Kwani wakiwa depo hawafundishwi mambo ya timing? kama unajua kuna mambo ya timing kwanini askari anawageuzia mgongo watazamaji kwenye mpira?
Nilipokuwa JKT niliambiwa kuwa kwenye lindo usikae sehemu ya wazi pande zote nne ili uwe makini na upande wa mbele tu, yaani nyuma yako lazima kuwe na kizuizi kama ukuta, mwamba, nk ili adui asitokee nyuma yako. Kama hakuna ukuta basi angalia zaidi sehemu yenye hatari zaidi. Usivute sigara usiku kwenye lindo ili adui asifahamu ulipo, usiwashe taa yoyote ulipo, walinzi msikae wote sehemu moja, msiangalie wote upande mmoja. Haya yote yalikuwa mafunzo ya kujaribu kupunguza hiyo timing yako unayohubiri.