Ni lini adui wa mwanamke akawa mwanaume


Anapenda kubisha ila ukimwambia anakwambia una muattack personally na haulengi mada. [emoji23]

Hebu achana na hii defensive mechanism yako haikusaidii kitu zaidi ya kukufanya ujifariji tu ili uonekane una hoja, mnajadili hoja zinazozalisha maswali mengi kuliko majibu halafu mkiulizwa hayo maswali mnakimbilia kusema fulani anajadili hoja kwa kuhamahama, mnajenga hoja zenu based on social constructs mnasingizia nature halafu mnataka tukubali kwa madai kwamba huo ndio uhalisia, na tukihoji msingi wa huo uhalisia mnadai tunabishana ili tushinde, kwa kifupi hoja zenu zinalazimisha tu ile kauli ya "it is what it is so bear with it"
 
Mwanamke kuwa na uchumi mzuri ni jambo jema.
Tukisema mwanamke hatumaanishi mtu kutoka mbali , kila mwanaume alipo Kuna mwanamke.
Mwanamke ni dada yako, ni Binti, mke, mama, shangazi ambao hao ndo wanawake hata ukigeuka unawaona.
Kwa mfano me nataka Binti yangu, dada yangu , shangazi, rafiki wafanikiwe kielimu na kiuchumi.
Tatizo ni hizi NGOs zinazoleta uadui wa usawa ambao ni vitu vipo wala havigombaniwi na mwanamke kumuonya kila mwanaume ni adui jambo ambalo sio kweli.
Nenda mahakamani au police uone akili za ovyo za baadhi ya madhara ya elimu ya usawa.
Sasa mnataka usawa wa kuvaa suruali mmepewa, usawa wa madaraka mmepewa, kibiashara mmepewa,
Sasa why wengi wana fail
 
Mkuu jisemee wewe usiwasemee wanaume wenzio wanaume wengi bado wanapambana kwa nguvu zote kuhakikisha 50/50 inakufa ili turudi kwenye absolute Mfumo dume, hii inawafanya wanawake nao wazidi kuongeza nguvu kuupambania huu mfumo wa haki sawa ili usiangushwe na ndio hapo mwanamke anapoonekana anapambana na mwanaume, kuhusu wanawake kupewa usawa walioutaka na kufail naona kama imekaa kipropaganda zaidi kuliko kiuhalisia kwani mbona wanaume wengi wanafail ila jamii haioni tatizo ila mwanamke akifail inaonekana amefail kwa sababu ya uanamke wake
 
Haki sawa zipi ambazo mwanamke hapewi?
Na anazidai Kwa nani?
Na mwanamke akizipata hizo haki itakuwaje?
Ni nani mtesaji wa hawa mama, wake zetu, Binti zetu, shangazi, bibi, n.k?
 
Mkuu haya unayaongea yanafanyika kwenye jamii ipi? maana mimi sijawahi kuona semina au kongamano la wanaume wanaoongelea haya mambo ya 50/50 isipokua ni wanawake tu ndio wanafanya ivyo hata marais wanaume tuliowahi kuwa nao sijawahi kuona ambae anaongelea mambo ya jinsia ila mama samia mara kipindi cha mwanzo cha uongozi wake mara kadhaa ashatoa kauli za kifeminia. Sasa hii ya kusema wanaume wanapambana kurudisha mfumo dume unaitoa wapi mkuu.
 
kuhusu wanawake kupewa usawa walioutaka na kufail naona kama imekaa kipropaganda zaidi kuliko kiuhalisia kwani mbona wanaume wengi wanafail ila jamii haioni tatizo ila mwanamke akifail inaonekana amefail kwa sababu ya uanamke wake
Mwanaume akianzisha mradi anaupambania yeye mwenyewe kufa na kupona ila wanawake wengi huwa wanafeli biashara nyingi za wanawake zinaiingiza hasara ila zina-survive kwa kupewa burst na wanaume either waume zao au madanga. Angalia field yoyote ambayo haihusishi utofauti wa kijinsia angalia top elites idadi kubwa ni ipi kati ya wanaume na wanawake.
 
