Ni kweli kuwa Shaka ni mpwa wa Rais Samia? Na kama ni kweli CCM mmebariki nepotism hii ndani ya chama?

Hakuna sehemu yenye nepotism kama CHADEMA. Mwanzilishi wa Chama, Mtei, ni baba mkwe wa Mwenyekiti wa kudumu, Mbowe. Lema ni ndugu huko Machame. Lucy Owenya mtoto wa mmoja wa waanzilishi Ndesamburo. Wale Covid19 ukimtoa labda Mdee karibu wengine kama sio ndugu ni mke au kimada wa kiongozi. Yaani huko Ufipa balaa tupu. Fuatilieni. CHADEMA kuinyooshea kidole CCM kuhusu nepotism ni sawa na kuanzisha ugomvi wa mawe wakati wakiwa kwenye nyumba ya vioo.
 
Ridhiwani ni mtoto wa Kikwete rais mstaafu, Salma mama yake Riz1. Hussein ni mtoto wa mwinyi, Karume nao baba na mwana Marais. Sasa ajabu ya samia na Shaka iko wapi?
Mambo ya Ndugunaizeshen hayo tulikuwa tukisemaga zamani !! Pesa hazitoshagi ni tamaa kwa kwenda mbele mpaka siku ya mwisho !! Ambayo ipo tu na ni lazima ifike !!😅😅
 

Sexless ufahamu au ufuatiliaji wako ni mdogo sana kisiasa

Unasemaje uwezo wa Herí James umefikia mwisho ilhali kwasasa ni DC-Ubungo!??? Unafatilia mambo kweli au unakurupuka!??

Shaka alikuwemo kwenye siasa na kashika nyadhifa kadhaa ndani ya CCM na Serikalini kabla hii ya uenezi aliyoteuliwa na Samia

Pia, hili ukiliangalia kwa upande wetu huku Chadema ndio kuna nepotisms ya kiwango cha juu sana

Mbowe kapigiwa debe ya uenyekiti kutoka kwa baba mkwe Mzee Mtei,

Mbowe kazaa na Joyce Mukya kisha akaja akampigia debe ya ubunge viti maalumu.
Ndesamburo nae akamuweka mwanae Lucy ubunge viti maalum

Tundu Lissu nae hakubaki nyuma akampigia debe dada yake aitwae Christina Lissu awe Mbunge viti maalumu

Nenda kaangalie vyeo vingine vya kiutendaji ndani ya Chadema, uone kina John Mrema, Mallya, Tarimo nk walivyojazana chamani,,,, hapo utapata picha tuna upinzani/Chadema wenye taswira ipi
 
Mwenzio ameongelea uhalisia wewe unaongelea hisia. Eti sijui nani kampigia debe nani. Una uhakika wowote kuwa waluwapigia debe.

Mwenzio anaongelea kuhusu Samia kumteua Shaka kuwa Katibu mwenezi. Huo ni ukweli na ni uhalisia. Kitu kinachotakiwa kuthibitishwa, je, ni kweli kuwa Shaka ni mpwaa wa Samia?

Mjifunze namna ya kujenga hoja au kujibu hoja. Wewe unataka kulinganisha embe na pilipili.

Hivi kumteua mtu ni sawa na kumpigia debe? Una uhakika ulipwataja kama kweli waliwapigia debe watajwa? Hata kama ingekuwa ni kweli waliwapigia debe, hiyo inathibitisha kuwa wao wapiga debe siyo wa kuwafanya maamuzi. Maana yakewanawapigia debe kwa wafanya maamuzi. Rais Samia alimpigia debe Shaka kwa nani ili wafanye maamuzi? Hapa anazungumziwa kiongozi mfanya maamuzi kumbandika ndugu yake kwenye nafasi ya uongozi, tena mtu aliyekuwa amesimamishwa kazi kwa uhalifu wa kijinai.
 
Tatizo hujaelewa hoja, umekimbilia kujibu. Tulia, usome vizuri kabla ya kuchangia.
 
Mleta hoja kauliza kuhusu undugu kati ya wawili hawa.

Wewe unaongelea habari ya shaka kukulia CCM!

Jibu Swali acha blah blah!
 
Sioni tatizo, hakuna ubaya, shaka anaimudu kazi yake na anauzoefu nayo!, Anaifaa ccm.
 
Hakuna shida shaka kuwa mpwa wa Mama.....
 
Shaka alifukuzwa na Magufuli Kwa rushwa mbona huongelei
 
Tuwe tunajifunza kujibu maswali yanayoulizwa, hakuna asiejua historia yake ya siasa. Swali lilikuwa ni mpwa wa Rais?!
 
Wameanza kukiri wenyewe kuwa nchi inaongozwa na mbumbumbu
Your browser is not able to display this video.
 
Hiyo ni kweli wahuni wameshika hatamu ...mabeberu ya kizungu yanachekelea
 
Shaka yupo kwenye duru za CCM/ UVCCM kabla wewe hujaingia JF na kutengeneza account yako. Ni kwamba tu Mwendazake aliwavuruga mwaka 2016.
Hujajibu swali la msingi, na swali ni hili:
Je, Shaka ni "mpwa" wa Rais Samia??

Tupe jibu hilo halafu tuanzie hapo mjadala wetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…