Wapi kwenye Biblia panasema kuwa Wakristo wanakufa?Kama alitengua dhambi ya asili kwanini bado tunaendelea kufa? na kuteseka? kama kale?
Wapi kwenye Biblia panasema kuwa Wakristo wanakufa?
Wewe sio mwili na nyama na damu bali wee ni Roho inayo ishi kwenye Mwili na nyama. Labda hukulifahamu hilo. Roho yako ambayo ni wewe haifi bali unatoka tu kwenye mwili na nyama na damu na kwenda sehemu nyingine.
Exhibit:
2 Corinthians 5: 8 We are confident, I say, and willing rather to be absent from the body, and to be present with the Lord.
Kwanza kabisa umeonyesha udhaifu mkubwa sana na ukosefu wa ufahamu wa nini kilitokea hapo mwanzo.
1. Ailye ambiwa asile tunda ni Adam na sio Hawa kama ulivyo sema hapo juu.
2. Hawa aka Eve alipo kula tunda, hakuna kilicho tokea na mambo bado yalikuwa shwari, hili hukulifahamu.
3. Alipo kula tunda Adam ndio macho yao wote wawili yalifunguka na kujiona wapo uchi.
4. Mungu alipo kuja chini alimuuliza Adam, nani kakwambia upo uchi na sio Eva.
5. Adam mbavu yake ndio iliyo muumba Eva. Hivyo basi.......
6. Adam kwa kuwa ndie aliye tumiwa kutengeneza Eva, hiyo ndio sababu ya dhambi kufuta binadamu kwasababu ya asili yetu ni Adam.
7. Wewe unashangaa kwanini dhambi aliyo fanya Adam ikufuate lakini haushangai kwanini DNA yako na baba yako zinashabihana.
8. Wewe unashangaa kwanini Adam dhambi yake ikufuate lakini haushangai kwanini mtu mwenye Ukimwi akikuingiza damu yake na wewe unapata ukimwi. Your blood is Adamic.
9. You need the blood of Jesus to nullify the corrupted blood of Adam.
10. Ndio maana huwezi kwenda Mbinguni bila ya kutumia damu ya Yesu.
11. Kumbe basi the second Adam ndie alikuja kutengua ile dhambi ya asili.
12. Bila ya Yesu Mungu, weye huendi Mbinguni bali Jehannam inakungoja.
YESU NI MUNGU MKUU
Kwanza kabisa umeonyesha udhaifu mkubwa sana na ukosefu wa ufahamu wa nini kilitokea hapo mwanzo.
ya asili yetu ni Adam.
7. Wewe unashangaa kwanini dhambi aliyo fanya Adam ikufuate lakini haushangai kwanini DNA yako na baba yako zinashabihana.
8. Wewe unashangaa kwanini Adam dhambi yake ikufuate lakini haushangai kwanini mtu mwenye Ukimwi akikuingiza damu yake na wewe unapata ukimwi. Your blood is Adamic.
9. You need the blood of Jesus to nullify the corrupted blood of Adam.
10. Ndio maana huwezi kwenda Mbinguni bila ya kutumia damu ya Yesu.
11. Kumbe basi the second Adam ndie alikuja kutengua ile dhambi ya asili.
12. Bila ya Yesu Mungu, weye huendi Mbinguni bali Jehannam inakungoja.
YESU NI MUNGU MKUU
Upendo na kunyesha kwa kumvua kuna uhusiano gani hapa? Jifunze kufikiria kijana. Zaidi ya hapo, wewe unalinganisha "Upendo" na "kuamini".
IN BLUE:
1. Kwanini Mungu alimtuma Mwanae?
2. Kwanini Mwanae ilibidi afe?
3. Kwanini Mwanae na sio Malaika?
4. Kuokoka kutokea nini na au wapi?
5. Kwanini watu wokoke?
Hii mada ni pasua kichwa
Kamwe haitakuja kueleweka kwa watu mpaka watu wawe na elimu ya tauhid
Unamaanisha nini mkuu?
Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote hayuko consistent na ulimwengu ambao una kutandikana, kwa sababu alikuwa na kila uwezo, ujuzi na upendo kuumba ulimwengu ambao hauwezekani habari za kutandikana.
Kuwezekana kuwepo kutandikana kunaonesha ulimwengu huu haujaumbwa na mungu huyo.
Kabla ya kusema sana kuhusu mungu, thibitisha kwamba yupo.
Ama sivyo sema unapiga hadithi za kusadikika zisizo na haja ya kuthibitishwa.
Mkuu, na kiswali kidogo kwako sasa Mungu akifa hii dunia yake alioiumba anamuachia nana?
Unapokurupuka tu kutoka huko vuuu na kuja kuandika maelezo bila hata kusoma mada inahusu nini na inaongelea mambo gani unakuwa hujajitendea haki wewe mwenyewe na wale ambao watakusoma
Mada yangu inahusu mambo mawili
1; Vile ambavyo uwepo wa ulimwengu huu ulivyo matokeo ya upendo wake Mungu
2; Ushahidi kwamba Mungu wa kwenye bibia ni Mungu na anathibitisha kwamba anaweza kuwa hakimu wa haki na Mungu wa huruma hapo hapo
Unaweza kuona kwamba hoja yako inajibiwa kwenye mada,nenda kasome kisha uje ujenge hoja kutokana na mada na sio nje ya mada
Ukija na maelezo ambayo yapo nje ya mada sitajisumbua kukujibu!
