DOKEZO Ni kweli Hospitali ya Taifa Muhimbili kulala kwa siku ni gharama zake ni tsh 50,000?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Ngoja nikuelimishe kidogo

Hiyo gharama inachajiwa kama wewe umeenda pale bila rufaaa na ukienda bila rufaa unawekwa kwenye kundi la private client

Ukieenda na rufaa gharama zake nafuu hazipo ivyo kabisa ilo kundi linaitwa costsharing ambapo serikali inakuchangia gharama za matibabu

Ukienda nenda kiholehole lazima gharama ziwe juu
 
Nchi inaongozwa na kikundi cha wahuni.
 
Kulala yaahn kugeuza mgongo kulia na kushoto na kulala chali(kulalia mgongo) kwa masaa kadhaa kwa siku ni tsh 50,000 na kumbuka hiko kitanda ni kama vya boarding
 
Huna akili.
 
Kwanini gharama ziwe juu kwani huyo anakuwa sio mtanzania hakuna shule uliyonipa zaidi hizo ni hadaa tu za serikali.....mtu kazidiwa ghafla uanze kusbiri rufaa anadhani uhai ni sabani utaenda dukani kwa mangi ununue kama ikiisha.
 
Kulala yaahn kugeuza mgongo kulia na kushoto na kulala chali(kulalia mgongo) kwa masaa kadhaa kwa siku ni tsh 50,000 na kumbuka hiko kitanda ni kama vya boarding
Ofcourse haifai sababu bei hio sio affordable lakini sidhani kama watu wanakwenda hospitali ili walale bali ni zile huduma zinazopatikana sababu sidhani kama ukisema utasimama basi watakuchaji pesa ya sakafu.....

Anyway hii nchi sasa hivi watu hawana kabisa basic needs...
 
Mkuu kuna mtu anaumwa ugonjwa ambao inabid akae hospitali hata mienzi miwili na hapo ujue tatzo lake ni very kubwa operation za milion zimetumika mtu kama huyu huoni unamuumiza sana.....hapo ndugu lazima wakuchoke maana ruti za kuleta chakula plus gharama za matibabu sio powa.
 
Bima za kibongo ni utapeli mwengine kama wa michango ya NiFFA na watu wa kariakoo
ziko real mi nimewakatia watu wa familia na mmoja alikuwa na magonjwa ya muda mrefu gharama za matibabu nilishasahau kitambo sana. Tatizo tunapenda kubeza kila kitu. Hakuna tatizo kubwa kama kuwa anarchist, unakuwa unaishi kwenye denial state kila wakati huku wewe ndie unaeteseka!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…