ELFU 25000 YANGUUU [emoji26][emoji25][emoji25]
Kipindi cha 2009 nilikuwa town nazungukaa mara wakapita wa mama wawili nilikuwa nimejisogeza mahali nakulaa yale matunda ya mchanganyiko ya buku. Maana jua lililuwa kalii
Basi nilivyo waona wanapita wame beba ma t shrt makalii sana kiukwelii.. Kwa nilivyo kuwa nawa angaliaa wakajua kabisaa nime yapenda yani kiukweli nilivutiwa nayoo.
Tukaongea beii ma 3 ikanitoka 25000 nikaona sawa tu haina shida nikaweka kwenye mfuko huyoo ghetto.
Nilivyo fika sijauliza nikawaonyesha majaama wakasema hapa kwelii umechagua basi nika weka kwenye ndo nikaloweka nikaja kufua baadaeee jioni sana mda umeenda.
Sasa majanga ni hapa. Natoka nje ile saa 5 sioni t shirt ikabidi niulizee manzii mmoja hivi akasema hajaona hata yeye. basi nikarudi ndani nika waambia jamaa zangu kuwa wameiba zile nguoo.
Jamaa akasema haiwezekani hapa hamna historia ya wizi na yeye akatoka nje akaangalia akaona kuna t shirt 3 akasema muulize mwenye hizi hapa atakuwa kachanganya.
T shirt moja ilikuwa ya damu ya mzee
T shirt nyingine ya kijani ile dark green
T shirt nyingine ya black
Nikasema ngoja niangalie mwenye nazoo hizi,
Sasa kuna kijana ana husika na ishu za ngombe ni kama house boy wa yule mama mwenye nyumba.
Nikamfuata na kumuuliza kuwa mbona umechukua nguo zangu. Akasema hapana yeye alifua juzii.
Kurudi dhaaaa bwana weee kumbe zanguuu yanii zime paukaaa rangi imetoka sijuiiii ziko kama za 1456 .
Yani kama kijani ndo imekuwa kijuvuuu.
Nikamuita jamaa nikamwambia akasema !!!
MR. MJINI SHULE. Akasema kunywa chai usije ukaanza kutapatapa hapa.
Kumbe hii tabia ipo town wamama wale wa mtumba wanamwagia maji nguo zinakuwa kama mbichii rangi inakuwa,imekolea.
Yanii zile nguo niliacha hapo hapo. SITA 4 GET KWA KWELI.
Sent using
Jamii Forums mobile app