Haki sawa zipi ambazo mwanamke hapewi?
Na anazidai Kwa nani?
Na mwanamke akizipata hizo haki itakuwaje?
Ni nani mtesaji wa hawa mama, wake zetu, Binti zetu, shangazi, bibi, n.k?
So unadhani wanawake walitoka tu out of blue na kuanza kudai haki sawa bila kuwa na sababu yoyote, ofcourse wanazidai hizo haki toka kwa wanaume sasa wewe ulitaka wazidai toka kwa nani kwani mfumo dume ulitengenezwa na nani, wanaume ndio watesaji wa wanawake na hawamaanishi wanaume wote bali baadhi ambao walishindwa kutumia mfumo dume vizuri
 
Yani unataka hadi wanaume waandae semina au makongamano ndio ujue kwamba wanapinga mfumo wa haki sawa, kwani humu mitandaoni huoni namna wanavyopinga ukiwemo wewe au hujui impact ya mitandao kwenye dunia ya leo ambayo globalization ime takeover, aliyekuambia kwamba siku hizi njia pekee ya kuaddress kila global issue ni kuandaa semina na makongamano tu ni nani
 
Ndio maana mwanzo nikakuambia haujaelewa mada. Hatukatai usawa hatukatai mwanamke kujitengenezea kipato shida inakuja pale anapotaka kuuvaa uanaume kwenye jamii au ndani ya nyumba hapo ndipo hakuna mwanaume timamu atakubaliana napo
 
Hata mitandaoni bado wanawake wanaoamasisha ufeminia ni wengi ukilinganisha na wanaume wanatetea mfumo dume. Kwa haraka mimi naweza kukutajia Mange kimangi, Flavian Matata, Joyce Kiria, Fatma Karume hawa ni waamasishaji wa ufeminia naomba nitajie baadhi ya wanaume public figure wanaotetea mfumo dume. Kuhusu mtazamo wangu mimi kuhusiana na 50/50 ni wewe ndio huwa haunielewi mimi sipingi usawa napinga unafiki wa kuji-position kwa kuangalia masilahi kama unataka usawa basi tu-apply usawa kwenye kila kitu for once and for all sio huu unafiki ukijimudu kiuchumi unkua feminist ukiwa broke unakua submisive ili uhudumiwe
 
Haki zipi zitaje ?
Yaani wewe unaamini baba yako anakunyima haki anakudhulumu, kaka yako hakutakii mema, mjomba wako hataki uwe na uchumi mzuri.
Mfumo dume ukoje? Uko wapi?
Kwaiyo NGOS zinakuja zilete fujo dhidi ya mfumo dume usiokuwepo.
Mnataka Nini Kwa wanaume? Wanawake wamekuwa mawaziri hadi Sasa Rais lakini Bado wanaamini Kuna mfumo dume?
Mnataka wanaume wakojoe wamechumaa au vip?
Mnataka Nini usawa upo?
Tuache chokochoko za ovyo.
Mwanamke ni mwanamke na itabaki ivo.
Na mwanaume ni mwanaume, usawa au hauwezi kuwepo tupo tofauti sana, hiyo ni nature.
Tuko tofauti kimabile, kiakili, uwezo, nguvu,
Tukubali na league iishe usawa ni never.
 
Unajua hizi propaganda zenu dhidi ya wanawake nazifananisha na zile za mtu mweupe dhidi ya mtu mweusi, sasa hapa usiseme nimetoka nje ya mada bali nakupa mfano hai na halisi ili uone ni namna gani hii mifumo inavyo operate kwenye hii dunia hivyo soma ili uelewe siyo ili mradi tu ubishe, kwa miaka mingi watu weupe wamekuwa wakitutawala watu weusi na kutuaminisha kwamba hiyo ni nature wao weupe waliumbwa kututawala weusi kwa sababu ndio wana akili na maarifa kuliko weusi, na wanadai hii iko kibiblia kabisa (refer kwa watoto wa Nuhu ambao ni Shem, Ham na Jafet), baada ya kututawala na kutunyanyasa kwa miaka mingi baadaye tukaanza kudai uhuru na haki na hatimaye wakatupa, lakini unaona hadi leo jinsi wanavyotusakama kwamba bado hatuwezi kujitawala bora tungewaacha tu waendelee kututawala

