa tu kuwa kashinda jamaa akaniambia kuna muhindi mwenzie toka India (expatriate) atasimamia hiyo project (kutumia plan yangu), moja ya makubaliano yetu ya awali ilikuwa nitaisimamia mimi hiyo project yote endapo proposal yangu itapita.

Aliposema mambo ya expatriate tu nikatoa notice yangu ya mwezi mmoja ya kuacha kazi.

Kipindi nataarisha plan ya hiyo project nilifanya research ya kutosha nikijua nitasimamia mimi mwenyewe hivyo niliweza kuhalalisha baadhi ya matumizi ya budget nikijua nitafanikisha vipi baada ya research yangu.

Phase ya kwanza ya project ilianzia mikoa ya Tanga, Arusha na Moshi. Muhindi alipopewa mzigo installation ianze akachemka baada ya kumaliza Tanga tu. Pesa ilikata na kazi hata robo haijaisha.
Kila sehemu ilikuwa na time limit kama ilivyoanishwa kwenye proposal plan, muhindi alichemka phase ya kwanza tu huku ikiwa keshachukuwa advance ya Mkaburu.

Nilifanya presentation mimi mwenyewe kwenye bidding kwa niaba ya muhindi, hivyo sharti aliliopewa na makaburu ni kuwa aliendaa na kufanya presentation ya proposal ndio asimamie project la sivyo atanyang'anywa kazi.

Ilibidi muhindi anitafute tukae chini tena akiahidi offer kubwa kulinganisha na ya awali. Nilimkatalia na wakati huo huo nili apply kivyangu kwa makaburu wanipe project mimi kama mimi.

SIkuwa na kampuni yangu hivyo ile project ikahamishiwa kuwa in house project kumaanisha walianzisha kitengo maalum cha signage ndani ya kampuni yao kuanzia production mpaka installation na mimi nikapewa hicho kitengo kukisimamia. Hivyo badala ya Project Manager nikawa Division Manager.

Kwa ile phase ya kwanza ilimlazimu muhindi kumaliza na ilibidi areport kwangu moja kwa moja kwa niaba ya kaburu, karma is real.

Sehemu ya kazi iliyobaki iliisha kwa wakati na mpaka sasa kupitia hiyo project kitengo cha signage kwenye kampuni ya kaburu kimekuwa one of the leading signage companies kwa Tanzania.

Katika maisha chochote kinachopaswa kuwa chako kitakuwa chako tu haijalishi kitachelewa kwa kiasi gani.
Duuuh....hichi kisa kinanihusu kabisa... ila mi sikufanikisha kama wewe mkuu... Mimi nilifanya na Wakenya , tena ni mwaka jana tu miezi ya mwishoni... tulikorofishana sana , mimi ilikuwa issue ya malipo... daaaah...
Pole na hongera sana mkuu...
 
Hapana mkuu sio mimi...[emoji28][emoji28][emoji28]
Ndio wewe bana toka kule! 😂😂😂

Umepotea kwenye game mdogo wangu kwa kuendekeza mitungi na papuchi a.k.a mbususu za wanawake warembo... Nimenukuu maneno ya baba yako mlezi Mkubwa fella 😅👍🏾
 
Tatizo kubwa la wahindi ni kudharau uwezo wa kiakili wa watu weusi. Siku zote wanaamini mtu mweusi ni wa kuburuzwa. Hata ikitokea akakubali ufanisi wako atahakikisha anamuweka muhindi mwenzie karibu ili achukue ujuzi wako na mwisho wa siku akutimue pale anapokosa haja na wewe.
Upo sahihi kabisa mkuu! Ni watu wa hovyo sana linapokuja suala la kukubali utendaji mzuri wa mtu mweusi.
 
