Ni kwanini unajenga nyumba ya ghorofa?

Ni kwanini unajenga nyumba ya ghorofa?

Hayana, maji meupe yapo fresh tu .... Mwasonga Dar es salaam zoo, maji uhai, uwanja wa Yanga mitaa ile unajichukulia kiwanja na kusubiri.
Huo ndiyo ujanja.
Buy land and wait .... Don't wait to buy land


Kutoka posta hadi hapo ni shi ngapi na na masaa mangapi?
Pia je vile vya kukatiana kwa ya chini kabisa vina range kwenye sh. ngapi
 
Kujenga gorofa labda apartment upangishe vinginevyo ni kusababisha ugomvi wakati ukifa na kila mmoja atataka gorofa lako.
Pili unapozeeka una sukari, pressure, moyo,mguu kwishney yaani utatesa tu watu kukubeba.
Jenga nyumba ya chini tu bana.
 
Kujenga gorofa labda apartment upangishe vinginevyo ni kusababisha ugomvi wakati ukifa na kila mmoja atataka gorofa lako.
Pili unapozeeka una sukari, pressure, moyo,mguu kwishney yaani utatesa tu watu kukubeba.
Jenga nyumba ya chini tu bana.
Kwani ghorofa haliwezi kues na vyumba vya chini?? Au ghorofa inaanzia juu moja kwa moja
 
viwanja huku AR ni 15M kwa kiwanja cha 20kwa 20, ni muhim kujenga kwenda juu ili ulinde pesa yako ila pia utie heshim mtaan kwenu
 
Miaka michache ijayo miji mikubwa kama DAR hakutakuwa na maeneo ya kujenga
 
Mie nimejenga ghorofa kwa kuwa niliweka nadhiri toka mtoto. Enzi hizo dingi alikuwa anatuchukua krismasi anatupeleka kwenye swimming pool pale Police Officers Mess Oysterbay, sasa nilivyokuwa naona mijengo maeneo ya kule nilijiwekea nadhiri nikipata hela lazima nijenge ghorofa.

Niliweka ki-balcony cha kunywea wine nje ya chumba changu juu toka nihamie sijawahi kukaa hapo zaidi ya kupasafisha tu mavi ya njiwa wa jirani ambao wamepageuza kama kijiwe chao
Kwanini sasa hukai hapo ( balcony) au umelogwa mwenzetu?
 
Back
Top Bottom