KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,181
- 17,187
Akheri ungesema "mleta mada kakariri kwamba 'Mwanza ni kanda'", ambayo sio kweli. Mimi naona yeye na wewe hamtofautiani sana kwa mitazamo yenu.Wanachosahau kingine ni kwamba wasukuma wana mikoa mitano, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Tabora na Geita, ni kabila kubwa kuliko makabila yote, mleta mada kakariri kwamba wasukuma wanatoka Mwanza peke yake.
Ni sheria gani inayosema maadhimisho lazima yawe Dar au Dom,?Huku kukiwa na lundo la tuhuma kuwa utawala wa awamu ya tano umegubikwa na ubaguzi wa kikanda hatimaye Rais John Pombe Magufuli atakuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 58 ya uhuru wa Tanganyika. Sherehe hizo kwa mara ya kwanza zinafanyika nje ya makao makuu ya nchi ukiachilia mbali serikali ilipohamia Dodoma.
Swali la msingi ni kwanini sherehe hizo ziende jijini Mwaanza eneo ambalo limetawaliwa na kabila atokalo Rais Magufuli? Ni hoja gani hasa iliyotumika kuzipeleka jijini humo?
Ni jambo la ajabu kuona serikali ikikumbatia waziwazi upendeleo wa ukanda! Haya yanayofanywa yanatupa sisi ari ya kujiridhisha kuwa tumetawaliwa na upendeleo wa waziwazi wa kikabila awamu hii ya uongozi.
Kwa maana hiyo sasa jeshi, viongozi wote wa juu pamoja na wageni wanapelekwa Mwanza ili kuhudhuria sherehe za uhuru.
Siwezi kusema mengine yaliyotokea huko nyuma katika utawala huu yakionyesha mwenendo mbaya wa kikabila ila kiukweli jambo hili halileti picha nzuri hata kidogo.
Hii ni Tanzania imejengwa ila kiobomoa ni kazi rahisi sana.
labda tuulize kwani hii ni mara ya ngapi kufanyika Mwanza?Mbona mimi sioni tatizo maana Mwanza sio mji wa Wasukuma peke yao humu sasa hivi kuna makabila ya kila mkoa wa Tz kama huamini waulize waha
Huwa nalisikia tu hilo la Mwalimu "Nyerere kuonya" juu ya makabila fulani...lakini sijawahi kuona ushahidi wa maandishi au hotuba juu ya hilo.Sina shida na watu wa kabila lile mkuu. Mbona hata wapinzani wakienda kule wanapokewa vizuri tu? Nina shida na huyo aliyepeleka sherehe huko! In fact anafanya wasukuma wenzake waanze kufikiriwa tofauti ingawa najua wapo wasiopendezwa na haya. Nakupa mfano wachaga, wahaya, wanyakyusa na wasukuma Nyerere aliwahi kutuonya kuwa wametawaliwa na ubinafsi. Sasa hatukuwahi kumpata Rais kwenye makabila hayo hapo kabla ila sasa tumempata Magufuli na ameenda mulemule alikoonya Nyerere. Hii inajenga taswira kwamba tumeshakanyaga nyoka sasa siku tukiona jani tushtuke! Kusema kweli hapo kabla sikutegemea kuona haya ninayoyaona. Mpaka huwa najiuliza hivi kuna watu huwa hawaoni aibu?
Tangu aingie madarakani hii ni Mara ya ngapi unafanyika Mwanza? Chutama mkuu. Chuki hazitakusaidia Sana.Hamuwezi kuelewa ila mwenyekiti wenu ni mtu anayetukuza ukanda kwenye mambo ya kitaifa.
Sawa, naomba unipe sababu kuu ya Magufuli kupeleka sherehe za Uhuru Mwanza. Tafadhali epuka maneno ya "Tumeamua iwe sasa ni mzunguko" Maana nitakuuliza "Ni kwanini kwa mara ya kwanza tuanzie nyumbani kwa kabila la Rais?" Najua kutokuwa na jibu hivyo yaepuke maneno hayo!Huwa nalisikia tu hilo la Mwalimu "Nyerere kuonya" juu ya makabila fulani...lakini sijawahi kuona ushahidi wa maandishi au hotuba juu ya hilo.
Sikatai, inawezekana alifanya hivyo kwa sababu alizoziona yeye kwa wakati huo.
Lakini sikubaliani na dhana ya kulishikia hilo onyo, liwe kama ni jadi isiyoweza kubadilika. Tulipokuwa tumekwishafikia kama taifa wakati Mwalimu Nyerere anatuaga, ni dhahiri tulikuwa tumepiga hatua kubwa ya kutosha ya kuendelea kukumbatia dhana ya ukabila kuturudisha nyuma, na hivyo itulazimu kuendelea kushikilia 'onyo' alilotoa Mwalimu wakati ule.
Kazi pekee tuliyokuwa tumebakiwa nayo kuifanya ni kuchambua kwa makini mTanzania yeyote anayejitokeza kuwa kiongozi wetu bila ya kujali kabila analotoka.
Sisi kazi hiyo imetushinda, na matokeo yake ndio haya tunayoyaona sasa.