Bwana wewe Eiyer! kwani wewe ndo Adamu? unahusika vipi kwa kosa walilofanya Kina Adamu na Hawa wastani wa miaka 6000 iliyopita? Ulikuwepo kwenye makubaliano ya Adam, Hawa na Mungu? Ulikuwepo wakati Adamu na Hawa wanakula Tunda? Mwanafunzi shule akikosa huwa anachapwa na kupewa adhabu yeye kama yeye lini ulishaona anachapwa mwanafunzi kwa kosa alilofanya yeye mwenyewe kisha mchapaji/mwalimu anaanza kuwatafuta na ndugu zake wa huyo aliyekosea awachape na kuwapa adhabu!? ili hali waliofanya makubaliano ya kuwa hili ni kosa na ukikosa nitakuchapa ni kati ya mwalimu na Mwanafunzi!, na ndugu wengine walikuwa hawapo hapo kwenye hayo makubaliano. Ile adhabu kama hadi sasa ingekuwa inawapata kina Adam na mwenzake Hawa ingekuwa ni sawa sababu hilo kosa linawahusu wao wenyewe, na walishaonywa ila hawakusikia huenda hata wewe Eiyer ungekuwa Adam ungekataa kula lile Tunda? sasa utajisikiaje Baba yako aibe Ng'ombe huko kijijini kisha wananchi wenye hasira kali wamchome moto yeye, kisha wafunge safari kukufuata wewe mjini na kisha kukuchoma moto wewe na watoto wako na mke wako?
Yesu alifundisha kwa mifano mimi nadhani utanielewa.
Umekuwa ukitumia "immanent critique" ili kupinga uwepo wa Mungu,hapa naona umeamua kuitupilia mbali,hueleweki kabisa uko wapi na unasimamia msingi upi kujengea hja zako
Kama unataka mtu akuthibitishie uwepo wa Mungu acha kutumia immanent critique and vise vesa
Mada yangu inajibu hoja zenu kwa kutumia hiyo hiyo immanent critique yenu na unapaswa ubakie humo humo na sio kutoka nje,kama unataka uthibitisho wa uwepo wa Mungu baki huko huko bila kuchanganya mambo
Lakini pia hiyo immanent critique yako kwa mtu kama wewe ambae unakana uwepo wa Mungu haikufai kabisa kwasababu haitetei kutkuwepo kwa Mungu bali inaacha mlango wa uwezekano wa Mungu kuwepo
Immanent critique inachallenge sifa za Mungu anaesemwa kwenye biblia kama kweli kaumba ulimwengu huu kwasababu ya namna ulivyo,kama kweli itaonekana kwa sifa zake haiwezekani kuumbwa nae hiyo haitakuwa na maana kwamba hakuna Mungu bali itaonekana Mungu mwenye sifa kama hizo atakuwa hajaiumba dunia na inawezekana kuna mungu mwenye sifa nyingine kaumba hii dunia
Kwa maana hiyo immanent critique haikubaliani na dhana ya kutokuwepo kwa Mungu bali kinyume chake!
Kwa nini nisitumie immanent critique kama itanifikisha katika ukweli?
Hata katika kusolve mathematical equations kuna "Let a = b".
Nikianza uchunguzi wangu kuhusu kuwapo kwa mungu kwa kusema.
"Let "god exists" = true"
"Let "god is all powerful"= true"
"Let "god is all loving" = true"
"Let "god is all capable" = true
"Let "god created the universe" = true"
Then why this all loving, all powerful and all capable hodhead create a universe in which evil is possible while he could have created one in which evil is not possible?
Tunaanza na huyo mungu wa kwenye biblia (na quran na dini nyingine nyingi by the way) mwenye sifa hizo kwanza.
Unakubali kwamba huyu mungu ni wa maboksi?
Ukiahakubali hilo tutaenda huko kwingine, lakini kubali hili kwanza. Kwamba huyo mungu wa biblia uliyemtaja ni wa maboksi.
Halafu utasemaje immanent critique haikubaliani na dhana ya kutokuwepo kwa mungu bali kinyume chake wakati dhana yoyote, ikiwemo ya kuwepo kwa mungu yeyote, inaweza kupigwa immanent critique.
Wewe kweli unaelewa immanent critique ni nini au una parrot ninachoandika hapa tu?
Immanent critique haikubaliani na dhana ya kuwepo Mungu kama nilivyokwisha kusema kwamba inaacha mlango wa kuwepo mungu mwingine,kwasababu hiyo kama itakuja dini nyingine ambayo itatengeneza dhana yake kulingana na madai yako na namna dunia ilivyo,hii inamaana hutatumia immanent critique tena maana yake itakuwa imefeli hapo,utataka mtu akupe uthibitisho wa uwepo wa huyo mungu
Na kufikia hapo utakuwa huna nyimbi nyingine tofauti na hiyo na wewe utadaiwa ushahidi wa madai yako
Pamoja na hayo yote,hapa kwenye mada hii unajenga hoja yako nje ya immanent critique au unaitumia?