Yani kila tunapokosea wanatusema kwamba sisi bado hatujitambui na hatuna akili wala uwezo ndio maana nchi zetu bado ni masikini na viongozi wetu ni wala rushwa na kila kukicha wanapishana angani kuenda kuomba mikopo na misaada kwao hivyo kuwafanya waendelee kututawala katika mfumo wa ukoloni mamboleo, yani bado wanaeneza propaganda zao kwamba mtu mweusi akiachwa ajifanyie mambo yake mwenyewe ataharibu na atakuwa threat kwa ustawi wa dunia hivyo anatakiwa asaidiwe na aendelee kutawaliwa, wanacheza na saikolojia zetu kutufanya tusijiamini na kuona kweli hatuwezi ili mradi tu tuendelee kujiona tunawahitaji wao kwa sababu tumeishia kudwell kwenye hizo propaganda zao na lengo lao la kuendelea kututawala kama zamani lifanikiwe, lakini je pamoja na hayo yote mbona waafrika hatujaacha kupambania uhuru wetu na haki zetu na kila kukicha tunatafuta namna ya kuwadhihirishia kuwa tunaweza bila wao kwanini tusisalimu tu amri na kukubali kuendelea kuwa chini yao, maana ukiangalia yote wanayosema ni ukweli kuhusu sisi kuwa masikini na kuwa na utawala mbovu lakini sidhani kama ni kweli kwamba hatuwezi kabisa kujitawala na pia sidhani kama hiyo ni sababu ya kuwaruhusu wao waendelee kututawala

Ni vile tu hawatupi room ya kuimprove wanaangalia mabaya yetu tu ila mazuri yetu wanajifanya hawayaoni na wakiyaona wanadai wao ndio wamechangia kwenye hayo mazuri yetu, yani mtu anakupa uhuru wa mchongo huku hapo hapo anakusakama halafu ukifeli katika hali ya kawaida tu ya kibinadamu anakimbilia kusema nilijua tu atashindwa hawezi kushindana na mimi bado ananihitaji ndio maana bado anakuja kuomba msaada kwangu, sasa ilete hiyo katika huu mfumo wa mwanaume kumtawala mwanamke kisha utaelewa namna hii mifumo inavyofanya kazi, halafu nakuuliza je kufeli kwa wanawake ambako ni kawaida kibinadamu ni kweli sababu ni kwamba hawawezi au ni kwamba bado wamedwell kwenye propaganda za wanaume maana kama ni kufeli hata wanaume wengi tu wanafeli na haionekani tatizo, ila akifeli mwanamke inaonekana amefeli sababu ya uanamke wake kwahiyo je kufeli kwa wanawake ndio kunajustify kwamba bila wanaume hawawezi hivyo waendelee tu kujisubmit kwao hadi mwisho wa dahari hata kama hawafurahii kufanya hivo
 
Maelezo marefu siwezi kusoma hayo. Wewe kama unataka usawa basi tu-apply usawa kwenye kila kitu kinachotukutanisha kiwe sex tu. Kila mmoja anakaa kwake kila mmoja anawajibika kujihudumia mwenyewe ukija geto kwangu unatombwa unasepa nikija kwako nakutomba nasepa hakuna mambo ya kubebeshana gharama za nauli wala matunzo. Tukilala lodge au tukitoka out gharama zote zinaganywa 50/50.
 
