Ni Kosa gani la ovyo ulilowahi kufanya tangu uanze kuendesha gari?

Matuta ya Shekilango Road ni makubwa kama ugomvi.
 
Aiseeee pole mkuuu.

Hii ilikuwa ni risk sana.

Shukuru huyo mwenye Nissan naye hakuhama maana mngevaana uso kwa uso.

Ni DashCam gani hiyo unatumia?
Shukrani sana aisee..

Yaani hizo sekunde kadhaa akili inawaza alternatives kibao.. Uzuri dereva wa dalalada wengi ni wazoefu kwenye hatari..!

Aisee hiyo ni simu..!
 

Una uzoefu wa kuendesha gari barabara za kwenda mkoa kwa muda gani?

Maana ninachokiona hapa ni ukosefu wa uzoefu, sehemu ipo plain hivyo dereva mzoefu hawezi fanya kosa ulilofanya...
 
Una uzoefu wa kuendesha gari barabara za kwenda mkoa kwa muda gani?

Maana ninachokiona hapa ni ukosefu wa uzoefu, sehemu ipo plain hivyo dereva mzoefu hawezi fanya kosa ulilofanya...
Muda mrefu..

Ndio maana inaitwa kosa.. Sababu dereva ni mzoefu..
Kwa learner isingekuwa kosa.. Anajifunza..!
 
Mkuu pole sanaa
 
Mimi nafikiria kuchomekea kipisicha nondo chini ya gas pedal ili nisivuke 80, au kuna njia nyingine? au nibandike karatasi "speed kills" kwenye usukani.
Maana unajisahau unakuwa rough mpaka unajishangaaa.
 
Mbona ndo njia yangu daily....hilo tuta mbona sijakumbana nalo[emoji849][emoji848]
 
Mmeanza jf wote mna magari mfyuuuu[emoji57][emoji57]
Kwahiyo wote wanaochangia mada jukwaa la siasaeni wanasiasa.
Jukwaa la afya wote Ni madaktari kule.

Mada hapa Ni kwa wenye magari au ww Ni dereva wa gari lolote iwe kwa kuajiriwa,uliazima ukaendesha na ulishafanya kosa la kijinga barabarani. Unataka kutuambia memba wote was jf wamekomenti hapa.

Jione we huna gari, Ila wengine wanayo.

Km vile una kawivu flani ivi.

Furaha yako Ni kuona watu hawachangii chochote basi ufurahi kwamba watu hawana magari.

Una mawazo ya kimaskinie.
 
Hehehehe[emoji23][emoji23][emoji23] Sawa mkuu
 
Ebana mimi siku moja nikiwa fuel station si nikakosea njia ya kutokea bana , nika pita katikati ya zile pipe /mashine zile za kiwekea mafuta.

Eh bwana eh kitu kikachubuka chubuka japo body haiku bonyea bonyea.
Mi bhana siku niko speed na v8 mara ghafla nikapishana na lori si ikabidi mimi mle ndani nikwepeshe kichwa (kama nakwepa ngumi)nikajikuta porini tyre zinazunguka hewani zote
 
matukio ni mengi ila hili ni mojawapo
gari ilikuwa imetoka kubadilishwa shockup pamoja na steering rack sasa haikufanyiwa wheel alignment kwa hy ukiwa sehemu barabara imenyooka ilikuwa ina vuta kushoto
sasa si nikajifanya mtabe nikaendelea kuliendesha gari hivo hivo pasipo kulifanyia wheel alignment kwa kipindi kirefu

sasa siku moja natoka tazara nataka nielekee buza kwa kupitia sokota kukatizia nuruyakini msikitini to mwembeyanga
nikiwa mwembeyanga nilijisahau kuna MTU alikuwa ananipigia simu sikupokea hadi simu ikakata sasa nikasema ngoja niachie sterling nichukue simu niangalie aliyenipigia na simu ilikuwa kwenye siti ya nyuma dah ilikuwa kosa nilishtuka kwa tairi ya gari ya mbele upande wa kushoto kupasuka baada ya gari kugonga mikokoteni pamoja na pikipiki mbili zilizokuwa mbele kwa kweli siwezi kusahau

hapo ndo nilipojua kuwa kumbe hii slogan ni ya muhimu
Driving + Phone= Accident
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…