Ina maana jamaa ndio hivyo kaanza kampeni za 2020, au sio? Tena kampeni za kikabila!Nimekuelewa Sana mtoa uzi nami niliposikia kwamba sherehe za Uhuru zitafanyika mwanza kwenye uwanja wa CCM kirumba nikajua tayari Jiwe kaendeleza ukanda na ukabila wake,leo Nyerere road yote nyeupee peee Machinga wote wameondolewa
Mkuu G Sam, swali lako mbona ni rahisi sana kulijibu? In fact tokea mwanzo wa mada hii nimekuwa nikikupa dokezo juu ya swali lako, labda hupendi tu kunielewa ninachoandika.Sawa, naomba unipe sababu kuu ya Magufuli kupeleka sherehe za Uhuru Mwanza. Tafadhali epuka maneno ya "Tumeamua iwe sasa ni mzunguko" Maana nitakuuliza "Ni kwanini kwa mara ya kwanza tuanzie nyumbani kwa kabila la Rais?" Najua kutokuwa na jibu hivyo yaepuke maneno hayo!
Dar haiwezi kufa vitakufa hivyo vimji viso uhaiMara nyingine Magufuli mnamuonea bure. Mnafahamu fika Chato ilikuwa Kagera, Kagera wana jadi yao na Mwanza jadi yao iweje leo eti Magufuli anatoka kabila la Mwanza? Hata kama bado hajavuka mipaka ya nchi.
Halafu watu wa Dar es Salaam na Arusha nimegundua hampendi maendeleo yapelekwe sehemu nyingine za nchi. Ningelikuwa Magufuli kwanza Dar es Salaam ningeifuta kwenye ramani ya taifa hili maana ndio chanzo cha umaskini sehemu nyingine za taifa hili.
Kama mnaona ukanda basi peleka mswada bungeni tuwe na states ambazo zitasimama Kama Kanda uione mtavyoburuzwa.
Watu wa ajabu sana nyie.
Muulize...Hivi Mkapa alishindwa kufanya haya huko Mtwara tena eneo hasa lololotumika kwa ukombozi?
Dar haiwezi kufa vitakufa hivyo vimji viso uhai
Ubaguzi hautatuacha salama! Kwani kuna shida gani kufanyikia Mwanza?Huku kukiwa na lundo la tuhuma kuwa utawala wa awamu ya tano umegubikwa na ubaguzi wa kikanda hatimaye Rais John Pombe Magufuli atakuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 58 ya uhuru wa Tanganyika. Sherehe hizo kwa mara ya kwanza zinafanyika nje ya makao makuu ya nchi ukiachilia mbali serikali ilipohamia Dodoma.
Swali la msingi ni kwanini sherehe hizo ziende jijini Mwaanza eneo ambalo limetawaliwa na kabila atokalo Rais Magufuli? Ni hoja gani hasa iliyotumika kuzipeleka jijini humo?
Ni jambo la ajabu kuona serikali ikikumbatia waziwazi upendeleo wa ukanda! Haya yanayofanywa yanatupa sisi ari ya kujiridhisha kuwa tumetawaliwa na upendeleo wa waziwazi wa kikabila awamu hii ya uongozi.
Kwa maana hiyo sasa jeshi, viongozi wote wa juu pamoja na wageni wanapelekwa Mwanza ili kuhudhuria sherehe za uhuru.
Siwezi kusema mengine yaliyotokea huko nyuma katika utawala huu yakionyesha mwenendo mbaya wa kikabila ila kiukweli jambo hili halileti picha nzuri hata kidogo.
Hii ni Tanzania imejengwa ila kiobomoa ni kazi rahisi sana.
Tatizo watu wamekaa kuona nini kinafanyika waje kulalamika hapa, mada haina mashiko yoyote zaidi ya chuki na roho mbaya tuHakuna hoja hapa na tafadhali leteni mada zenye mashiko na manufaa kwa nchi ili tujadili na kueleweshana.
Naona akili yako iko na tope kidogo.Mara nyingine Magufuli mnamuonea bure. Mnafahamu fika Chato ilikuwa Kagera, Kagera wana jadi yao na Mwanza jadi yao iweje leo eti Magufuli anatoka kabila la Mwanza? Hata kama bado hajavuka mipaka ya nchi.
Halafu watu wa Dar es Salaam na Arusha nimegundua hampendi maendeleo yapelekwe sehemu nyingine za nchi. Ningelikuwa Magufuli kwanza Dar es Salaam ningeifuta kwenye ramani ya taifa hili maana ndio chanzo cha umaskini sehemu nyingine za taifa hili.
Kama mnaona ukanda basi peleka mswada bungeni tuwe na states ambazo zitasimama Kama Kanda uione mtavyoburuzwa.
Watu wa ajabu sana nyie.
Kila mtu ana mara yake ya kwanza ya kuanzia kitu iwe kuoa, kwenda shule, kunywa. .., kuvuta, kula chakula cha aina fulani n.k , wazazi au watu waliojirani na wewe wanaweza kufrahia jambo hilo au kuchukizwa, sasa kama wewe umechukizwa usipande chukizo lako kwa watu waliopendezwa na hiloKwahiyo mzunguko uanze 2019 tens nyumbani kwa Rais..Haya bwana! Ninachojua ni kuwa ameenda kubembeleza kura za wasukuma kama kawaida yake maana sherehe zijazo tutakuwa tumemaliza uchaguzi mkuu.
Kumbe chato ni kwa wahaya sio wasukuma ....Mara nyingine Magufuli mnamuonea bure. Mnafahamu fika Chato ilikuwa Kagera, Kagera wana jadi yao na Mwanza jadi yao iweje leo eti Magufuli anatoka kabila la Mwanza? Hata kama bado hajavuka mipaka ya nchi.