Ni kwanini unajenga nyumba ya ghorofa?

Ni kwanini unajenga nyumba ya ghorofa?

Kwa watu kadhaa waliokua wanajenga nimeona msingi range 45mil to 55. Na ni hizo hizo room 4 za kulala ukiacha store na vingine. Hapa naenda site ya ndugu yangu katumia 55.
Mkuu acha kutisha watu , inawezekana jamaa zako wanaibiwa na mafundi , msingi wa ghorofa ya vyumba vinne hauwezi kufika mil 45 , hata Kama ardhi ni ya kuhamisha.
 
Mkuu acha kutisha watu , inawezekana jamaa zako wanaibiwa na mafundi , msingi wa ghorofa ya vyumba vinne hauwezi kufika mil 45 , hata Kama ardhi ni ya kuhamisha.
Na aliyekuambia anainiwa na mafundi ni nani? Materials inayotumika baba.nothing more than that. Hivi kila kitu lazima gharama zifanane mkuu?
 
Sidhani kama upo serious.
Kanishangaza kweli jamaa. Na hapo anabisha ukute hana update yoyote ya kuhusu ghorofa wala hajawahi kujenga wala kumiliki wala kivyovyote. Sikuaga najua kama ni gharama hivi mpaka nilipokuja kushuhudia mwenyewe na si kwa mtu mmoja
 
Sawa,nasubiri tuwekane sawa.nahitaji maelezo ya slab ya kati tu.A-Z.
Kuhusu slab gharama zake ziko hivi

1.Zege 1m2=40,000/= (premix grade 20)
2.Formwork 1m2=25,000 (na milunda au unaweza Kodi steel plate)
3.Nondo za 1m2=15kg x 2,000=30,000/=
4. Kufunga formwork 1m2=5,000

Jumla ni 100,500 kwa mita 1 ya mraba

Wakati huo gharama za kupaua ziko hivi:-

Mabati ya Decra/Fortiza mita moja ya mraba Ni 100,000/=(pamoja na mbao)

Mabati migongo mipana (IT4&5) mita moja ya mraba ni 50,000(Pamoja na mbao)

Halafu gharama ya gypsum board kwa mita moja ya mraba Ni 20,000 (pamoja na mbao)

Hapo nimejaribu kukokotoa gharama zote kwa eneo la ukubwa wa mita moja ya mraba. Kama utahitaji ufafanuzi zaidi sehemu yoyote nijurishe, ili nikipata nafasi nikupe jibu.

Yote kwa yote narudia kusema kuwa, Ni Economical kujenga Ghorofa kuliko nyumba ya kawaida. Tofauti kubwa naiona kwenye ufundi tu.

Kwenye Nyumba ya kawaida unaweza okoteleza fundi yeyote hata kutoka nyumba ya 2 toka kwako (wa 10,000 kwa siku). Hajui hata maana ya mix ratio ya mortar na zege. Nyumba haina hata msingi wa zege chini.Matokeo yake nyumba nyingi za kitaa huchakaa kabisa kabla hata ya miaka 50.

Ghorofa lazima utumie professional fundi ambao Ni wachache saana. Na nyumba itakuwa imara zaidi na itadumu zaidi ya miaka 100.

Hata kwenye nyumba ya kawaida ukitumia professional fundi itakuwa imara zaidi na kudumu zaidi. Tazama majengo mengi ya serikali yalivyo imara
 
Sasa wewe hiyo inakushughulisha nini?

Wewe kula raha, life's too short
Aibu tunashindwa kuangaliana asubuhi maana nikikaa kwangu naona chumbani kwao direct. Wanajitahidi kufunga mapazia ila kuna kipindi kutokana na joto wanaacha wazi.

So kiustaarabu tu nimeamua kuipotezea balcony
 
Ghorofa raha bwana weee. Kuishi juu km ndege? Unakula upepo tu kwa siri yako. Na mmeo mzuri mzuri. Mbali na heshima ni raha sana isiyo kifani. pia hasa ziwe ghorofa 3 👙👙👙👙😆kwenda juu unaweza usiwe unakula lkn unanenepa tu.

hkn kelele huko juu!!! kushuka chini mara moja moja sana.

km kariakoo jamani ukiishi ghorifani utadhani uko shamba. kimyaaaa!!! hkn vumbi km zilivo gorofa za salasala! mpyutuu! angalia unaishi wapi.
 
Na aliyekuambia anainiwa na mafundi ni nani? Materials inayotumika baba.nothing more than that. Hivi kila kitu lazima gharama zifanane mkuu?
Ndo maana nikatumia terminology 'kutisha' najua materials zinatofautiana sana , uskishajiona unatumia extravagant material automatically unakosea mandate ya kuwa reflected sababu si kila mtu ana uwezo huo wako,
Msingi kwa mil 45 ghorofa ya vyumba vinne si ujenzi wa kawaida
Any way soda ya sh 500 kitaa unaweza kuuziwa 5000 hapa hapa mjini .
 
