Ni kwanini bado Waarabu wanatubagua, hata Mwafrika anapokuwa Muislam wanamkatalia kumuoa binti yao?

Leo hii nchi ya arabs anaweza tokea mtu mweusi kuwa miss, Morocco tu hio walikuwa wanaongea ubaguzi tu kombe la dunia, akili hamna ndio maana mzungu anawabonda huko middle East.
Hivi kuna Cheo kikubwa kwenye Nchi kushinda Kiongozi wa Nchi Raisi, Sultani, Emir etc?

Kama kuna Maprince, Masultan na viongozi wengine wenye Asili yq Africa kwenye Hizo nchi kuna Cheo gani kinapita Hivyo.

Sheikh saad aliekua Amir wa Kuwait


Qaboos Sultan wa Oman aliefariki Karibuni
 
Waislam tuna vigezo vya Kiislam vya kuoana.

Huo ubaguzi unaosema wewe haupo kwenye Uislam, umeshindwa kuuelewa tu Uislam.
 
Sisi ni wabaguzi kuliko hata hao tunaowalaumu.

Ngoja nisimulie hiki kisa Kwa kifupi

Siku moja nikiwa mapumziko nilikutana na mtoto wa kiarabu kwenye restaurant moja mjini, alikua na rafiki yake mweusi.

Nilipiga nae story mbili tatu then nikaomba contact, Mtoto akadai simu yake kaiacha chini kwenye gari but akamuomba rafikie ( mweusi) achukue contact yangu ili baadae anitafute.

Cha kushangaza mweusi alitaka kuzingua kuchukua contact yangu [emoji3][emoji3] hata sijui alinichukulia vipi!
Mwarabu akarudia tena .....hey I say take his contacts plz!!!!

Ndo akawa ameichukua .

Mwarabu alinitafuta usiku na tukawa vizuri mpaka Leo.

Kwa hiyo ubaguzi tunao sisi wenyewe kabla ya kuwanyooshea vidole wengine.
 
Ndio iko hivyo, tit for tat,
Sio unabaguliwa unalia, ukibaguliwa na wewe bagua maisha yanaenda mbele.
Fact. Ubaguzi ni kitu cha kawaida tu watu wanakipa airtime. Mimi nilibaguliwa sana nilivyobahatika kwenda nje wala nikawa sitilii maanani mpaka jamaa wakaacha kunibagua tukawa tunabonga fresh. Yaani nilikua siumii kabisaaaa mradi yangu yanaenda.
 
Una chuki nao kisa hawana elimu lakini wamekupita maendeleo!! Hao wasiokua na elimu si ndio dada zako wamejazana huko kufanya kazi za ndani? Wasiokua na elimu ndio wanakuja kuwekeza kwenye bandari yenu,

Je na sisi tupo kundi gani???
Kuwekeza kwenye bandari sio kwamba wanakuja kutusaidia bali na wao wanataka kunufaika ndio maana wanajipendekeza kuweka picha ya SSH kwenye mnara pale Dubai, kwani wawekezaji ni wao pekee?

Hata arabs wamejazana sana Africa na wameajiriwa na kampuni za weusi, tena hao ndio wengi kuliko I dians, Chinese na wazungu, wamepanga huku mtaani tunaishi nao, ila mwafrika akienda kule wanampiga nyundo kichwani, kuwatesa nakuwaua, wanaona mtu mweusi ni mnyama, elimu hawana.
 
Msikiti gani na uko sehemu gani?
 
Waache waendelee kukalia majungu, umbea na malalamishi mtandaoni huku wanaume wenzao wakitafuta namna ya kutawala dunia.

Ukiona wanalia lia ooh TunABaGuliWa ujue wamekosa namna ya kutembea na wanawake hao hakuna sababu nyingine ya msingi.

(Ila siungi mkono mambo ya Dp World)
 
Hao ni arabs weusi wapo wengi tu, nenda ka google tena.
 
Wapi wanapokupenda we mtu mweusi? Mbona Roma ipo Italy na Italy inaongoza kwa ubaguzi hata kwa wakristo wenzao? wachezaji weusi kibao wanabaguliwa kina lukaku wakigusa mpira wanashangiliwa kwa sauti za nyani , huko spain kina Dani alves 2013 wametupiwa ndizi uwanjani, Juzi tu Vinicius Jr wa R.madrid alikua anapigiwa sauti za kinyani akiwa uwanjani, mifano ya ubaguzi ipo wazi sana kina Mario Balloteli ni mu Italy ila kwenye Mechi ya Verona akiwa anaenda kupiga kona Akawa anapigiwa milio ya nyani na waitaly wenzake had akasusa akatoka uwanjani

Au huo siyo ubaguzi? ubaguzi ni kukataliwa kuoa tu?
 
Hata hao waarabu wa Tinde na Bukene,wanaolewa na weusi wenye mawe tu.

Na huo uzao chotara hupitia changamoto ya ubaguzi ukijumuika kwenye shughuli za ukoo wao kule ujombani.
 
Hata hao waarabu wa Tinde na Bukene,wanaolewa na weusi wenye mawe tu.

Na huo uzao chotara hupitia changamoto ya ubaguzi ukijumuika kwenye shughuli za ukoo wao kule ujombani.
Mila na desturi zako tofauti. Waarabu waliopoTanzania wengi wao, mila na desturi zao ni Uislam na katika Uislam kuna vigezo vyake vya kuoana.

Ukiona umekataliwa basi elewa kuwa hivyo vigezo hujakidhi. Ulie tu.
 
Hakika [emoji106]

Kuhusu DP World unawachukuliaje?!!!!! [emoji23]

#MamaAnaupigaMwingii[emoji7]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Mila na desturi zako tofauti. Waarabu waliopoTanzania wengi wao, mila na desturi zao ni Uislam na katika Uislam kuna vigezo vyake vya kuoana.

Ukiona umekataliwa basi elewa kuwa hivyo vigezo hujakidhi. Ulie tu.
Ubaguzi tu, hamna cha vigezo, usisingizie uislamu.
 
Wangekua hawana elimu wasingekuja kuwekeza kwenye bandari na mbuga zenu, ni aibu kwa mtu anayejiona ana elimu kutawaliwa na asiye na elimu tangu karne ya 9 huko hadi leo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…