Ni kwanini sasa miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika iadhimishiwe jijini Mwanza?

Hivi huwa kuna ushahidi wowowte kuonyesha Nyerere aliwahi kuayasema makabila hayo au Uvumi tu nishatafuta andiko sauti video sijawahi ila alionya kuhusu ukabila lakini sikuwahi ona akiyatamka bayana na kama angaliesema basi angeliwataja wasukuma kwa sababu walitaka sukumaland federation iendelee na pengine leo tungekuwa na nchi kama Lesotho na yeye akaona mbali ndiyo chanzo cha uchifu kufutwa au kutokuwa sehemu ya serikali
 
Akheri ungesema "mleta mada kakariri kwamba 'Mwanza ni kanda'", ambayo sio kweli. Mimi naona yeye na wewe hamtofautiani sana kwa mitazamo yenu.
Tofauti ni kubwa. Mleta mada hajaelewa kwamba maandishi ni sawa na maneno yatokayo mdomoni, siku zote huumba.

Mauaji ya Rwanda yalianza na maneno ya watangazaji wa radio.
 
Sio wote mkuu
 
Mtu wa ajabu sana ni wewe. Eti ningekuwa Rais Dar es Salaam naifuta, unaifutaje kwa mfano?
Maandazi kweli!
 
Ni dhahiri siasa zetu ni za kinafiki na ulaghai mkubwa. Tunasema ni awamu ya kutumia vizuri pesa za umma lakini kuna matumizi ya ovyo ya pesa za umma katika mambo mengi ya hovyo.

Kutokana na kuamua kufanyia sherehe za uhuru jijini Mwanza, mwezi mzima malori ya jeshi yamekuwa barabarani na makonteina kwenda Mwanza kwaajili ya kupeleka zana za maonesho siku ya maadhimisho ya sherehe.

Hivi kulikuwa na ulazima huo?
 
Hii hoja hapana, nadhani mleta mada kama kuna kitu tofauti tuambie, vinginevyo acha ifanyike popote hii ni sherehe kama zingine.
Siku zote, hata katika mataifa mengine sherehe kama hii hufanyika makao makuu ya nchi. Unatakiwa kufahamu hilo. Hii ndiyo sababu hakuna kipindi chochote cha utawala wa Marais wengine, sherehe hizi ziliwahi kupelekwa mahali pengine popote zaidi ya mahali yalipo makao makuu ya serikali. Au sasa hizi makao makuu yapo Mwanza?
 
Ni sheria ipi iliyovunjwa mkuu. Hayo ni maadhimisho tu mkuu, na sio sherehe halisi za Uhuru wa Tanganyika. Kumbuka hatupo mwaka 1961 , huu ni waka 2019. Ukitaka hata Moshi kule Marangu inaweza fanyika alimradi ni sehemu ya Jamhuri.
Siyo kila kitu kinaongozwa na sheria. Kuna mambo mengi tu yanafanyika hakuna sheria. Kunapokuwa hakuna sheria ya moha kwa moja kuelekeza jambo fulani, hekima, busara, utamaduni na mazoea huzingatiwa.
 
mkuu sherehe za uhuru kufanyika Mwanza imekuwa nongwa? nlidhani Magu anahitaji pongezi kwa kuondoa mazoea ya sherehe hiyo kufanyika sehemu moja tu mwakani Iringa au Mbeya au Tanga au Kigoma nk
Unaelewa gharama zinazotumika kuhamisha sherehe kama hizo kufanyika eneo tofauti kila mwaka?
 
Wewe unayewaza kwa angle ya Kanda na Kabila ndo mkabila. Kwani Mwanza sio Tanzania.
Pia ni vema ukajua kuwa serikali haipo kwa ajili ya kukidhi matakwa ya Kikabila na Kikanda.

Huna hoja. Hebu nenda ukahangaike na uchaguzi wenu wa Kanda na utujuze matokeo.
 
Hamuwezi kuelewa ila mwenyekiti wenu ni mtu anayetukuza ukanda kwenye mambo ya kitaifa.
Kama kilivyo chama kinatukuza Ukabila na kuuvisha joho la Ukanda ili kuvicha ukweli.
 
Ngoja tumkumbushe mleta mada.
Mwaka 1979 mwalimu aliyapokea majeshi yetu yaliyotoka vitani Uganda katika vita ya kumuondoa nduli Idi Amini aliyekuwa ameivamia sehemu ya nchi yetu huko Kagera katika mji wa Mwanza.
Shughuli hii Ilikuwa ya kitaifa lakini haikufanyika makao makuu ya nchi kama mleta mada anavyotaka kutuaminisha.
 
Kwani Mwanza hawakupigania Uhuru kama Wachaga?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…