Mkuu hapa umeongopa. Gharama ya msingi wa ghorofa unaijua kweli? Yaan ule msingi ni nyumba kamili na chench inabaki tusiongopeane
Nimekuelezea kuna tofauti ndogo ya nyumba ya kawaida na nyumba ya ghorofa moja kama unajenga kupitia wataalamu utaona hizo tofauti ila kama unajenga kupitia mafundi wa mitaani huwezi kutambua tofauti.
Mtaalamu anakupigia hesabu ya kila nyumba ya kawaida na nyumba ya ghorofa ni vifaa gani vinatumika.
Sijagusia ghorofa mbili na kuendelea.
Nimezungumzia tofauti ndogo jaribu kusoma na kuelewa.
 
Mkuu kwaheri
 
Ghorofa raha bwana weee. Kuishi juu km ndege? Unakula upepo tu kwa siri yako. Na mmeo mzuri mzuri. Mbali na heshima ni raha sana isiyo kifani. pia hasa ziwe ghorofa 3 [emoji160][emoji160][emoji160][emoji160][emoji38]kwenda juu unaweza usiwe unakula lkn unanenepa tu.

hkn kelele huko juu!!! kushuka chini mara moja moja sana.

km kariakoo jamani ukiishi ghorifani utadhani uko shamba. kimyaaaa!!! hkn vumbi km zilivo gorofa za salasala! mpyutuu! angalia unaishi wapi.
Na ukitema mate yanaishia hewani[emoji23]
 
Ndo maana nikatumia terminology 'kutisha' najua materials zinatofautiana sana , uskishajiona unatumia extravagant material automatically unakosea mandate ya kuwa reflected sababu si kila mtu ana uwezo huo wako,
Msingi kwa mil 45 ghorofa ya vyumba vinne si ujenzi wa kawaida
Any way soda ya sh 500 kitaa unaweza kuuziwa 5000 hapa hapa mjini .
Sijamtisha mtu kwakua ndo uhalisia niliouona mkuu
 
Kama unafanya kazi mitaa ya Posta sikushauri uishi mitaa hii. Ni almost impossible.
Ila kama unataka kuhodhi ardhi, this area has all the trimmings of becoming a very vibrant and independent urban area.

Kwa kijana, ningekushauri ununue ardhi huku. Kuna ujenzi wa factories, sports complexes, Shule na vyuo, hotels na watu wengi wanashusha nyumba za maana huku ingawa ni early stages.

Ni 22 km from ferry/posts na Bei elekezi ni 5,000shs per sqm. Market price ni 10,000 mpaka 20,000 per sqm na karibu kote kuna town plan.
In early 2000s, 3mil ilinipa 35 acres...(Not to be bragging)
sawa mkuu...shukrani sana kwa ushauri na hongera kwa kuhodhi ardhi
 
Sidhani kama upo serious.
Mkuu tunaweza tukatofautiana kwenye exposure ya mambo flani flan ,Ila the best thing human can do ni kuwa tayari kujifunza any time , mil 45 msingi wa ghorofa sio ujenzi wa kawaida .
Moja ya mishe zangu zinaniweka karibu sana na vifaa vya ujenzi na wataalamu wake , gharama zake nazijua ,
Kuna mtu humu ni dr Kama sikosei hata kwenye uzi huu amechangia yeye alikuwa huru kutueleza ujenzi wake toka anaanza hadi anahamia kwenye ghorofa yake , japo lilikuwa halijaisha vizuri Ila alihamia akiwa amespend mil 64 .
 
Ndo maana nikatumia terminology 'kutisha' najua materials zinatofautiana sana , uskishajiona unatumia extravagant material automatically unakosea mandate ya kuwa reflected sababu si kila mtu ana uwezo huo wako,
Msingi kwa mil 45 ghorofa ya vyumba vinne si ujenzi wa kawaida
Any way soda ya sh 500 kitaa unaweza kuuziwa 5000 hapa hapa mjini .
Mie miwili iliyopita nilisimamia ujenzi wa jengo la ghorofa 1, liko Mwandege mkuranga. Ina vyumba vi4 na nguzo 11, Kama sikosei msingi haukuzidi 14,000,000 . Sasa huo msingi wa 45,000,000 Duh!!!!!!!, Anyway labda material yanatoka California
 
Watu wanatumia drewa nadhan badala ya mchanga figure zako zipo sahihi sana mkuu japo bado ni on the high side sababu naamini mkuranga material zote zinatoka mbali ukiacha mchanga.
 
Back
Top Bottom