Habari za muda huu wapendwa

Bila shaka kwenye safari ya maisha kila mmoja wetu amewahi kukumbana na visa na mikasa mbali mbali kwenye purukushani za maisha

Mikasa ambayo imekuwa ikitupa mafunzo na mafundisho maishani mwetu na wakati huo huo kubadilisha kabisa mitazamo ya maisha yetu juu ya watu.

Watu wetu wa karibu ni watu tunaowategemea kwenye maisha yetu Kwa mambo mbali mbali lakini pia watu hao hugeuka na kutuletea vilio vya kudumu vyenye machungu maishani mwetu.

Je umewahi kufanyiwa mkasa, kisa au tukio Gani baya na ndugu au mtu wako wa karibu?

Mimi niliwahi kuchomewa utambi kazini na mtu wangu wa karibu...ambaye nilikuwa na share mambo yangu kibao na hata niliwahi kumpa mtaji wa biashara, lakini kumbe alikuwa anachukia mafanikio yangu tangia hapo nikabadilisha kabisa mtazamo wangu juu ya marafiki na watu wangu wa karibu. Kwa kifupi nikawa na chujio mdomoni mwangu na kichwani mwangu.
Jina langu linatosha kukueleza nini ndugu walinifanyia kwa mujibu wa Biblia Takatifu. Kumbuka tu Kaini alimuua ndugu yake Abel kutokana na wivu. Sadaka ya Abel ilikubalika na ya Kaini ikakataliwa. Kwa ufupi maisha kwangu yamekuwa ya misukosuko kutoka kwa ndugu wa karibu.
 
Kuna jamaaa mmoja alifukuzwa geto sekondari na wenzake hakua na msosi Wala Kodi ya nyumban mm niko kidato Cha pili yeye Cha tatu, nikamulea Hadi akamaliza shulen vizuri, siku ya mwisho nikamuomba aniachie vitabu akaomba hela, nikawa Sina, akapata kazi baadae Mambo mazuri nikwa na mm namishe kidogo nikamwambia nipo hapa Arusha vipi nikuone ndugu tusalimiane hajkujibu chochote. Akabadilishwa kituo Cha Kaz akaja mkoa nilipo akaletwa anatafuta nyumban ya kupanga kabla ya salamu akaniomba msamaha.
Daahhh .. aseehhhh enhee what was your response?!!!
 
Iv hizi issue za kutesana kwa kukaa aakwa ndg ziko kweli?
Nimekua ndg wanasomea kwetu(ndg wa upande wa mama) sikuwan ona shida yoyote wamepata
Sisi wenyewe tumesomea kwa ndg baba wadogo hapa dar hatujawah pappta shida yoyote
Now kwangu ndg wamepita kibao wengine kusoma na wengine wanakuja mjini kutafuta mishe ya kufanya sijawah ona shida sometime nakaaga na watu siwajui but amna shida
Najiuliza iv unamtesaje mtu? Kama hutak kukaa nae si umwondoe tu ? Na unapomtesa mtu iv kesho yako unaijua kweli?
Baba mdogo aliwah tuambiwa wakat huo tunakaa kwake vijana kama 7 iv wite tunasoma " ukipokea wagen ndani kwako hutakaa upungukiwe chakula kamwe" huu msemo haujawah toka kichwan na niwe mkweli sometime nakaaaga na watu kwangu na hali inakuwa haiko poa biashara haziend but hatujawah kupungukiwa chakula ndani kamwe.
 
Nilijitoa sana hasa kwenye kusaidia ndugu mfano kwenye sherehe zao nilitoa mpaka laki 3 kama mchngo ,cha ajabu siku naoa mimi hakuna aliyetoa hata mia zaidi ya mama aliyetoa akiba yake yote .

Wengine hata kufika hawakufika...
Weka hii kwenye akili yako "usichangie watu ukifikiri na wewe ukitaka kuoa utachangiwa"
 
Nilijitoa sana hasa kwenye kusaidia ndugu mfano kwenye sherehe zao nilitoa mpaka laki 3 kama mchngo ,cha ajabu siku naoa mimi hakuna aliyetoa hata mia zaidi ya mama aliyetoa akiba yake yote .