Ndio maana mwanzo nikakuambia haujaelewa mada. Hatukatai usawa hatukatai mwanamke kujitengenezea kipato shida inakuja pale anapotaka kuuvaa uanaume kwenye jamii au ndani ya nyumba hapo ndipo hakuna mwanaume timamu atakubaliana napo
Kuuvaa uanaume ndiyo kukoje huko hebu kuelezee
Wewe una mifano ya wanawake wangapi ambao wakipata mafanikio wanakuwa feminists ila wakiwa broke wanakuwa submissive, una uhakika gani kwamba hao feminists ndio hao hao wanaobadilika na kuwa submissive kulingana na hali zao za kiuchumi hebu tujadili uhalisia siyo mtazamo wako binafsi, kuhusu majukumu nimeshaongea na wewe sana kuhusu hili ila kila siku unarudia yale yale nilishakuambia siku mkikubali kufanya majukumu yote mnayoyaita ya mwanamke na kuyachukulia kama yenu basi hata wanawake wataanza kufanya yenu na kuchukulia kama ya kwao
Na ndio hiki nilichokuwa nasema kwamba mnajenga hoja zenu based on social constructs halafu mnasingizia eti nature na mkiulizwa msingi wa hiyo nature yenu mnadai tunapingana na uhalisia, hivi kwanini unalazimisha kumtawala kiumbe mwenye utashi kama wewe yani unalazimisha kumtawala kwa misingi gani hiyo ambayo inashindwa kubadilika kulingana na wakati na mazingira, na kwanini wanaume ndio muamue kipi kinachowafurahisha wanawake na kipi kinachowaumiza kwanini mnawasemea, kama wao wanawake wanaona kwamba kuwa chini ya wanaume kunawapa maumivu zaidi kuliko kujitawala wenyewe kwanini ninyi mnapinga, na kuwalazimisha waone kwamba kuwa chini yenu ndio kunawapa furaha zaidi kuliko kujitawala wenyewe kwani mmewashikia akili kwamba wao hawawezi kuamua ni lipi linaloleta furaha na lipi linaloleta huzuni kwao
 
Wewe una mifano ya wanawake wangapi ambao wakipata mafanikio wanakuwa feminists ila wakiwa broke wanakuwa submissive,
Christina shusho, joyce kiria n.k.. nawe nitajie hao wanaume wanatetea mfumo dume mitandaoni ambao kwa mujibu wako unasema ni wengi kuliko wanawake
 
Umelinganisha ubaguzi wa rangi (race discrimination) na mfadhaiko wa kijinsia (gender dysphoria).

Swala na wazungu kubagua waafrika ni swala la kibaguzi of which haki na maslahi hayana mashiko na rangi bali haki ya kimsingi ya kibinadamu.

Mtu mweupe akiachana na mwafrika na wasiingiliane hakuna kitakacho haribika kwasababu watu weusi wataendelea kudominate dunia, watazaliana kwa wingi na kutengeneza political space ya watu weusi na hatimae kustawi na kuwa superior race sababu watajanga system zao.

Haya tugawane mabara hapa. Feminists mpewe bara lenu mtengeneze Utopian state ya feminists, mtatoboa?

Mtajipiga miti wenyewe, mtazaliana vipi, nani atakuwa mama na nani atakuwa baba, nani atasimamia nje ya nyumba nani atasimamia ndani ya nyumba?

Hivi unajua recently Feminism imeanza kuwa. Classified kama mental health issue? [emoji848]

Huko magharibi 3rd wave feminism propaganda imekuwa associated na gender dysphoria issues kama ushoga, transsexualism, mental issues kama depression, suicides, devorce, low birth rate etc.

Why wewe unahisi upo sahihi sana kusapoti ujinga kama kama huu halafu unataka uonekane ni mwanamke unayoitakia mema jamii yako? [emoji848]
 
Ukiachilia mbali kuzaa na kunyonyesha majukumu ambayo kibailojia wanaume hatuyawezi majukumu mengine ya nyumbani yote huwa tunawasaidia wapenzi wetu kama muda unaruhusu.
 
We sema tu unataka kukwepa hoja hayo maelezo yana urefu gani wewe mara ngapi tunakutanaga kwenye mijadala kama hii, naandikaga magazeti marefu zaidi ya hilo na unasoma na kujibu magazeti ambayo nami huwa nayasoma pia halafu leo unasema huwezi kusoma, kama huwezi kusoma maelezo yangu basi haina haja ya kuniquote maana inapoteza maana nzima ya huu mjadala hayo mengi yote uliyoandika hapo nafikiri kuna comment ina majibu yake
 
Me naomba siku tukutane Twitter space, halafu ujenge hoja zako vema, haya yote tunayoongea tuyapeleke kule tuongee man to man halafu tuone ukijenga hoja zako kwa kinywa, unasemaje? [emoji848]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…