Unajua hizi propaganda zenu dhidi ya wanawake nazifananisha na zile za mtu mweupe dhidi ya mtu mweusi, sasa hapa usiseme nimetoka nje ya mada bali nakupa mfano hai na halisi ili uone ni namna gani hii mifumo inavyo operate kwenye hii dunia hivyo soma ili uelewe siyo ili mradi tu ubishe, kwa miaka mingi watu weupe wamekuwa wakitutawala watu weusi na kutuaminisha kwamba hiyo ni nature wao weupe waliumbwa kututawala weusi kwa sababu ndio wana akili na maarifa kuliko weusi, na wanadai hii iko kibiblia kabisa (refer kwa watoto wa Nuhu ambao ni Shem, Ham na Jafet), baada ya kututawala na kutunyanyasa kwa miaka mingi baadaye tukaanza kudai uhuru na haki na hatimaye wakatupa, lakini unaona hadi leo jinsi wanavyotusakama kwamba bado hatuwezi kujitawala bora tungewaacha tu waendelee kututawala
Yani kila tunapokosea wanatusema kwamba sisi bado hatujitambui na hatuna akili wala uwezo ndio maana nchi zetu bado ni masikini na viongozi wetu ni wala rushwa na kila kukicha wanapishana angani kuenda kuomba mikopo na misaada kwao hivyo kuwafanya waendelee kututawala katika mfumo wa ukoloni mamboleo, yani bado wanaeneza propaganda zao kwamba mtu mweusi akiachwa ajifanyie mambo yake mwenyewe ataharibu na atakuwa threat kwa ustawi wa dunia hivyo anatakiwa asaidiwe na aendelee kutawaliwa, wanacheza na saikolojia zetu kutufanya tusijiamini na kuona kweli hatuwezi ili mradi tu tuendelee kujiona tunawahitaji wao kwa sababu tumeishia kudwell kwenye hizo propaganda zao na lengo lao la kuendelea kututawala kama zamani lifanikiwe, lakini je pamoja na hayo yote mbona waafrika hatujaacha kupambania uhuru wetu na haki zetu na kila kukicha tunatafuta namna ya kuwadhihirishia kuwa tunaweza bila wao kwanini tusisalimu tu amri na kukubali kuendelea kuwa chini yao, maana ukiangalia yote wanayosema ni ukweli kuhusu sisi kuwa masikini na kuwa na utawala mbovu lakini sidhani kama ni kweli kwamba hatuwezi kabisa kujitawala na pia sidhani kama hiyo ni sababu ya kuwaruhusu wao waendelee kututawala
Ni vile tu hawatupi room ya kuimprove wanaangalia mabaya yetu tu ila mazuri yetu wanajifanya hawayaoni na wakiyaona wanadai wao ndio wamechangia kwenye hayo mazuri yetu, yani mtu anakupa uhuru wa mchongo huku hapo hapo anakusakama halafu ukifeli katika hali ya kawaida tu ya kibinadamu anakimbilia kusema nilijua tu atashindwa hawezi kushindana na mimi bado ananihitaji ndio maana bado anakuja kuomba msaada kwangu, sasa ilete hiyo katika huu mfumo wa mwanaume kumtawala mwanamke kisha utaelewa namna hii mifumo inavyofanya kazi, halafu nakuuliza je kufeli kwa wanawake ambako ni kawaida kibinadamu ni kweli sababu ni kwamba hawawezi au ni kwamba bado wamedwell kwenye propaganda za wanaume maana kama ni kufeli hata wanaume wengi tu wanafeli na haionekani tatizo, ila akifeli mwanamke inaonekana amefeli sababu ya uanamke wake kwahiyo je kufeli kwa wanawake ndio kunajustify kwamba bila wanaume hawawezi hivyo waendelee tu kujisubmit kwao hadi mwisho wa dahari hata kama hawafurahii kufanya hivo