Wengine hata kufika hawakufika...
Mkuu kweli ukakubali maza atoe akiba yote Kisa shehere ?
 
Ndugu yangu wa mbali kaja mjini kakaa kwangu miezi 2. Cha ajabu alivyoondoka kaenda kunianika kijijini kuwa tunakula wali maharage Kila siku jioni....na Dagaa kabichi mchana na kwamba wife atakua mchoyo!
Aisee
 
Nilishawahi kuajiriwa na muhindi mmoja kama project manager. Ali apply tender iliyohusisha kuweka signage (mabango) nchi nzima kutoka kampuni moja maarufu ya Makaburu (South Africans). Kipindi hicho ilikuwa project yenye thamani ya kama $100,000.

Kabla ya kupata tender kulikuwa na bidding ambapo moja ya sharti ilikuwa ni kuwakilisha installation plan (proposal) iliyohusisha uchambuzi wa matumizi ya budget, utekelazaji wa kazi mpaka kukamilika kwake.

Nilifanya kazi ya kuandaa plan wiki 2 nzima usiku na mchana maana ilikuwa inahitajika haraka. Ilipotimia na kuwakilishwa muhindi akashinda tender.

Ilipoidhinishwa tu kuwa kashinda jamaa akaniambia kuna muhindi mwenzie toka India (expatriate) atasimamia hiyo project (kutumia plan yangu), moja ya makubaliano yetu ya awali ilikuwa nitaisimamia mimi hiyo project yote endapo proposal yangu itapita.

Aliposema mambo ya expatriate tu nikatoa notice yangu ya mwezi mmoja ya kuacha kazi.

Kipindi nataarisha plan ya hiyo project nilifanya research ya kutosha nikijua nitasimamia mimi mwenyewe hivyo niliweza kuhalalisha baadhi ya matumizi ya budget nikijua nitafanikisha vipi baada ya research yangu.

Phase ya kwanza ya project ilianzia mikoa ya Tanga, Arusha na Moshi. Muhindi alipopewa mzigo installation ianze akachemka baada ya kumaliza Tanga tu. Pesa ilikata na kazi hata robo haijaisha.
Kila sehemu ilikuwa na time limit kama ilivyoanishwa kwenye proposal plan, muhindi alichemka phase ya kwanza tu huku ikiwa keshachukuwa advance ya Mkaburu.

Nilifanya presentation mimi mwenyewe kwenye bidding kwa niaba ya muhindi, hivyo sharti aliliopewa na makaburu ni kuwa aliendaa na kufanya presentation ya proposal ndio asimamie project la sivyo atanyang'anywa kazi.

Ilibidi muhindi anitafute tukae chini tena akiahidi offer kubwa kulinganisha na ya awali. Nilimkatalia na wakati huo huo nili apply kivyangu kwa makaburu wanipe project mimi kama mimi.

SIkuwa na kampuni yangu hivyo ile project ikahamishiwa kuwa in house project kumaanisha walianzisha kitengo maalum cha signage ndani ya kampuni yao kuanzia production mpaka installation na mimi nikapewa hicho kitengo kukisimamia. Hivyo badala ya Project Manager nikawa Division Manager.

Kwa ile phase ya kwanza ilimlazimu muhindi kumaliza na ilibidi areport kwangu moja kwa moja kwa niaba ya kaburu, karma is real.

Sehemu ya kazi iliyobaki iliisha kwa wakati na mpaka sasa kupitia hiyo project kitengo cha signage kwenye kampuni ya kaburu kimekuwa one of the leading signage companies kwa Tanzania.

Katika maisha chochote kinachopaswa kuwa chako kitakuwa chako tu haijalishi kitachelewa kwa kiasi gani.
[emoji1545][emoji1545]
 
Back
Top Bottom