Ni kweli hali ya maisha imekuwa ngumu, na pia ni kweli hizi tozo hazikubaliki, sasa wananchi tuseme kwa vitendo imetosha

Ni kweli hali ya maisha imekuwa ngumu, na pia ni kweli hizi tozo hazikubaliki, sasa wananchi tuseme kwa vitendo imetosha

Lissu anakula kuku ulaya, Mbowe keshalambishwa asali bila sisi wananchi kufanya maamuzi tutaendelea kudidimizwa.
Kungekuwa na wasanii wanajieldwa ningewaandikia script ya kuwaumbua Hawa wapuuzi
Wamechoka nao.
Alipgwa risasi akaumia nusura kufa hatukuandamana, mbowe akakaa ndani mali zake zikaharibiwa hatukuandamana.
Wakaona hivi kwanini tufie mazoba, wacha tuayaache
 
Mama anawanyoosha sukuma gang. Wamewekewa tozo tena! Magufuli alitutesa sana jamani.
 
Kabla ya kuandamana,tutumie njia ya mazungumzo na viongozi.
Kumbukeni hasara za maandamano zinaweza kuligharimu taifa letu;ikiwa ni pamoja na kuharibu miundombinu,mali za watu binafsi na hata kugharimu maisha.

After all:
SI TUNA WABUNGE AMBAO NI WAWAKILISHI WETU?.
Machawa akili zenu zipo kwenye makalio, wabunge hawa walioteuliwa na Magufuli na kupelekwa bungeni?

Wakati wanapitisha miswada ya kipumbavu bungeni hawakuwa wabunge hawa?
 
Kwahyo sasa tunaanzia wapi na tunaishia wapi hayo maandamano maana tunaumia sana tunajitahid kufanya kazi kea bidii lakini tunafanyia watu matumbo yao wao wamekaa tunaoteseka n sisi watu wa chini
 
Je, nani atamfunga paka kengele? 🚶‍♀️🚶‍♀️🚶‍♀️🚶‍♀️🚶‍♀️🚶‍♀️🚶‍♀️🚶‍♀️🚶‍♀️🚶‍♀️
 
''Wasamaria wema wamemuokota aliyegongwa na gari barabarani. Wakamkimbiza hospitali. Daktari anataka laki tatu kumtibu. Linaundwa group kuchangisha. Serikali inakata tozo badala ya kulipia matibabu ya raia wake''- Askofu Benson Bagonza
 
Hii nchi si sahihii kuleta mtoto labda mpaka hiki kizazi chetu kipite.

Kwa kuongeza, hata rambirambi zinazochangwa kupitia ma-group ya mitandaoni nazo zinatozwa tozo.
 
Tukatae tozo. Tukatae walamba asali.
 
utaratibu wa kutolewa control number ya malipo ya tiba unaweza kuondoa changamoto hiyo..badala ya kumtumia mtu fedha ya matibabu basi unailipa bill moja kwa moja iwe kwa simu au benki
 
Hii nchi si sahihii kuleta mtoto labda mpaka hiki kizazi chetu kipite.

Kwa kuongeza, hata rambirambi zinazochangwa kupitia ma-group ya mitandaoni nazo zinatozwa tozo.
Juzi nimewatumia hela ya sanda washikaji waliofiwa na babu yao nimeshangaa sana !
 
Back
Top Bottom